Ndoa yangu inateketea

Ndoa yangu inateketea

Kwanza namba nikujenge kiimani... Majaribio ktk Maisha ndo sehemu ya Maisha. Haijarishi kubwa kiasi gani lkn Mungu anajua unalimudu.. Katika kipindi hiki unachopitia mtafuta Sana Mungu maana ni kipindi cha kupimwa imani yako. Muda or time healed... Surrender all things to your God. Ndoa ni spiritual connection hivyo mambo Muombe Mungu tu ili ushinde jaribu.. Muda utaongea tu usiangaike kama divorce atatafuta yeye maana Wana washauri wao wa kubomoa.. Naamini soon utarecover na kuona Maisha mapya ya furaha na amani na kumsahau kabisa. Mungu atakujenga utainuka na kuwa na mafanikio makubwa... Maisha ya Mungu. Trust in God.
 
Pole sana Mkuu,
Kitendo cha mke wako kutafuta uhamisho wa kwenda Dar, nyumbani kwao ilipaswa kukupa ishara kuwa kuna jambo baya katika ndoa yenu kwa upande wake...

Mke wako ni mtu anapenda vitu (material wife) na kazi alonayo inampa kiburi.
Na pia familia yake inahusika katika kumshauri vibaya.

Kama kweli unampenda mke wako, bas tafuta mganga wa kienyeji afanye yafuatayo,
1.Amfukuzishe kazi na asipate kazi milele na
2.Amrudishe kwako.

Kila la kheri...
Huu ndio ushauri wa kiafrika. Msilazimishe uzungu na hamuuwezi, mwisho wa siku mnalia tu
 
Tungemsikiliza na yeye tungejua shida iko wapi. Inawezekana kuna kitu umefanya/kimemkera kutoka kwako na hujasema hapa. Au ameona hueleweki. Mtu hawezi fanya maamuzi ya hivo tu from nowhere.
 
Pole sana Mkuu,
Kitendo cha mke wako kutafuta uhamisho wa kwenda Dar, nyumbani kwao ilipaswa kukupa ishara kuwa kuna jambo baya katika ndoa yenu kwa upande wake...

Mke wako ni mtu anapenda vitu (material wife) na kazi alonayo inampa kiburi.
Na pia familia yake inahusika katika kumshauri vibaya.

Kama kweli unampenda mke wako, bas tafuta mganga wa kienyeji afanye yafuatayo,
1.Amfukuzishe kazi na asipate kazi milele na
2.Amrudishe kwako.

Kila la kheri...
Akifukuzwa kazi sasa watakula nini na mkuu hana kazi?Ushauri mbaya huu😅
 
Pole sana kwa changamoto ya ugonjwa na ya Mke wako, jitahidi kushirikisha Wazazi wa pande zote mbili ikibidi viongozi wa dini kutokana na imani yenu ikishindikana ndoa ivunjwe kisheria, Mungu akusaidie.
 
Naam.


Usishangae ... Wanawake wangapi wasokua na kazi ,wamewakimbia waume zao???


Wangapi??? Au unajitoa ufaham.



Inshu hapaa ni kupata mwanamke Mwema wa maisha yako, Awe anauchumi mkubwa, awe hana Uchumi, akiwa mwema atakua mwema, akiwa sio mwema atakua sio mwema.

Unataka kuniambia wanawake wote wenye kazi na uchumi wao, wote wana tabia ya kijinga kama yahuyo???????.




Hoja ya jana ilikua... Mwanaume Oa mwanamke hata kama kakuzidi uchumi. Maadam mmeelewana , OA...


Wewe umekomaa, atakudharau, atakufanyaje, sasa hiyo inaonyesha HUJIAMINI.
[emoji123][emoji123]
 
Every man's nightmare is losing a job when he has a family to take care of.

Sasa ukutane na mwanamke ambae amebaki anahudumia familia halafu sio muelewa.

The devil in her comes out blaring massive horns.

Kaza moyo, cut her off. Usimpigie usiwe na mawasiliano aina yeyote na yeye. Kubali awalee watoto sababu after all huna kazi na yule ni mama yao sio mtu baki.

Concentrate on afya yako then pambana uinuke tena. Simama na Mungu wako na ujipe time. Its just a matter of time atajirudisha kwako na majuto na kilio huku wewe ushapona.
 
