Natafuta Ajira
JF-Expert Member
- Mar 25, 2020
- 14,421
- 40,936
Yap, kiserikali inavunjika, lakini kidini kwa upande wa katoliki ndoa haivunjiki mpaka kifo au itokee mwanandoa mmoja kalukwa akili. Lakini kibongo bongo mara nyingi tunaachana kienyeji tu. Hakuna cha mahakama wala kanisa.Well inawezekana hatujui upande wa pili ila anaruhusiwa kuomba kuvunja kwa mkataba wa ndoa. Ndoa ni mkataba unaosimamiwa na serikali. Upande mmoja ukitaka kutoka usiulazimishe kubaki.
Imeandikwa kuwa mwanaume atamuacha ***** na babae naye ataambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja, basi alichounganisha bwana mwanadamu asikitenganishe, na amuachae mkewe na kuoa mwingine azini na amuoaye mke aliyeachwa azini pia, Musa aliwaandikia kuwa atae kumuacha mkewe amuandikie taraka lakini alifanya hivyo kwa ajili ya ugumu wa mioyo yenu, lakini bwana Yesu anatuambia kuwa hakuna sheria ikupasayo kumuacha mkeo isipokuwa Uasherati.Mshauri/mwelekeze basi hizo sheria
Ok umeeleweka dada angu. Mahakamani mnaweza mkavunja ndoa kwa talaka. Lakini upande wa dini ndoa ya kikristo haivunjiki, sema kibongo bongo tukishindwana huwa tunaachana kienyeji tu.Shida sio kesi mimi sitafuti huruma hapa, nimeelezea tuna mwaka tunazungushwa na usuluishi bila barua ya kuamriwa ili tuendelee na upande mwingine. My dear yan unahis mm natafta huruma ili iweje ikiwa hata sasa nataman kuwa separate…. What i need ni kuanza upya maisha bila kikwazo wala kutembelea njia ya mtu.
Ndoa ya kikristo haivunjiki isipokuwa kwa dhambi ya uzinzi ama kifo!Ok umeeleweka dada angu. Mahakamani mnaweza mkavunja ndoa kwa talaka. Lakini upande wa dini ndoa ya kikristo haivunjiki, sema kibongo bongo tukishindwana huwa tunaachana kienyeji tu.
Shida sio kesi mimi sitafuti huruma hapa, nimeelezea tuna mwaka tunazungushwa na usuluishi bila barua ya kuamriwa ili tuendelee na upande mwingine. My dear yan unahis mm natafta huruma ili iweje ikiwa hata sasa nataman kuwa separate…. What i need ni kuanza upya maisha bila kikwazo wala kutembelea njia ya mtu.
Kuna cheti cha ndoa cha dini? Ndoa zote Tanzania zinavunjwa na mahakama na wanatowa devorce decree.Ndoa ya kikristo haivunjiki isipokuwa kwa dhambi ya uzinzi ama kifo!
Hakuna! Kwa kweli ndiomaana mahakama ya mwanzo ina kazi nyingi sana😅Kuna cheti cha ndoa cha dini? Ndoa zote Tanzania zinavunjwa na mahakama na wanatowa devorce decree.
Yani ukae kifungoni kisa paroko? Wao wenyewe mbona hawaoi unadhani ni wajinga hawajui shida na madhara ya kuingia kwenye ndoa.
Fanya maamuzi ya kiume.Nina myaka 10 kwenye ndoa iliojaa visa, vipigo na kunyan’ganywa umiliki wa mali, Nilipofikia sasa naogopa hadi kununua kijiko kwan ndugu zake wakija ubeba vitu bila kuomba.
Mwaka 2018 vilitangazwa viwanja kigamboni nikamshirikisha mwenzangu kununua akasema ni mbali, nikajipinda nikanunua ila ikawa ugomvi mkubwa sana hadi nimeshindwa kukitaftia hati naogopa…
Mwaka 2022 nikanunua gari nikiwa na malengo ya kufanya tax baadae. Ila akaja na shida nimsaidie kadi ya gari achukulie mkopo bank nikampa kwa maandishi.
