Ndoa ndoano, nimepoteza kipato mke wangu kaanza kunidharau

Ndoa ndoano, nimepoteza kipato mke wangu kaanza kunidharau

Very sad🥲🥲🥲 huwezi amini rafiki yangu demu wake wameishi mwaka wa kwanza mpaka wa tatu alikuwa wanatokea mkoa mmoja huko chuga
Mbaya baada ya chuo jamaa kapotea kweny ramani ajira hamna kodi inamshinda akiwa anatafakari alipata dili moja jamaa ni mtaalamu sana wa website sijui ufundi anao kichwani akapata Kama mil 3 akasema nusu anampa demu ajiendeshe kibiashara nusu yeye ili wasaidiane

Akiwa anatafakari hela ipo na tabasamu lisharudi anapokea mwaliko kuwa demu wake anataka kuolewa na jamaa anapiga kazi TRA kamuuliza demu demu kamkana eti hamjui kingine demu alitoa mimba ya mshkaji hapo kati

Jamaa hana mood ni mda tangu mwezi wa kwanza na demu bado anaishi na jamaa anakaa kigogo hapo jamaa kakutana nae mara mbili basi roho inamuuma demu ana kimimba cha jamaa alitaka kujiua nikamshauri asepe dar es salaam karudi chuga yuko town anakula pamba anashusha belo za mtumba anashika parefu mitupio ya maana miezi minne tu anaroll na wazungu maana ana dili za utalii pia ..

Bro move on sorry ndo dunia
 
Nime ufeel uchungu wako... hahahah...
Samaki, kuku, Nyama, mama vitakupa faraja...
Mie nimefeel uchungu wa mtoa mada 😂😂😂

Mtoa mada kuna comment kasema wife kamjibu mbovu kisa apechalolo.. na mm si ndio nimesema ‘wakome kutanguliza hela? 🤔 🧐

Umewataja hao samaki na mimi naanza kweli kufeel uchungu 😜😜
 
Kabla ya mamb kuyumba ulikua una mshirikish mishe zako ? Kam jibu sio bas hapo ndipo umeyumba
Lakini hawa Viumbe hawana jema mkuu! Na hasa wa hiki kizazi cha HAKI SAWA.

Ila pia, kama mwanzo na msingi wa mahusiano ulikuwa ni fedha kwa asilimia kubwa, hakuna namna, ndivyo wanavyokosa(ga) uvumilivu hivyo.

Muhudumie kwa kila kitu kwa miaka dahali, ikiwa ni pamoja na kumfungulia mabiashara. Yumba ukae idle kwa miezi 3 mfululizo uone!
 
Mie nimefeel uchungu wa mtoa mada 😂😂😂

Mtoa mada kuna comment kasema wife kamjibu mbovu kisa apechalolo.. na mm si ndio nimesema ‘wakome kutanguliza hela? 🤔 🧐

Umewataja hao samaki na mimi naanza kweli kufeel uchungu 😜😜
Ndiyo maana nikampa muongozo kwamba, hata kama unazo siku zingine awe anamkazia hana, siku zingine anamlegezea anampa, wataenda sawa...

Njoo uchukue upunguze machungu yako...
 
Utasikia wale jamaa tafuta hela. Hela haikupi true love amini hilo

Shida yetu sisi wanaume tunafikiri ukiwa na hela unaweza kuwa na mwanamke yoyote na hapo ndipo unapoangukia kwa slay queen kwasababu ya uzuri wao.

Unaona kabisa huyu mwanamke kila muda anapiga vizinga haipiti siku 3 anaomba mpk kilo 2 kwa vile una hela unatoa toa tu na haya ndiyo matokeo yake.

Kuna kufukuzwa kazi, biashara kuyumba, matatizo ya kiafya n.k km umeoa mwanamke anayekupenda utakuwa naye kipindi chote.

Kuna watu wanaishi maisha ya kuungaunga lakini wanafurahia ndoa zao.

Maumivu ya kudharauliwa yanauma sana ukute lijitu ulilihangaikia kulilisha, kuliuguza na kulivalisha.

Pole sana. Jifanye kupotezea, angalia wapi unaweza kurudi kwenye mishe zako. Ukirudi mchukulie kama beki 3 na endelea na maisha yako.

Asante sana,Yan skuiz najibishwa hovyo, naonekana sio mwanaume. Daaah

Kunamda nataman kumpasua nikaozee jela maana kujiua siwez
 
Kipimo cha upendo huanzia kwenye misukosuko kama hiyo mojawapo.

Je ataendelea kukupenda na kukupa faraja na heshima hata pale ambapo unakuwa huna mbele wala nyuma?

Na hapo hata tendo sijui kama unapewa na appetite yako ukute imekata kwa muda au siyo?!

Pole mwaya, tafuta vibarua usichague kazi huku ukimuomba Mungu atafungua njia.
 
Halafu ukute ulivyokuwa na kipato ulikuwa hushikiki kwa michepuko,

Sasa umefulia ndio unakuwa mzigo kwa mkeo na familia huwa inaumaga.

Hapo sasa mke ndipo anatakiwa kuishi Kwa imani bila kukuongezea stress maana ulozinazo zinatosha.

Maana mwingine anaku-enjoy tu kwa kukukwambia vipi mahawara zako bado mnawasiliana?

Waambie wakusaidie hela ya kula au Ada ya mtoto!
 
Wakati una kipato chako heshima na utii huwa unaonekana, ukipoteza kipato ndio utajua mkeo ni gaidi kwa kiasi gani.

Inauma sana mke kukuona si lolote wala si chochote kisa tu huna mpunga
Pole sana ndugu, hayo yatapita tu
 
Kuwa na pesa haimaniishi ndiyo utakuwa na furaha kwenye ndoa. Wanawake wenye upendo wapo, huyo alikupenda kwasababu unavyo nawe hukumsoma.
Ajira mpya nimekosa paka sasa, huenda ningepata mapema ingeokoa Amani ya nyumba, NSSF nao hawatoi mafao yetu yote labda ningepata mtaji mzur nikaokoa Amani ya familia yangu.

Daah kweli kua uyaone
 
Back
Top Bottom