Ndoa ya rafiki yangu imedumu miezi miwili tu! -kweli ndoa ni mtihani?

Girland

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2016
Posts
2,489
Reaction score
4,253
Rafiki yangu ni mfanyabiashara Kariakoo hivyo pesa ya kubadili mboga sio Tatizo lake kabisa. Amedumu katika mahusiano zaidi ya miaka 8 na mwenza wake wa maisha kabla ya kuamua rasmi kufunga ndoa mwishoni mwa November 2023.

KILA MTU HAELEZI TATIZO
Wasuluhishi wameshindwa kwani kila mtu haongei tatizo ni nini, mwanamke hana nia ya kurudi tena na kaenda kwao!!

Kama watu hawa hawapendani, Je waliwezaje kudumu kwa miaka 8?Je kataa ndoa wana point tuwasikilize 😀?
 
Kwa maisha ya sasa hivi ni upuuzi tuu kufunga ndoa, ni mwendo wa kucheza mechi za ndondo na kulea watoto tuki shindwana unaenda kwenu watoto nitajua watakua vipi, na mahari inalipwa nusu nusu ili ukienda kwenu nisipate hasara kubwa
 
There's no vaccine against stupidity.
 
Ndoa ndoano.

Ile miaka 8 ilikuwa mahusiano ya hiari.

Ndiyo maana wamedumu muda wote huo.

Kwenye ndoa ni mahusiano ya lazima. Huyu ni mke wangu, nimemuoa. Nimemtolea mahari. Nimemnunua. Hili jiko langu.

Ndiyo maana miezi miwili tu, kwishney.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…