Habari wana JF wote kwa ujumla,bila ya kupoteza muda naomba kuja kwenye mada husika.
Mimi ni kijana wa miaka 35,ndoa yanagu mpaka sasa inamiaka 5 tuu.
Ktk kipindi chote hichi tumeishi kwa furaha na upendo mkubwa tumebahatika kupata watoto 2.
mke wangu ni mtumishi chuo kikuu(mwalimu)na mimi ni unga unga mwana pangu pakavu baada ya kampuni fulani ya mawasiliano niliyokua nafanya kazi kufungiwa na serikali kwa madai ya kukwepa kulipa na kuhujumu uchumi hivyo kesi bado iko mahakamani.lakini sijawahi kukosa rizik japo kipato changu ni kidogo ila upendo na furaha viliendelea kushamiri.
KUANZA TATIZO

Mambo yalianza kua mabaya ktk ndoa yangu pale tuu mke wang alivyohamishwa kikazi na kuja hapa Dar ktk chuo kikuu fulani mwaka huu mwez 3.hivyo mimi niliendelea kubaki mkoni kwa lengo la kujipanga ili nihamie dar ili niwe karibu na familia yangu.
Ifahamike kua uhamisho wake haukua wa malipo kutokana na yy ndo aliomba kuhamishwa hivyo alipofika hapa Dar alifikia kwao maana yeye ni mzaliwa wa hapa dar.
Baada ya miezi 2 kupita mimi pia nikatoka mkoani na kuja hapa Dar,ila nilifikia nyumban kwetu kwa wazazi wangu (Mkuranga)
Harakaki za kutafuta nyumba zikaanza,kwa bahati mbaya wakati sijalipia nyumba nikafiwa na mzazi wangu(baba) chakushangaza mke wangu hakuweza kufika msibani kwa madai ya kukosa ruhusa kazini.
Sikua na neno maana bado nilikua kwenye majonzi,baada ya msiba kumalizika nilinza kujisikia homa kali na kulazwa hospitali,baada ya vipimo niligundulika ni Covid 19,
Mungu alisaidia nikaruhusiwa na kuendelea na matibabu nyumban,
Wakati naendelea na matibabu mawasiliano na mke wangu yalikua ya tabu sana,simu za zilikua hazipaikan kwa madai mtoto wetu mdogo ameharibu simu yake hivyo ilinibidi niwe namtafuta mama mkwe kuongea na mke wangu,
Hali ya kimawasiliano ilizidi kua mbaya zaid kadri siku zinavyozidi kusonga mbele,akawa hanitafuti,mpaka mimi nimtafute yeye,upendo wake kwangu ulikua umepungua sana kwangu.
Maana hata kunijulia hali imekua vigumu kwake.
Kibaya zaid alinza kufuta account namba yake ya wasapu na kuwa online kupitia Facebook.nilivyomuuliza mbona nakuona online ushanunua simu nyingine?alinijibu kua ni ya ndugu yake wanaishi karibu pia namjua huyo mtu.
Nilimuomba namba ya simu anayoitumia ya huyo ndugu yake akanipa.
Chaajabu sasa nikipiga ile namba anapokea muhusika wa ile simu na ananimbia yy yuko mbali kidogo na mke wangu.
Hii hali ilinishangaza sana kwan mda ambao nachat na mke wangu Facebook ndo mda huo nimepiga simu baada ya yy kunipa hiyo namba na kaniambia ndo anaitumia kwenye hiyo simu,
Niliendelea kuvumilia hii hali kwakua sikua na jinsi maana bado naendelea na matibabu.
Hapa juzi kanitumia ujumbe kupitia Facebook anasema tuachane yy amechoka na maisha ya ndoa hivyo anahitaji kua single,haoni faida ya kua kwenye ndoa.
Kwa kwel moyo wangu wote ulikua unawaka moto kwa maumivi makari sana
Kwakua bado naumwa halafu nakutana na changamoto kama hii.
Ilinibidi nimtafute kwa kumpigia simu kupitia kwa mama ake akampa simu nikaongea nae.
Nilimuuliza kwan kipi kibaya ambacho nimekufanyia mpaka umefikia maamuz hayo ya kutaka tuachane?alinijibua kua yy amechoka na kudharauliwa hapo kwao maana inaonekama kama mimi nimemdamp tuu hapo kwao,
Nilimuuliza kwan hujui hali yangu ya kiafya kwasasa? Akanijibu kua anajua ila hayo ndo maamuzi aliyaamua kwan kichwa chake hakiko sawa,pia kazin kwake pia hajapandishwa mshahara hivyo hayuko sawa. Baada ya kuniambia hiyo alinikatia simu.