Mpaka sasa 2026 sijawai kuiona hio kadi ya gari kila nikiongelea ananiambia nifanye ninalotaka… Nimeshirikisha wazazi na kanisa hakuna matokeo zaidi ya usuluishi kila siku, Natamani kuwa single, nataman kuanza moja ila nazungushwa na usuluishi kila siku.
Siku hizi kuna vituo jumuishi, ndoa na Mirathi vinashughurikiwa hapo, Primary court wameondolewa huo mzigo wa deal na case za msingi tu.Hakuna! Kwa kweli ndiomaana mahakama ya mwanzo ina kazi nyingi sana😅
Yeah ila inategemea na aina ya shauri thamani yake, mfano mirathi yenye utat mkubwa au rufaa kutoka primary court Huwa zinapelekwa magistrate, hivyo vituo jumuishi havibadilishi mamalaka ya mahakama ya mwanzo!Siku hizi kuna vituo jumuishi, ndoa na Mirathi vinashughurikiwa hapo, Primary court wameondolewa huo mzigo wa deal na case za msingi tu.
Vituo jumuishi vina mpaka majaji, sasa Jaji na hakimu nani mkubwa.Yeah ila inategemea na aina ya shauri thamani yake, mfano mirathi yenye utat mkubwa au rufaa kutoka primary court Huwa zinapelekwa magistrate, hivyo vituo jumuishi havibadilishi mamalaka ya mahakama ya mwanzo!
Talaka za kiislamu/kimila mara nyingi zinaishia primary court!
jaji ni mkuu, kwahiyo hizi polisi dawati la jinsia, ustawi wa jamii na msaada wa kisheria zime upgrade siku hizi? Sikuwa najua mkuu!Vituo jumuishi vina mpaka majaji, sasa Jaji na hakimu nani mkubwa.
You are listening too slowly, vituo jumuishi ni mahakama na siyo madawati.jaji ni mkuu, kwahiyo hizi polisi dawati la jinsia, ustawi wa jamii na msaada wa kisheria zime upgrade siku hizi? Sikuwa najua mkuu!
Pole sanaMimi sio singo maza Tuna myaka 10 ya ndoa tulijaliwa mtoto mmoja alifariki 2021 kwa covid.
Nikusahihishe kidogo,Kikatoliki zipo sababu zinazofanya ndoa kuwa batili kama ugonjwa wa muda mrefu (hii ina-apply mmoja akishindwa kutoa tendo la ndoa kwa mwenzake kwa muda mrefu),uzinzi,mwanandoa mmoja kutoonekana (kukimbia) kwa muda mrefu na kama hivyo ukichaa japokuwa Kanisa halihimizi wanandoa kufikia mwisho wa ndoa kwa sababu kama hizi that's why kimewekwa kipengele cha kuvumiliana mpaka kifo.Yap, kiserikali inavunjika, lakini kidini kwa upande wa katoliki ndoa haivunjiki mpaka kifo au itokee mwanandoa mmoja kalukwa akili. Lakini kibongo bongo mara nyingi tunaachana kienyeji tu. Hakuna cha mahakama wala kanisa.
Ni hatari talaka haipaswi kuwa kitu rahisi rahisi mke kazidisha chumvi au sijui mume hajatengewa maji ya kuoga basi mke arudi kwao.Papa yule mjerumani alizungumzia hili tatizo, sio kwamba talaka kwa wakiristo hazipo ila mchakato unakuwa mrefu.
Alisema kuna watu unaweza kuwalazimisha wakae kwenye kumbe matokeo yake yakawa mabaya zaidi, wasiomuelewa wamsema anahalalisha talaka ila kwa ndoa kama hiyo uvumilivu ukifika mwisho ndio tunasikia watu wamechinjana.
Kuna watu unajua kabisa wakiendelea kuishi pamoja ama watawekeana sumu au watakatana mapanga kipi bora, waachane au waendelee kuishi pamoja na kusubiri wauane ndicho alichomaanisha yule papa.Ni hatari talaka haipaswi kuwa kitu rahisi rahisi mke kazidisha chumvi au sijui mume hajatengewa maji ya kuoga basi mke arudi kwao.
Kanisa Katoliki linatetea sana muunganiko wa kifamilia (watoto walelewe na wazazi wao halisi waliowazaa) kwa mustakabali wa kuwa na jamii bora hivyo talaka zikiwa nyepesi sana hali itakuwa mbaya.