Usiku wa kuamkia leo nimeota ndoto ambayo nimeshindwa kuitafsiri kabisa, picha linaanza ilikua usiku, niko mimi, wife na mwanangu mdogo wa miaka miwili maeneo ya Kamata DSM kama unatokea Posta kuelekea mataa ya Kamata.
Baada ya kuvuka reli kabla ya mataa nakutana na mdada amevaa jezi ya yanga ile ya njano.....ananiuliza nimuelekeze mtaa wenye mafundi...nami namuelekeza mtaa wa Makamba, tukaendelea mbele na wife,wkt huo mwanang nimembeba kifuani nikiwa nimemkumbatia(ndo style nnayopenda kumbeba tukiwa matembezini).
Baada ya kuvuka mataa ya kamata km unaelekea mkuki mall....wife akaongeza mwendo na kuniacha na mtoto nyuma, kumbuka ndotoni hapo ni uck mnene,na hapakua na mtu mwingine barabaran Zaid ya yule dada nlomwelekeza pale nyuma..... baada ya wife kutuacha,pale kwenye bango la digital, anatokea mwanamke from nowhere ananipiga bonge la mtama...naanguka chali lkn still nimemkumbatia mwanang....yule mwanamke anaanza kuniburuza kwa kunivuta mguu ilhali bdo nipo chali...ananivusha barabara km tunaekea kariakoo....tulivyovuka pale jiran na kibanda Cha askar naona Kuna kichaka au kipori kidogo....yule mwanamke anaanza kunikaba na kujarb kunipora mtoto....hapa Kuna Jambo nataka niseme... always nnapokutana na pisi ndotoni hua najarib niwezavyo nimgegede,aidha kwa ushawish au kwa kumbaka.lkn this time sikua na mzuka huo kabisa...nlijitahd sana kumzuia asinipore mtoto lkn alikua na nguv kuliko mm.... nikaanza kukemea kwa njia ya maombi na kutaja sana jina la yesu.... baada ya maombi kwa muda flan yule mwanamke akaanza kuishiwa nguv, nikapata nguv ya kumtoa aliponikaba na kumrusha ktk kichaka karb kilichokua na miiba, akaanza kulia kwa miiba jinsi ilivyokua inamchoma....baada ya hapo wakanizunguka watu kibao kunipa pole/kunipongeza kwa kilichotokea....mm nikawa nalia kwa hisia sana na uchungu mkubwa mixa kwikwi...sikuweza kumjibu yeyote kat yao walionizunguka.nlikua nalia tu....Sasa nikaja kushtuliwa na wife kitandan (live Sasa hapo)kumbe kile kilio na kwikwi nlikua naendanazo live pale kitandan....wife ananiuliza vipi???.... nikiangalia kweli nimeloa machoz balaa...ile rhythm ya kulia bdo nnayo.nlishindwa kumjibu kitu kwakweli ila asibuh nlimsimulia.... kwakweli nmeshndwa kuifafanua hii ndoto inamaana gani???