Ndoa za kikristo hazifati maandiko ya kwenye biblia, zinafata sheria za viongozi wa makanisa

Ndoa za kikristo hazifati maandiko ya kwenye biblia, zinafata sheria za viongozi wa makanisa

Musa alipooa mke zaidi ya moja alikuwa na ;engo la kuzaa kama Panya ??
wewe zaa tu
wakristo wanafuata injili
agano la kale ni kwa ajili ya visa vya zamani
ndio maana tukafundishwa jinsi ya kusali na amri kuu ni upendo
 
Hadi sasa sijaona kanisa linalofata maandiko kama yalivyo kwenye biblia, sheria zinazofatwa ni za viongozi wa makanisa zikiwemo sheria za utesaji za kulazimisha mapadre wasifanye sex maisha yao yote, ndizo hizi sheria iliwafanya kina Dokta slaa wakimbie upadri, waliobaki ndio hawa wengi wenye watoto wa siri mitaani na lundo la kesi za kulawiti watoto wa kiume
ukweli mchungu
 
Kwani mkuu umefungishwa ndoa ambayo haijafuata maandiko? Maana ndoa zetu maandiko yanasema utaachana na wazazi na utaambatana na mume/mke, maandiko yanaagiza mwanaume kumpenda mke na mke kumuheshimu mume, kama maagizo hayo yakivunjwa automatically ndoa inakua haijatendewa haki
mbona hujamalizia mstari vizuri, malizia na watakua "mwili moja"

Mwanaume ni mwili moja na kila mwanamke ataekutana nae kimwili, iwe ni kwenye ndoa yenye baraka zake Mungu ama Nje ya ndoa akiwa na malaya, Kwa hio pale mwanaume anapokuwa mwili moja na mke wake bado haiondoi kwake kuwa mwili moja na wake wengine. hata sisi wanadamu tupo zaidi ya bilioni lakini Mungu yupo moja ila kila anaeungana roho yake Mungu hutengeneza roho moja, Ndivyo ilivyo hivi kwa wanawake wengi wakiolewa na mwanaume moja kila moja wao huwa ni mwili moja na mme moja.

Siongei maneno matupu bila maandiko ya biblia 1-wakorintho 6:16

Au hamjui ya kuwa hata yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja, Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.
 
mbona hujamalizia mstari vizuri, malizia na watakua "mwili moja"

Mwanaume ni mwili moja na kila mwanamke ataekutana nae kimwili, iwe ni kwenye ndoa yenye baraka zake Mungu ama Nje ya ndoa akiwa na malaya, Kwa hio pale mwanaume anapokuwa mwili moja na mke wake bado haiondoi kwake kuwa mwili moja na wake wengine. hata sisi wanadamu tupo zaidi ya bilioni laini Mungu yupo moja tu lakini kila anaeungana roho yake na Mungu hutengeneza roho moja, Ndivyo ilivyo hivi kwa wanawake wengi waliolewa na mwanaume moja kila moja wao ni mwili moja

Siongei maneno matupu bila maandiko ya biblia 1-wakorintho 6:16

Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja, Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.
Sikuona haja ya kuandika kwa kurefu, by the way mkuu sijaelewa point yako hapa. Unamaamisha ndoa za kikristo hazifuati maandiko? Personalky nadhani ndoa zinafungwa kwa kufuata maandiko lakini wanandoa wanashindwa kutimiza maagizo yaliyotolewa kwenye maandiko ikiwa ni pamoja na kubunja viapo vya ndoa, kushindwa kutimiza majukumu ya ndoa, nk.
 
wewe zaa tu
wakristo wanafuata injili
agano la kale ni kwa ajili ya visa vya zamani
ndio maana tukafundishwa jinsi ya kusali na amri kuu ni upendo
Agano jipya halijazungumzia chochote kuhusu kukataza kuoa mke moja, uje na ushahidi
 
Umeulizwa Mussa alikia Malaya?
Mimi mambo ya kabla Yesu kuja kutuokoa huwa
Hadi sasa sijaona kanisa linalofata maandiko kama yalivyo kwenye biblia, sheria zinazofatwa ni za viongozi wa makanisa zikiwemo sheria za utesaji za kulazimisha mapadre wasifanye sex maisha yao yote, ndizo hizi sheria iliwafanya kina Dokta slaa wakimbie upadri, waliobaki ndio hawa wengi wenye watoto wa siri mitaani na lundo la kesi za kulawiti watoto wa kiume
Si ukaoe serikalini na kwenye cheti kuna option ya ndoa ya wake wengi.
 
