Ndoa yangu changa inataka kuniua

Ndoa yangu changa inataka kuniua

Wahesimiwa wa mmu, ndoa yangu ya mwaka mmoja inakaribia kuniua, ushauri wenu muhimu sana.

Huyu mwanamke nimejuana naye miaka miwili kabla sijaamua kumuoa, ingawa pia maamuzi ya kumuoa yaliharakishwa na kumpatia ujauzito akiwa mwaka wa pili chuo.

Matatizo sasa yanaanzia hapa:
1. Baada ya kumuoa katikati ya mwaka jana akiwa anakaribia kurudi chuo, aliamua kujifukuzisha chuo kimya kimya kwa kutoingia darasani. Ni mpaka mwaka huu mwanzoni ndo nilipojua ukweli, nikamsaheme nikifikiri ni mimba iliyomfanyia hivyo na nikamsaidia kuchaguliwa kwenye chaguzi za juzi hapa

2. Alianza tabia ya kuiba hela nazo rudi nazo nyumbani, hapa nikafikiri ni mdada wa kazi baada ya kumtimua lakini tabia ikaendelea. Hapa ilinilazimu niwe naficha hela kwenye gari.

Si akaja kugundua akaanza kuzifuata huko huko kwenye gari, sasa hapa nikawa nazificha sehemu ambazo asiye fundi hawezi zifikia. Hapa kunaujinga mwingi sana umefanyika mpaka ikafika yeye kukata hela ya chakula.
(Anabana hela ya chakula, chakula kina kata katikati ya wiki).

3. Wizi wa hela ya sadaka, hapa niliandaa hela ya sadaka ya shukrani, nikaiweka kwenye bahasha na tukaiombea, nikafunga bahasha na gundi. Kesho yake asubuhi tunaenda kanisani nikagundua bahasha ilifunguliwa na nusu ya hela imepigwa.

4. Kuna vitu vimeanza kutoweka nyumbani, begi kubwa la nguo, set za mapazia niliyonunua kwa bei kubwa, simu yangu ya ofisini (Naitumia mara chache, kwa shughuli za ofisi) na godoro dogo la chumba cha wageni. Nilivyoongea naye jana kuna kila ishara kuwa ameviuza.

Dah naombeni ushauri maana najiona kabisa kwenda kuua mtoto wa watu, maana sioni kitu anachokifanya na hizo hela zaidi ya nyumba kujaa makopo ya juice na soda.

Na hata hivyo ameanza uvivu, usafi kwake ni changamoto saa nyingine naogopa kwenda jikoni.
Sasa kwa mtu wa aina hiyo utafanya maendeleo gani kwenye hii dunia..jiulize mwenyewe halafu ujijibu.
Huyo ndo mtu wa kuanzisha nae familia?
 
Sasa kwa mtu wa aina hiyo utafanya maendeleo gani kwenye hii dunia..jiulize mwenyewe halafu ujijibu.
Huyo ndo mtu wa kuanzisha nae familia?
Mkuu kusema ukweli ukiachana na ukweli kuongezeka kwa majukumu kumenisaidia kuongeza jitihada za utafutaji na kuweza kuongeza kipato changu mara mbili zaidi ya kabla ya ndoa. lakini pia gharama na stress za kununua vitu ambavyo sikupaswa kununua tena kunanirudisha nyuma na kunanipa hofu ya kuendeleza hali ya nyumbani.
 
Mkuu kusema ukweli ukiachana na ukweli kuongezeka kwa majukumu kumenisaidia kuongeza jitihada za utafutaji na kuweza kuongeza kipato changu mara mbili zaidi ya kabla ya ndoa. lakini pia gharama na stress za kununua vitu ambavyo sikupaswa kununua tena kunanirudisha nyuma na kunanipa hofu ya kuendeleza hali ya nyumbani.
Umesema umemuoa akiwa chuo probably bado ana umri mdogo sana..ana mambo ya kitoto na akili hazijakomaa.
Bado ana akili kama za wale mabinti wa chuo,hayupo tayar kuwa mke wala mama.
Pole mkuu
 
Hapa nafanyaje kumuwezesha yeye kuoa maisha hayapo hivyo???
Maana mbinu zangu zote zimeshindikana
Nyongeza.
Usimshirikishe mambo yako ya kifedha.maana tabia yake ndo hivo.
Kuwa msiri,jifanye uko broke,usishee kadi ya ATM ama namba za mpeaa nk.mpaka atapobadilika labda.
 
Why umpige tukio, unajenga ama unabomoa, ameomba msamaha msamehe, akirudia piga chini
Nilikua na maanisha baada ya kukosea na kuniomba msamaha, huwa tunakaa na wiki 2 au 3 za amani. baada ya hapo atafanya tena tukio la design hii
 
Kwa wakongwe sisi moja ya mbinu za medani ni kumpandisha cheo awe Bi Mkubwa!

Hapo atasaidiana na Bi Mdogo kufanya mipango mahsusi ya maisha.
Kusema ukweli hii inaonekana ndo suluhisho, ila tatizo nafsi yangu haitaki kabisa kusikia habari hizo
 
Back
Top Bottom