Ifahamike kua kipindi hiki chote ninachoumwa kaja kuniona mara moja tuu mpaka sasa ni mwez umekata hajaja kuniona.
Na mda huu yuko likizo haend kazin.

Naombeni ushauri wenu na mawazao nini nifanye kuinusuru ndoa yangu?hali yangu kiafya bado haija kaa sawa.ndoa inazidi kuniumiza msaada wenu tafadhali.
Nani kakuambia siku hizi ukiwa mbali na mke wako, na usiwe na pesa ya kumsaidia na kwenda kumwona mara kwa mara ETI BADO KUNA NDOA. Pole sana. Ameshakuwa mke wa mwingine. Ww ni mme wa cheti tu. Jipange kimaisha sababu hauna mke tena.
 
Si anataka kuachwa muache mzee, usilazimishe kijani kuwa nyekundu, kwanini ubembeleze mapenzi, utakufa bure kwa kufosi mambo. Kwani bila ya yeye wewe hupumui, kifupi hana mpango na ww na ukilazimisha atakuja kukupiga tukio moja uione june-july
Hakuna kitu kama hicho......jamaa kwa sasa anapaswa Ku lay low.....apambane kutafuta fedha atafute mwanamke mwingine hiyo ndio dawa.....
 
Pole sana Mkuu,
Kitendo cha mke wako kutafuta uhamisho wa kwenda Dar, nyumbani kwao ilipaswa kukupa ishara kuwa kuna jambo baya katika ndoa yenu kwa upande wake...

Mke wako ni mtu anapenda vitu (material wife) na kazi alonayo inampa kiburi.
Na pia familia yake inahusika katika kumshauri vibaya.

Kama kweli unampenda mke wako, bas tafuta mganga wa kienyeji afanye yafuatayo,
1.Amfukuzishe kazi na asipate kazi milele na
2.Amrudishe kwako.

Kila la kheri...

Ubaya ubaya au sio mkuu?[emoji28]
 
Mwache aende mkuu japo ni ngumu kuhandle hali hiyo.
Chukua watoto uishi nao,hapo kwako itakuwa rahisi sana wewe kumsahau yy.halafu pambana kuzisaka kwa namna yoyote ile ili wanao wawe katika furaha tu.
Mwanamke akikutamkia hakutaki hilo ni jambo la kushukuru mungu sana tena sana.
Naamini kama watoto ulikuwa unaishi nao vizuri na walikuwa wanakukubali basi jua hawawezi kukusumbua kuhusu mama yao.

Mfano mimi mwenyewe
Ndoa yangu ya miaka 8 niliivunja mwaka huu mwezi wa pili.baada ya maugomvi yasiyoisha ndani kila siku.nikabaki na wanangu wawili mkubwa miaka 7 na mdogo miaka 4.

Nini nilifanya?
Baada ya kuachana nae nilifuta mawasiliano yake kabisa na kumblock kila sehem.
Nilitafuta kisimu kidogo na laini yake vipo nyumbani nikampatia namba kama atataka kuwasiliana na watoto apige kule ataongea nao.
Na iko hivyo hadi ninapoandika ujumbe huu.amekuwa akinitafuta kwa namba tofauti na kutuma tena wazee kila mara lakini hii safari haiwezi jirudia tena na tena.na kila namba anayonitafuta nayo yaani ile nikijua ni yy hakuna kinachofuata zaidi ya block tu.

Kwangu nimefanikiwa hili jambo kwa asilimia kubwa sana.kwa sababu....!!!!!

Nilijenga msingi imara kwa wanangu tangu yy akiwepo na nilikuwa naplay part kubwa sana ya baadhi ya majukum pale nyumbani ndio maana hata yy alivyoondoka wanangu hawajawahi kunisumbua mama yao yuko wapi na kwa nini kaondoka?imagine mtoto wa miaka 4 tena wakiume unadhani huo usumbufu ungekuwaje kuhusu mama yake?lakini huyu wangu hajawahi kuniuliza.unajua kwanini?

Yeye akiwa nyumbani anafanya majukumu yake,na mimi ilikuwa nikirudi kusaka mkate nilikuwa nafanya pale alipoishia yy.kuna nguo chafu nafua,chakula bado basi nafanya maandalizi yote na kupika kuna sehemu hapajakaa sawa ndani narekebisha then naendelea na mambo yangu mengine.uzazi wote wa watoto wawili sijawahi saidiwa na mtu hadi kumkanda ni mimi mwenyewe imagine hapo.