Sikuona haja ya kuandika kwa kurefu, by the way mkuu sijaelewa point yako hapa. Unamaamisha ndoa za kikristo hazifuati maandiko? Personalky nadhani ndoa zinafungwa kwa kufuata maandiko lakini wanandoa wanashindwa kutimiza maagizo yaliyotolewa kwenye maandiko ikiwa ni pamoja na kubunja viapo vya ndoa, kushindwa kutimiza majukumu ya ndoa, nk.
Yes!! Ndoa za kikristo haifati maandiko kikamilifu, rudia kusoma uzi nimeshaelezea

Tukianza na viapo tu hapo, Hivi viapo kumbuka vilitungwa na viongozi wa makanisa na wala havipo sehemu yoyote kwenye biblia,,,
 
Mimi mambo ya kabla Yesu kuja kutuokoa huwa

Si ukaoe serikalini na kwenye cheti kuna option ya ndoa ya wake wengi.
Nimekuuliza swali huko nyuma kuhusu kauli yako kwamba mwanaume kuoa wake wengi ni umalaya,

Nakuuliza upya tena, Kina Musa walikuwa malaya ??
 
Yes!! Ndoa za kikristo haifati maandiko kikamilifu, rudia kusoma uzi nimeshaelezea

Tukianza na viapo tu hapo, Hivi viapo kumbuka vilitungwa na viongozi wa makanisa na wala havipo sehemu yoyote kwenye biblia,,,
Kwani ulitaka viapo vya ndoa vitungwe na nani mkuu? Au Yesu ashuke atunge? Hata Biblia imeandikwa na wanaadamu, Mungu ametupa utashi wa kujiongoza au kutengeneza miongozo ndio maana hata nchi inakua na viongozi, sheria za nchi zinatungwa na wanaadamu na hii yote ni utashi ambao mwanadamu amepatiwa na Mungu.
 
Hizo Ndoa za kikristo zimefikia mahala sasa tunaweza kuziita ndoa za kisheria kwasababu watu wanaona mahakamani kuna unafuu kuliko kufata Sheria za ndoa za kikristo.

Usijidanganye kizazi hiki kwamba mke mwema anashushwa na Bwana, Mwanamke unaweza kumchunguza mwaka mzima mkiwa kwenye uchumba na ukaona Yes! Hapa nimepata wife material, Muoe Sasa uone timbwili lake na makucha aliyoficha, hutakosa kuona rangi yoyote, Kiburi kitaanza Kwa jeuri ya ndoa akiona kwamba wote mpo sawa Sasa.

ukienda kuanza kufatilia divorce kanisa linakwambia ulikula kiapo cha kuachana nae mpaka kifo ama uje na ushahidi wa mwenzako ni muashareti, Yani kuleta tu huo ushahidi ni kukiri wazi umechapiwa!! aibu ilioje hii kwa mwanaume! kwanini yasiishe kimya kimya tu, Mbaya zaidi huwezi kutoa talaja hata kama nyumbani hakuna amani, Kuna vipigo, mwenzako ni mchawi, hapendi ndugu zako, n.k hizi sababu kanisa hazizitambui,,, ndio ujinga huu unaofanya wakristo wengi kwenda kuyamaliza mahakamani na hata kuhonga honga wajinasue.

Kuhusu kuona wake wawili napo hapa ni kukaza mafuvu tu hasa kwetu waafrika

Watu wanakuja na utetezi wa mistari Ile ya Kila mwanaume awe na "mke wake", hivi nitoe mfano tu mtu ana wake watu,

mke wa kwanza sio "mke wake"?
mke wa pili sio "mke wake" ?
mke wa tatu sio "mke wake"?

Hata Kwa mwanaume mwenye mke moja nae huyo moja ni mke wake.

Pia tukija Kwa Yesu aliongelea tu kuhusu pale inapobidi umpe talaka mke na Wala hakuzungumzia chochote kuhusu kukataza kuoa mke zaidi ya Moja, wakati huo aliokuwepo kulikiwa na wa Israel wengi tu wenye mke zaidi ya moja kama mababu zao kina Musa walioleta amri 10 za Mungu.

Madhara yake siku hizi wakristo wengi hawana muda na sheria za viongozi wa makanisa wanakimbilia kuyamaliza mahakamani.

kumbana mwanaume kuwa na mke moja matokeo yake ndio haya tunayoyaona michepuko imekuwa kawaida sana siku hizi
Mathayo 19:8-10
Yesu akajibu, “Musa aliwaruhusu kuwataliki wake zenu kwa sababu mlikataa kupokea mafundisho ya Mungu. Lakini talaka haikuruhusiwa hapo mwanzo. 9 Ninawaambia kuwa, kila anayemtaliki mke wake, isipokuwa kutokana na uzinzi, na akamwoa mwanamke mwingine, anazini.”

Acha uzwazwa kuwa unasoma biblia
 
Nimekuuliza swali huko nyuma kuhusu kauli yako kwamba mwanaume kuoa wake wengi ni umalaya,

Nakuuliza upya tena, Kina Musa walikuwa malaya ??
Mathayo 19:8-10

Yesu akajibu, “Musa aliwaruhusu kuwataliki wake zenu kwa sababu mlikataa kupokea mafundisho ya Mungu. Lakini talaka haikuruhusiwa hapo mwanzo. 9 Ninawaambia kuwa, kila anayemtaliki mke wake, isipokuwa kutokana na uzinzi, na akamwoa mwanamke mwingine, anazini.”
 
Ndiyo alikuwa malaya.

Back
Top Bottom