Ndoto za Chato kuwa mkoa zayeyuka baada ya mikoa jirani kugoma kuachia maeneo yao

Toka lini wananchi wamekuwa na nguvu kiasi hicho nchi hii?
 
Tuombe Mungu iwe hivyo kwa kweli
Zingegawanywa sema Rais Samia amesema Mara nyingi kugawa maeneo sio kipaombele chake kwa Sasa,Ila Jiwe angekuwepo wangeshgawanya kufuta aibu ya hako kachato angagawa Moro na Tabora.

Pia Jiwe alishaahi maeneo Mengi kuyagawa kuanzia Wilaya Hadi Miji mipya.
 
Asante Mungu kwa kutuondolea yule Ibilisi mfitini, mbinafsi, muuaji , fisadi kubwa na lichawi likubwa lililoharibu akili za wananchi wengi ambao mpaka sasa hawawezi kukaa kutwa bila kumtaja
Utaishi milele ibilisi wewe
 
Utaishi milele ibilisi wewe
Kuna mpuuzi mmoja mfuasi wa Jiwe alipoziona post zangu alikasirika sana akasema nitakufa soon.
Nikamwambia kuwa Mimi sio level yake nikampa timeline kuwa baada ya muda fulani nitaenda pm nimsalimie kama tamkuta hai. Tayari hachangii Uzi wowote na pm hayupo online. Tayari ameshamfuata Jiwe.
Kama niliweza kumshawishi Mungu amuue kipenzi chenu ambacho mlikuwa mnakiombea kila wakati nyie vidagaa hamnisumbui
 
😂🙄😂😂😂
 
Sioni uhitaji wa kuelewa mada, wala uhitaji wa Kusoma mabandiko.

Najua, huu ndio Uhasama. Ndio Propaganda hasi, na za Kimkakati.
Mpunguze kuhuzunika. No body wants your PITTY.

Asubuhi njema na ya Amani.
 
Magufuli angeendelea kuishi chato ingekuwa makao makuu ya nchi by 2025!
 
Yule ni mbinafsi na gaidi wa kwanza kutokea tanzania. Alihamishia wanyama burigi chato na kujenga uwanja wa ndege katika kijiji chake, mambo ya kishamba kama hospitali ya rufaa, benk kubwa kubwa vitabaki tembo weupe tu.
Tetesi: Alikuwa na mpango wa kuhamishia mlima kilimanjaro chato! tehe tehe! Mobutu kuku wa zabanga the 2
 
Saizi unaugulia tuu huko [emoji1787][emoji1787]
Mimi siyo wa Chato ila tunasema kwamba mikoa mipya yote Tanzania ilianzishwa kisiasa siyo uhalisia. Kwa hiyo Chato imekosa mtetezi tu vinginevyo ingekuwa ni mkoa tu kama ilivyokuwa kwa Njombe na Katavi. Hata hiyo Manyara ilianzishwa kwa ushawishi wa Waziri Mkuu wa wakati ule. Ndio maana wilaya kama Simanjiro kupelekwa Manyara ni uonevu maana iko karibu sana na Arusha. Aidha, jiulize kwanini Sengerema iwe mkoa wa Mwanza badala ya Geita ambayo ilizaa Sengerema mwaka 1975 ? Na zote ziko ng'ambo ya Ziwa.
Narudia tena uanzishwaji wa mikoa mipya Tanzania ni siasa tu wala hakuna uhalisia.
 
Mengi tu, samaki, dhahabu, misitu na mbuga ya wanyama.
Mbona hayo hadi sasa hayajafanya pachangamke bado pamelala Zzzzzzzzzz hadi mwendazake akalazimisha
-Wanyama pori kuhamishiwa Chato ili eti kuwa na mbuga ya wanyama,hahahaaaaaa
-Kujenga airport,
-CRDB kulazimishwa kuweka tawi wakati hakuna biashara kitendo kilichosababisha majengo yake yamekuwa ni makazi ya popo,
-Traffic light za kuvukia wanyama badala ya magari.

Na bado mikoa ya jirani imegoma kumegwa ili kuanzisha mkoa hewa wa Chato,ina maana wanajua ni galagaja tu.

Huoni ni shida hiyo mzeebaba?
 
Njombe na Katavi Wana Uchumi mkubwa kuliko Mkoa pendekezwa na Sababu za msingi za kugawa zipo ikiwemo ukubwa wa Mikoa husika.

Sasa Kagera,Geita na Kigoma Zina ukubwa gani wa kuhitaji kugawanywa?
Siyo kweli Katavi kuna uchumi gani kuizidi Chato na maeneo yaliyopendekezwa ya Ngara, Kakonko, Biharamulo na Chato yenyewe ? Aidha, hiyo Njombe yenye watu wachache zaidi katika mikoa ya Tanzania bara ina nini cha ajabu zaidi ya miti ya mbao ? Uwe serious kidogo unapotoa hoja.
 
Ndio nakukatalia Sasa ,vigezo vya kuanzisha maeneo ni umbali/Ukubwa,nature of terrain,Idadi ya watu na Potential ya eneo kiuchumi/mapato.

Sasa Njombe ilikidhi vigezo vyote isipokuwa Cha Idadi ya watu lakini vingi ilikidhi..

Hivyo hivyo Katavi,Geita,Manyara nk.

Sasa Chato ya Nini hasa? Kwa vigezo gani? Chato Ni ya kulazimisha kwa sababu binafsi za Mwendazake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…