Miaka fulani ya zamani kipindi Alikiba anatamba na Cinderella nilikuwa Moro kwenye majukumu ya Kazi sasa jioni nikawa nimetulia maeneo ya home na washkaji wanakata gambe kuna mwana anaitwa Rama ambaye alikuwa rafiki yangu na shemeji yangu kwa dada yangu fulani akanshtua kwa simu kwamba anataka aje nilipo maana amepata taarifa nipo maeneo ambayo yeye yupo..dakika chache tu akafika akiwa na Alikiba na dada yangu katika story story za hapa na pale akanambia Alikiba anamuomba dada yangu awe video queen katika moja ya nyimbo zake ila yeye akakataa nikamwambia sawa uamuzi ni wako kingine ambacho alinambia na ndicho kinanifanya niandike comment hii eti akanambia anajaribu kumzururisha Alikiba na kumpa michongo ya hapa na pale kwa sababu jamaa akiwa kwao anashinda ndani kutwa nzima anaweza asionekane nje hata wiki kila akimoigia simu yupo ndani tu ndio akamwambia basi njoo Moro angalau tupeane kampani moja mbili ndio akaja..Siku ile nikashangaa inawezekana vipi kijana mkubwa kama yule awe anashinda ndani tu wakati mimi nikiwa Advance tu tayari nishaanza kudandia mabasi na kujua uhuni wote wa stendi miaka ya 1996! Hapo ndipo jibu linakuja Alikiba SI MCHAKARIKAJI