Kila siku watoto nilikuwa naamka nao,nawaogesha,niwape kifungua kinywa naondoka nao nawapeleka shule ndio nami naenda kibaruani kwangu.

Haya mimi nimeyaweza sababu malezi yangu sikulelewa kumtegemea mtu bali asilimia kubwa nijitegemee na kazi nyingi za nyumbani kwetu ilikuwa hazichagui wakike wala wakiume mpaka tunakuwa wakubwa.

Bro mambo ni mengi ila mteme huyo vinginevyo utaishi kwa tabu sana duniani hapa.hii vita manabii wenyewe waliopewa hekima na uwezo na muumba waliishindwa sembuse sisi.

Pambana upate hao wanao ukishindwa kukaa nao kutokana na changamoto za kimajukumu basi peleka kwenu hapo upambanie mkate wao tu huyo chap sana unamsahau.

Si lazima tuoe tena hali ya kuwa watoto tayari tunao kama hivi.mbususu mtaani kibao ni sisi tu kuchagua ipi inafaa kwa siku hiyo[emoji23][emoji23]..

MUNGU AKUSIMAMIE KWA KWELI KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU UNACHOPITA..
Ila hapo mapenzi hakuna tena zaidi ya mateso kwako
Wanaume wanaofanya kazi za nyumban kama wewe nawaonaga wa kipekee sana
 
Ningekuwa wewe baada ya kupona ningejikita kwenye mitikasi ya kupata hela. Mbona atarudi mwenyewe tu?

Tatizo la wanawake wengi si wa vumilivu. Anadhani hiyo situation utakuwa nayo kwa maisha yako yaliyobaki....hajui kwamba ni hali ya muda tu mambo yatakaa sawa.

Pole sana ndugu.
Wanakwake hawanaga akili....
huyu jamaa anayemdharau leo anaweza kuja kuwa tajiri mkubwa sana kesho....
Mungu wetu ana maajabu (full of surprises)
 
Itoshe kusema Pole sana Mkuu. Wanaume tunapambana sana kwa ajili ya familia zetu na ndicho kinachowafanya hawa wanawake wajifanye kutupenda. Haya mapambano ya kipungua au kufa kabisa kwa sababu yoyote ile, iwe kufukuzwa kazi au kuumwa ambako kutapelekea uache kupambana basi ndio mwisho wa mapenzi. Atajifanya kukupenda kwa muda tu kutafuta njia ya kutokea lakini atakuacha tu
 
Aisee, hivi kweli unaoa mwanaMke wa Dar? Huwa hawana akili timamu. Ni wachache sana wanaojitambua. Kama alijiombea uhamisho kwanini aseme umemdump kwao na wakati aliondoka mwenyewe.

Piga chini hilo jinamizi mkuu, najua inauma lakini hakuna namna. Kama BILLGATES na Mkewe waliachana ije iwe wewe.

Muache mwaka mzima, ukiona bado hajielewi, zama Singida kachukue msupuu uoe
 
Hao ndiyo wanawake kaka; hawajali maumivu ya wenzao kwenye jambo lao; wakibadilika wanakuwa wakatili kuliko simba.

nashauri kama ameomba muachane usilazimishe yatakukuta makubwa. Egemea ktk afya yako.. mwenzako amepata mwanaume mwingine.
 
Kuna wanawake waliolewa ili kutowa gundu tu, mnaweza kuishi pamoja na asikushirikishe mishe zake.

Mapenzi na ndoa yamekwisha siku hizi, Banana Zorro alishaimba kitambo tu.

Mahawara ndio wanaofurahia maisha kuliko wanandoa cha msingi mushiko iwe inakupitia tu.
Naunga mkono hoja
 
Acha mawazo ya ulozi wewe
Mkuu hatufahamiani, nakuomba ujiheshimu, na kama wewe ni mtu wa dini bas endelea na imani yako, nimeona mengi sana mpaka hapa nilipo, na katika watu wanaoongoza kwa unafiki ni watu wanaojifanya wameishika sana dini.

Hivi unajua watu wanavutwa kwa madawa kuhudhuria huko kwenye nyumba za Ibada(sio zote)?

Niishie hapa...
 
Back
Top Bottom