Hizo Ndoa za kikristo zimefikia mahala sasa tunaweza kuziita ndoa za kisheria kwasababu watu wanaona mahakamani kuna unafuu kuliko kufata Sheria za ndoa za kikristo.
Usijidanganye kizazi hiki kwamba mke mwema anashushwa na Bwana, Mwanamke unaweza kumchunguza mwaka mzima mkiwa kwenye uchumba na ukaona Yes! Hapa nimepata wife material, Muoe Sasa uone timbwili lake na makucha aliyoficha, hutakosa kuona rangi yoyote, Kiburi kitaanza Kwa jeuri ya ndoa akiona kwamba wote mpo sawa Sasa.
ukienda kuanza kufatilia divorce kanisa linakwambia ulikula kiapo cha kuachana nae mpaka kifo ama uje na ushahidi wa mwenzako ni muashareti, Yani kuleta tu huo ushahidi ni kukiri wazi umechapiwa!! aibu ilioje hii kwa mwanaume! kwanini yasiishe kimya kimya tu, Mbaya zaidi huwezi kutoa talaja hata kama nyumbani hakuna amani, Kuna vipigo, mwenzako ni mchawi, hapendi ndugu zako, n.k hizi sababu kanisa hazizitambui,,, ndio ujinga huu unaofanya wakristo wengi kwenda kuyamaliza mahakamani na hata kuhonga honga wajinasue.
Kuhusu kuona wake wawili napo hapa ni kukaza mafuvu tu hasa kwetu waafrika
Watu wanakuja na utetezi wa mistari Ile ya Kila mwanaume awe na "mke wake", hivi nitoe mfano tu mtu ana wake watu,
mke wa kwanza sio "mke wake"?
mke wa pili sio "mke wake" ?
mke wa tatu sio "mke wake"?
Hata Kwa mwanaume mwenye mke moja nae huyo moja ni mke wake.
Pia tukija Kwa Yesu aliongelea tu kuhusu pale inapobidi umpe talaka mke na Wala hakuzungumzia chochote kuhusu kukataza kuoa mke zaidi ya Moja, wakati huo aliokuwepo kulikiwa na wa Israel wengi tu wenye mke zaidi ya moja kama mababu zao kina Musa walioleta amri 10 za Mungu.
Madhara yake siku hizi wakristo wengi hawana muda na sheria za viongozi wa makanisa wanakimbilia kuyamaliza mahakamani.
kumbana mwanaume kuwa na mke moja matokeo yake ndio haya tunayoyaona michepuko imekuwa kawaida sana siku hizi