Sina access na mkubwa yeyote. Kiufupi, hakuna mtu aliyewahi kuniambia, si jambo hilo pekee bali kila nililoliota. Ni sawa na stori ya nabii Elisha na washami ambao kila walipokuwa wakitaka kuvamia Israeli, Elisha alimtahadharisha mfalme wa Israeli kuwa asipite njia flani na hivyo akajiepusha na mashambulizi ya washami.
Ukiwa karibu na Mungu, hatakuficha lolote. na hilo la Rais kufia madarakani, Mungu alinionyesha kama uthibitisho wa mwisho kuwa, kila aliloniambia kuhusu maisha yangu ni la kweli,
yaani kwamba, kama siamini, basi nikiona hilo jambo limetokea, kama nina akili timamu nitajua hata mambo yanihusuyo aliyoniambia, yalikuwa sahihi hata kama niliyapuuzia.