Ndoa ya wake wengi iruhusiwe kwenye ukristo kuokoa kizazi cha wanawake ambao wanazeeka makanisani bila waume

HAKUNA WIFE MATERIAL AKAKOSA MME.

HAO UNAOWASEMA WEWE NI WANAWAKE WASHENZI, WADANGAJI, MAKAHABA, WAZINZI NA WAASHERATI.

Mwanamke awe na Elimu nzuri kabisa akose mwanaume.

Labda uwaongelee wanawake wa KISHENZI WANACHEZA uchi.
 
Naunga mkono hoja....!
 
Uzuri Paulo husema kabisa kuwa maagizo mengine si ya Mungu ni yake kama mtumishi wa Mungu.
 
Sijajua hayo Maandiko ya kuoa mke mmoja mumeyatoa wapi. Sijaona katika Maandiko panapozuia wanaume kuwa na wake zaidi ya mmoja.
 
Haya yalikuwa maoni yake siyo ya Mungu Kiongozi. Kusema uwe na Mke, haimaanishi awe mmoja tu. Hapo kilichowasilishwa ni Ile Hali ya umiliki. Uwe na Mke wako. Kama utaoa zaidi Kila mwanamke atakuwa Mke wako wewe na jamii itakuwa kuwa ni mke wako.
 
Soma post no 16 utapata
Post No.16 amefafanua vizuri hili jambo, shida yake ni Moja kwamba anavyotafsiri umoja(singular) uliotumika katika Maandiko, haimaanishi uwingi umezuiliwa. Amejenga hoja yake kwakuwa Biblia imeandikwa katika umoja. Anacapitalise hapo.

Vifungu vyote alivyotaja hapo hakuna kinachozuia kuoa mke zaidi ya mmoja. Na zaidi ya yote vyote vilikuwa eraborative(vilikuwa vinafafanua maswali) na havikuwa directive(havikuwa vinatoa agizo). Visome upya kiongozi utakuta vilikuwa vinafafanua maswali fulani au hali fulani za kindoa.
 
We una wake wangapi
 
Yani hili somo ni la kuungaunga kweli! na hapo ndo umemaliza hoja zote kabisa!

Somewhere kwenye somo lako ulisema mitaala ilipoanza Mungu aliinyamazia huku akipanga kuwakomboa katika dhambi hiyo hapo baadae (Sorry nimeshindwa ku-quote as u have made is too long so it's to trace back every point). Halafu baadae in later paragraphs ukasema Mungu hakuongelea tena hilo suala la mitaala katika biblia kwakuwa halikuwa katika plan yake ya mwanzo.

Sasa swali ni kwamba alisahau kama hii ni dhambi ambayo watu wanaifanya japo haikuwa katika mpango wake wa awali? na tunajua Mungu hasau, sasa kwanini hakuikemea directly? Si ndo Mungu huyu huyu aliyesema Usiue, Usizini, Waheshimu wazazi wako n.k? lakini linapokuja swala la dhami ya kuoa mke zaidi ya mke mmoja (tena iliyofanywa mpaka na mitume wake wakubwa kina Moses, Sulayman, David, Yakobo etc.) azunguuuke sijui "Mke wako mwenyewe", "Atatoka kwa wazazi wake aambatane na mke wake" n.k. ... Hapana jamani acheni hizo.

Kubwa zaidi unasema kwa kujiamini kabisa eti Mungu alikuwa anawaza hivi na sio vile!!! kweli??? mbali na kusema kwamba Mungu anakaa akawaza (Mungu anisamehe hata kutamka neno hilo) bali pia una uwezo wa kujua nini Mungu alikuwa anawaza!!! na hakuna sehemu yoyote ambayo Mungu ameyafungua hayo kwa mwanadamu.

Hebu muogopeni Mungu na acheni kumsingizia Mungu kwa akili zenu za kibinaadamu.
 
HAKUNA WIFE MATERIAL AKAKOSA MME.

HAO UNAOWASEMA WEWE NI WANAWAKE WASHENZI, WADANGAJI, MAKAHABA, WAZINZI NA WAASHERATI.

Mwanamke awe na Elimu nzuri kabisa akose mwanaume.

Labda uwaongelee wanawake wa KISHENZI WANACHEZA uchi.

Unakosea sana,au huna dada ama watoto wa kike,hivi ration ya wanawake na wanaume unaijua vzr?tafakari vyema.
 
Solomon,Musa na hao wengn uliowataja hawakua WAKRISTO. Misingi ya Kikristo umewekwa na Kristu mwenyewe ambao kakataza mume kua na wake wengi! Ko ukitaka WAKRISTO waoe wake wengi UnamAanisha wasiiwe WAKRISTO Tena kwa maana hawajafuata maagizo ya Kristu mwenyewe.
 
Unakosea sana,au huna dada ama watoto wa kike,hivi ration ya wanawake na wanaume unaijua vzr?tafakari vyema.
Umenena hakika Mkuu. Kuna mabinti watulivu sana ila kuolewa tu hawajabahatika. Wala siyo suala la uzinzi, ukahaba, ushenzi au uesharati. Makahaba wanaolewa sana mbona.

Haya mambo ni magumu kuyaelewa mara nyingine. Universe iingilie tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…