Ndoa ni maandalizi ya tangu usichana wako

Ndoa ni maandalizi ya tangu usichana wako

Yes , I have that 33 , it's my age na sijutii but unajua shida ni hiyo , umewahi kuuliwa mchumba , umewahi kuuliwa mama mkwe ili usitolewe mahari , umewahi mchumba wako kupata ajali wakati anaenda kufuata suri ya harusi nusu afee , umewahi kupoteza mchumba wako siku karibia ya ndoa .??
Usibwabwaje mdomo wako kipuuzi na hujui shida za watu Kwa maana unawaona wenzako wanaishi single wamependa , umewahi kupata mis carriage SITA Kwa wakati mmoja ila hujui why , kama umeamua kuongea shit because umeamua tu ili upate likes sio wote wanapitia hali rahisi Kama zako umewahi pata misiba miwili au mitatu Kwa mara Moja ukazike baba , ukazike mama mkwe na ukazike mume mtarajiwa uadui utoke kwenye familia ya mume wanadai wewe ndio chanzo na hujui lolote wewe ni mpuuzi na mshenzi , kabisa
Pole Dada Unique Flower BIla shaka unahitaji kuombewa maana hiyo ni Gereza ya shetani.Ukifuatilia unaweza ukakuta imewatokea na dada au kaka zako pia BIla Mungu huwezi toboa.
 
TABIA 12 ZITAKAZOKUFANYA UWE MWENYE FURAHA MAISHANI

1. Samehe

Samehee hata wasiostahili kusamehewa.
Usikubali kuwa na kinyongo au ugomvi na mtu yeyeto.
Jifunze kupotezea.
Usimjibu kila mtu kila kitu.
Hata ukimya ni majibu.

2. Jiamini

Hakuna lisilowezekana chini ya jua. Anza sasa.
Wenye imani wana amani kila wakati.
Wenye imani wanakuwa na uhakika wa kile wanachokitarajia.

3. Jifunze

Mungu hakumuumba mtu kuweza kila kitu wakati wowote.

4. Jipende

Umeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Usijidharau wala kujishusha kiwango. Jitamkia mambo mazuri kila wakati.

5. Tabasamu

Furaha ni tiba ya moyo
Jifunze kuhesabu baraka ambazo Mungu amekupatia itakisaidia kutabasamu kila wakati.

6. Usihukumu

Hakuna mwaminifu chini ya jua. Kila mmoja anakosea hata wewe huwa unakosea na kuwakosea wengine.

7. Jiheshimu

Mfumo wa maisha yako ndio utakuwa msaada kwa wengine. Wewe ndiye utakayewafanya wengine kukutafasiri.

8. Panga malengo

Malengo ni taa, dira, ramani,kesho, mwelekeo, matumaini. Usiishi pasipo kujua kesho yako au pasipo kujua unapoelekea.

9. Fanya Ibada

Mahusiano yako pamoja na Mungu ndio chanzo cha kubarikiwa kwako.

10. Kula vizuri

Mwili wako ni hekalu la Roho Mtakatifu kuwa makini sana kwenye ulaji wako. Usile chochote unachotaka Bali kula chochote kinachohitajika mwilini mwako.

11. Kuwa mkarimu

Hukuja duniani na kitu Bali vyote ulivyonavyo chanzo chake ni Mungu. Lakini pia vyote utaviacha duniani siku yako ya kufa itakapofika. Ukarimu ni akiba ya baadae kwa ajili yako na kizazi chako.

12. Kuwa mwenye shukrani

Ukitambua na kutafakari ulipotolewa na huyu Mungu hakika hautashindwa kusema asante kwake.
Mshukuru Mungu kwa kila jambo hata kama mengine yanaenda vibaya endelea kumwambia Mungu asante.

R. I. P Benjamin William Mkapa
 
Back
Top Bottom