Black Rose,
haki ninayoisema hapa, ni kwakuwa Waislam ni significant portion ya Wananchi wa Tanzania, wanavuja jasho na kuilipa kodi serikali, basi wana haki ya kugharimiwa kwa kiasi fulani katika shughuli zao za kijamii Kama wanavyofanyiwa wakristo wanaopewa mabillioni yatokanayo na kodi zetu sote, kwani hoja kuu ya Wakristo kukataa Mahakama hii ni kigezo cha gharama, as if kodi zote za serikali zinalipwa na Wakristo peke yao. Tukisema tuhoji uhalali wa mapato ya serikali, basi tutadumaa, kwa maana itabidi Waislam itabidi wote waache kazi serikalini, Kwa maana mishahara yao inatokana na vyanzo visivyo halali, tukatae huduma zote za serkali kwa sababu vyanzo vya mapato yake vingine si halali. Ndiposa nikahoji kwani sadaka na michango yote ya kuendesha na kujenga misikiti uhalali wake tunaujua? Kwa kuwa nchi yetu Ina interaction ya dini mbalimbali, basi Allah ni mwenye kuelewa zaidi na ni mwingi wa kusamehe na wala si mwenye kuikalifisha nafsi ila kwa jambo inaloliweza, na atatuhukumu kwa dhamira zetu na wala si kwa udhaifu wetu tu. Nia ya kutaka serkali igharimie kwa kiasi fulani ni kutaka kupunguza uzito wa gharama kwa watakaohitaji haki zao katika mahakama hiyo, hasa wanawake, waweze kuipata kwa gharama ndogo, hivi kweli BR huwaoni wajane walioolewa ndoa za kiislam wakafiwa na Waume zao wanavyodhulumiwa kwa kufukuzwa majumbani mwao, wakanyang'anywa kila kitu, wanatelekezwa na watoto mayatima, ndugu za mume wanafanya hivyo kwa kisingizio cha mila na desturi, State Courts ziko so corrupted asipokuwa na fedha za kutosha hataambulia kitu. Haki za mjane wa Kiislamu ni nyingi sana, sio ile thumni peke yake, bali inaanzia kwa Mali alizopewa na mumewe enzi ya uhai wake, maskani yake katika nyumba aliyoishi na mumewe, sustainance yake kipindi cha eda, custody ya wanawe aliozaa na marehemu, haki za wanawe ambao bado ni wadogo kujimiliki wenyewe nk nk, it's a very complex issue, state laws zilizopo hazikuSubstanciate haki hizi, badili yake zimeImply tu kuwa sheria za ndoa na mirathi za Kiislam zikubalike kwa waumini wake, matokeo ni kuwa Mahakimu wengi hawazijui sheria hizo, wengi wanaishia kutumia state laws pekee, na hivyo kuwakosesha haki waislam wengi, wake kwa waume, ndo maana ikadaiwa mahakama ya kadhi.