NDOTO: Kila nikiota jambo hutokea kama nilivyoota; nifanyeje?

Kipi cha ajabu hapo, wakina Ronaldo, diamond, mbwana samatta n.k. wanatumia vipaji vyao kutajirika, wewe unashangaa nini, kweli masikini ni masikini tu hata Mungu akimpa haoni

Kwa kipato siko level ya masikini sijafikia tu kwenye bilionea ila chini ya hapo nipo siwezi muambia Mungu ni masikini! Tema chini.
 
Kwa kipato siko level ya masikini sijafikia tu kwenye bilionea ila chini ya hapo nipo siwezi muambia Mungu ni masikini! Tema chini.
Tatizo lenu nyie waswahili ukiwa na kanyumba ka vyumba viwili na kabajaji basi unarizika kweli, unajifanya mlokole, haya bana
 
Rejea post yangu hujaisoma ukaelewa, kukurahisishia wapo nnaowaota wamekuwa na baada ya muda flan wanakufa! Hata baadhi ya ndugu zangu waliotangulia niota.
Duh, aseee hatari. Kwahiyo ukiota hivyo huwa unawaambia au?
 
Unasema unasali sana, ili usaidiwe sema dini yako ndipo tutaweza kukushauri.
 
Mkuu kikubwa cha kukushauri jaribu kuichukulia hiyo hali positively, kisha watembelee magwiji wa mambo ya kiroho wakushauri namna bora ya kutumia hiyo karama kwa manufaa yako na manufaa ya watu wengine!

Asante
 
Mungu anasema na wewe,hutakiwi kuomba iondeke hiyo ni kalama. Unatakiwa usali zaidi Ili upate kuonyeshwa zaidi. Hiyo ni nguvu ya kipekee Sana ambayo watu wachache hutunukiwa. Mshukuru Mungu tena jiepushe na dhambi Ili upate kuwa Karibu na Mungu. Kama upo instagram mtafute kaka mmoja anitwa Emanuel of Jesus, kwa Maana Hata Mimi Nina kalama inayoshabihiana na ya kwako,Mimi inakuja kwa mtindo wa mawazo na kuhisi. Huyo kaka alinisaidia Sana kuielewa hii kitu. Au tafuta kiongozu wa kidini aweze kukusaidia zaidi.
 
Ndoto ni macho ya nafsi, maono ni macho ya rohoni kama ilivyo macho ya mwilini. Kila mtu huota ila wengi husahau kwa sababu mbalimbali ikiwemo aina ya vyakula tunavyokula, madawa ya hospitali, uchovu, uzembe na hila za maadui n.k. Nafsi ndo mtu mwenyewe, mwili ni jumba tu (cover). Mungu na maadui kama wachawi akiwemo shetani mwenyewe hutumia nafsi kumfikia mtu kwa njia ya ndoto. Hivyo usipuuze ndoto wala usiseme hutaki ndoto maana utazikosa fursa za maisha yako au kujiona mwenye mikosi, bali tafuta wataalam wa kutafsiri ndoto zako au omba Mungu akupe karama ya kutafsiri ndoto zako. Kwa wakristo-kumbuka Yesu alipotaka kuuawa na Herode, ndoto ya yusuph ilimponya mtoto Yesu. Hivi Yusuph angepuuza kama wengi leo tunavyofanya ingetokea nini? (kumbuka ni ndoto ngapi umepuuza leo zinakugharimu). Mfalme Suleiman alipata hekima ile ndotoni. Ndoto ni za binadam wote bila kujali dini ila matumizi ya ndoto hizo ndo yanatuweka ktk makundi tofauti tofauti kiimani na itikadi. Visivyoonekana ndo vinaoongoza vinavyoonekana. Mwisho soma Ayubu 33:14
 
Nakupongeza kwa kuwa na uwezo huo,, tambua nguvu zako za ndani unaweza kuwa mtabiri
 
Asante ndugu
 

Mkuu mimi sioti ndoto iliyojificha kwamba nahitaji tafsiri inakuwa iko kama ilivyo ndo tukio ama jambo halisi.
 
Kwaharaka naweza sema Una Majini Ya Ruhani tena ni mazuri ,,Hayana shida isipokuwa labda ww uwe Against nayo ,,,sijui hata nikusaidie VP ,,iLa jingine kwakuwa umesema Familia yenu pia Ina watu hawakupendi ,,basi Kuwa makini Sana ,,,

Hapa umetunga jambo lako, nimeeeleza ndugu, rafiki au yoyote....... Sijamaanisha hawanjpendi wakifanya jambo lolote juu yangu najua.
 
Madam Mwajuma mbona hilo boonge la deal......Yaani ningekuwa mimi ningefanya mpango wa kuota nanunua bomberdier tu fasta yaan.
 
Wewe ni bonge la mwanamke, ingekuwa sijaoa ninhekutolea posa. Mm mke wangu nihivyohivyo duuu full mabalaaaa, hatari san nyie watu.

Wakati fulani tulitaka kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine basi full picha la vurugu za uhamisho aliliona kabla. Na akaniambia mawili utaondoka uniache kwa kuanza kuhama wewe au kuacha kazi.

Mm niliacha kazi na yeye baadae kidogo walimpa uhamisho. Safi sana. Huko kwenye vidosho ndio balaa full network bando 5000gb.

Basi nikiamka tu namuuliza leo vipi hujaota? Kama unafanya sana ibada usiache. Mwambie shem aoe kama hujaolewa na kama tayari au bado zinaa usifanye utaoata mambo mazuri sana.

Mke wangu aliniambia hadi kifo cha mama yake alikiona ndotoni, wakati huo akiwa mgonjwa.
 
Mimi hali hii hunitokea sana ya kuota kitu na kutokea ila mara nyingi huwa za matatizo,aidha misiba,ajali pamoja na wizi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…