Umeandika upuuzi mtupu. Anyway kila mtu ana stahili yake ya kufunga ndoa. Kuna mtu anapenda akifunga ndoa amwalike kila mtu aidha kwa ajili ya kupata michango au kujinyanyua ili ionekane kuwa harusi yake ilikuwa babkubwa kwa kuhudhuriwa na watu wengi nk.
Kuna mungine haswa hawa watu wazima ambao walikuwa washafunga ndoa hapo kabla, wengi wao huwa hawapendi ndoa za mbwembwe kutokana na umri lkn pia haoni sababu ya kila mtu kumtangazia ndoa ilihali ndoa yake ya kwanza na ya ujana ilifana sana.
Tuje kwa Mrema na mkewe, anyway inawezekana ndoa yake ilikuwa ya siri kama unavyosema lkn je Mrema alipoanza kuzunguka na mkewe kwenda Dodoma kuonana na mh raisi huyo mumewe hakumuona? Mrema alipoenda kula honeymoon na mkewe huko mbugani mikumi na sehem nyingine za nchi mumewe hakumuona? Waandishi mbali mbali wa habari walipokuwa wanamtembelea Mrema na mkewe na sometimes kukutana nae na kumhoji maeneo mbali mbali ya nchi mumewe hakumuona?
Mimi simjui Doreen na pia nipo nje ya Tanzania, lkn taarifa zote napata, iweje yeye mumewe akose taarifa za mkewe hadi baada ya mumewe (Mrema) kufariki?
Hapa kuna mchezo umepangwa lkn kwa bahati nzuri wengi wetu tunauelewa mpana wa maswala hayo ndo maana imekuwa ngumu kutumezesha propaganda zenu.