Ahsante kwa maswali mazuri
Kwanza kabisa ili uote kitu lazima kuwepo na kumbu kumbu za taarifa mbali mbali kwenye ubongo wako ( short term and long term memmory).
Hizi kumbu kumbu huhifadhiwa kwenye ubongo wa kati na ubongo wa mbele,
Taarifa zinazopakiwa kwenye ubongo hukusanywa kwa njia kuu 5
- kuona
- kusikia
- Kunusa
- Kuonja
- Na kuhisi kwa ngozi au mitetemo
HIvyo basi mtu aliyezaliwa akiwa kipofu atapakia taarifa kwenye ubongo kwa njia nne tu, ambazo ni kusikia, kunusa, kuonja na kuhisi (mfano kumtambua mtu kwa kumshika, kutambua sehemu au njia inayoelekea chumbani kwa kugusa na fimbo n.k)
Ndoto zake zitakuwa ni za kuota anaambiwa jambo flani, kuota anatembea kwa fimbo kakutana na kitu flani, kuota amekunywa kinywaji flani kizuri, kuota amewasikia watu flani wakiongea jambo flani au kuota jambo lolote la hatari kama vile kudondoma, kuungua, ajari n.k isipokuwa taarifa zinazohusisha kuona tu ndio hataota
Kwenye ubongo kuna sehemu inayohusika na kuiga kwa mtindo wa kioo, yaani ukimuoma mtu flani anafanya jambo flani na wewe unajikuta umeiga au kufanya kama lilivyo mfano mtu akipiga miayo na wewe unaweza ukajikuta tu unapiga miayo automatic,
Hivyo hivyo kwa mzazi akitabasamu mbele ya mtoto basi na mtoto anatabasamu automatic kwa hiyo anakuwa amejifunza kwa mtindo huo wa kioo.
Sijui unanielewa mkuu??