Ndoa yangu changa inataka kuniua

Ndoa yangu changa inataka kuniua

[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
Nilikua sina raha ila kwa hii comment yako nimecheka sana mkuu
Sipati picha mkuu akiuzwa[emoji38][emoji38]yeye na viatu vyake
Hii ndiyo raha ya JF.

Anauzwa alafu bei ya kutupa. Auzwe na viatu? Mpaka afike hapo hana tena viatu.

Yamebakia malapa ya uani. Ndiyo mkuu akimbie nazo.
 
Wahesimiwa wa mmu, ndoa yangu ya mwaka mmoja inakaribia kuniua, ushauri wenu muhimu sana.

Huyu mwanamke nimejuana naye miaka miwili kabla sijaamua kumuoa, ingawa pia maamuzi ya kumuoa yaliharakishwa na kumpatia ujauzito akiwa mwaka wa pili chuo.

Matatizo sasa yanaanzia hapa:
1. Baada ya kumuoa katikati ya mwaka jana akiwa anakaribia kurudi chuo, aliamua kujifukuzisha chuo kimya kimya kwa kutoingia darasani. Ni mpaka mwaka huu mwanzoni ndo nilipojua ukweli, nikamsaheme nikifikiri ni mimba iliyomfanyia hivyo na nikamsaidia kuchaguliwa kwenye chaguzi za juzi hapa

2. Alianza tabia ya kuiba hela nazo rudi nazo nyumbani, hapa nikafikiri ni mdada wa kazi baada ya kumtimua lakini tabia ikaendelea. Hapa ilinilazimu niwe naficha hela kwenye gari.

Si akaja kugundua akaanza kuzifuata huko huko kwenye gari, sasa hapa nikawa nazificha sehemu ambazo asiye fundi hawezi zifikia. Hapa kunaujinga mwingi sana umefanyika mpaka ikafika yeye kukata hela ya chakula.
(Anabana hela ya chakula, chakula kina kata katikati ya wiki).

3. Wizi wa hela ya sadaka, hapa niliandaa hela ya sadaka ya shukrani, nikaiweka kwenye bahasha na tukaiombea, nikafunga bahasha na gundi. Kesho yake asubuhi tunaenda kanisani nikagundua bahasha ilifunguliwa na nusu ya hela imepigwa.

4. Kuna vitu vimeanza kutoweka nyumbani, begi kubwa la nguo, set za mapazia niliyonunua kwa bei kubwa, simu yangu ya ofisini (Naitumia mara chache, kwa shughuli za ofisi) na godoro dogo la chumba cha wageni. Nilivyoongea naye jana kuna kila ishara kuwa ameviuza.

Dah naombeni ushauri maana najiona kabisa kwenda kuua mtoto wa watu, maana sioni kitu anachokifanya na hizo hela zaidi ya nyumba kujaa makopo ya juice na soda.

Na hata hivyo ameanza uvivu, usafi kwake ni changamoto saa nyingine naogopa kwenda jiko

Na hata hivyo ameanza uvivu, usafi kwake ni changamoto saa nyingine naogopa kwenda jikoni.
Una watoto naye?
Mazuri yake ni yapi mkuu.
Ni dhahiri maamuzi ya kumuoa uliyafanya kwa hisia.
Pia naomba kabila lake.
 
Kama ulidate na kuoa type ya hawa ninaokaa nao ghetto yani wanaloweka mashuka mpaka yanaoza wanayatupa, wanaosha vyombo wakitaka kupika kisha baada ya hapo wanakaa siku nne hawajaosha mpaka wakipika tena. Nakuhakikishia utaishia kumfurahia mkienda Kidimbwi tu. Sijui kushauri ndoa
Mkuu cha kufurahisha yeye sio mtumiaji wa pombe, na pia kabla ya ndoa vyombo vilikua hajikai ila sasa hivi ndo kama hivyo mpaka asikie njaa nod vinaoshwa
 
Fanya jitihada pia za kujaribu kukaa nae kwanza muongee ugundue chanzo nini, usipopata suluhu hapo uende kwa ndugu, jamaa, marafiki, wanasaikolojia... baada ya hapo tena kwa wazazi wake...viongozi wa dini...mahakamani... ikishindikana hapo tena fanya uamuzi sahihi tu hata wa kuachana nae lakini usimdhuru kwa chochote maana hutatatua tatizo sana sana utaongeza ukubwa wa tatizo.
Nashukuru mkuu, nitajaribu maana nimepata ugumu kwa sasa kushare hizi na ndugu na jamaa.
 
Pole sana mkuu! Ni ngumi sana kumbadili tabia hiyo kwa haraka haraka itachukuwa muda na uvumilivu na hekima pia..!

Kwa mtazamo wako unahisi anakupenda kweli ?

Una uhakika kuwa hiyo mimba ni yako?
Nani alileta mawazo ya aliharakisha ndo?
Kusema ukweli kwa sasa sina uhakika alinipendea nini, nilifikiri ni vile ninavyomjali lakini sina uhakika.
Mtoto ameshazaliwa kwa kweli siwezimkataa.
Hilo wazo nililipata baada ya kutoona kasoro kwake na pia ili nimuwezeshe amalize shule bila stress
 
Mkuu, umeoa mke au umeoa mwizi?

Huyo ni mdokozi kwa asili lakini pia tabia yako ya Ubahili wa kutompa hela inakuponza.

Atauza vyote. Vitu vya ndani vitaisha, itafuata gari kisha nyumba 😂😂😂. Baada ya hapo nguo zako alafu utabakia wewe na mtoto. Nani atangulie kuuzwa?

Bila kufumba macho ni wewe. Utauzwa abaki yeye na mtoto.

Kimbia Mkuu. Mtu asiye na soni hata ya kupunguza hela ya sadaka ni mtoto wa Lucifer tu.

Kimbia. Viatu vikikatika wewe kimbia, bora miiba kuliko kuuzwa. Kimbia Mkuu.

Chaguo lako ni kukimbia ama kuamua kumpa hela zote unazopata. Chagua kwa busara.
Mkuu nashukuru kwa ushauri wako, kwa jinsi navyoona huko ndo tunapoelekea
 
Back
Top Bottom