Ndugai ashukiwa "kama Mwewe" na Mwenezi wa Njombe

Ndugai ashukiwa "kama Mwewe" na Mwenezi wa Njombe

Mbona hamkumwelewa kumbe eeh!? Alisema msikope atatoa zake za mfukon
 
Kufuatia kauli ya Ndugai kupinga serikali kukopa pesa kwaajili ya kumalizia miradi mikubwa iliyoasisiwa na hayati Magufuli, chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa njombe kimeipinga vikali kauli hiyo ya Ndugai ambaye ni spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Akizungumza wakati wa kukagua miradi ya maendeleo ikiwemo madarasa yanayojengwa kwa pesa za UVIKO-19, katibu wa siasa na uenezi mkoa wa njombe, bw Erasto Ngole amemtaka spika Ndugai kuwa na adabu kwani hata katika awamu ya tano serikali ilikopa lakini yeye kama spika hakuwahi kuhoji chochote kuhusu mikopo hiyo na kuwa Tanzania sio nchi pekee inayokopa duniani hivyo aiache serikali ifanye kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Kada huyo nguli amemtaka spika Ndugai kama ana hoja za msingi za kushauri aziwasilishe kwenye vikao vya juu vya chama kwa kufuata utaratibu la sivyo chama kitamshughulikia.

Aidha, kada huyo ameendelea kuwatahadharisha wabunge kuwa makini na spika Ndugai huku akidai kuwa alipata uspika mara mbili kwa kubebwa japokuwa hafai

"Ninawaomba wabunge mumwangalie sana huyu spika wetu, ameingia kwenye uspika mara mbili kwa kubebwa, hakuna asiyejua na tunajua jinsi ulivyoingia kwa kumwondoa makinda mpaka yuko nje tunajua" alisema kada huyo na kuongeza.

Mbali na kashifa ya kumwondoa Makinda kwenye nafasi ya uspika kwa zengwe, kada huyo amemtaka Jobu Ndugai kurudi nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu kupima akili yake kama bado inafanya kazi sawa sawa.

" ulienda India ukatibiwa kwa zaidi ya bilioni mbili za watanzania na inawezekana hujapona ndio maana unaropoka ropoka, inawezekana akili yako bado imeruzi, rudi India wakakucheki tena kama hicho kichwa chako kinafanya kazi sawa sawa".

Katika hatua nyingine, kada huyo kutokea njombe amemtaka spika Ndugai kuacha tabia ya kuchapa viboko watu wanaompinga au kumwambia ukweli

" umezoea wanaokusema kwenye ukweli unawapiga viboko, ulimpiga viboko mgombea mwenzako kule kongwa sasa mimi ni mpigaji mwenzako kama unataka kupiga njoo ukutane na mimi".

Pia, kada huyo amehoji juu ya uwepo wa wabunge 19 bungeni ambao hawana vyama ambapo amedai kwamba ni ishara kuwa spika hana uwezo na hafai kuongoza bunge isipokuwa anatumia ubabe.
Mnhhh!!!!
Ngoma inogileeee....

Ndugai jiuzulu tu.
 
Ndugai alipitishwa na vikao vyote vya CCM tena kwa kupigiwa kura na kuibuka mshindi ndipi jina lake likaenda kupigiwa kura na wabunge wote ambapo aliibuka kidedea kwa kuwashinda wagombea wenzake.

Huyo anayesema Ndugai alimshinda Makinda kwa fitina ni zaidi y kipofu kwa sababu kama ni lawama angezielekeza kwa wajumbe wa vikao vya CCM waliompigia kura Ndugai.

Tafuteni fursa za uteuzi kwa akili basi sio kujitoa ufahanu kwa arguments za kitoto.
Umesahau Magu alivyokuwa anaendesha mambo yake?
 
Ndugai kama anatayapata yote haya angefanya moango ajiuzulu vinginevyo ana wakati mgumu sana.
 
ujasiri wa kumkosoa job anaupata wapi jamani hiki chama cha kijani kimelogwa na nani..anaongea hayo kama hajui job ni mjumbe wa kamati kuuya chama..pia mpaka anafikia hatua ya kuwa mjumbe ,mbunge wa vichaa na bufa la nchi ya wanyonge ni kupitia taratibu za chama ?

kwa maneno ya bwana mdogo ukitazama kiundani zaidi shida sio job na simaanishi job ni mzima la hasha bali chama ndio msingi wa matatizo..kiufupi anakata tawi alilokalia.

itaendelea......
 
Sio Njombe tuu hadi Kilimanjaro kashukiwa 👇

Screenshot_20220101-210149.png
 
Aiseee kwasasa nchini hii inashida, huyo dogo inawezekana anahoja ila anavyoifikisha sasa,nayeye anakuwa muharifu kabisa.......halafu huyu unakuta siku anateuliwa kuwa DC kwaakili hizi tunasafari ndefu.....Ndugai inawezekana katoa ya kweli ila sasa nani atamsikiliza kwasababu ya unafiki wake?
Hakuna anayemsikiliza ndio maana anachekwa nchi nzima.
 
Back
Top Bottom