Ndugai: Taarifa ya CAG imeonyesha ATCL inapata hasara, je tuendelee kununua nyingine?

Spika wa Bunge Job Ndugai amewaasa wbunge kuchangia kwa uwazi bila kuogopa mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022 na sio kusubiri serikali ifeli kisha walaumu

Spika amesemakwa mfano Taarifa ya CAG imeonyesha ATCL imepata hasara ya bilioni 60 na kuuliza je ni sahihi kuendelea kununua ndege nyingine?

Pia ameshauri sekta binafsi kuhusishwa kwenye uwekezaji wa miradi mikubwa kama kununua mabehewa ya treni za kisasa zitakazokuja na sio kila kitu kufanya Serikali huku akisema wabunge nao inabidi washiriki na sio kuwaachia wawekezaji wa kutoka nje pekee japo nayo ni vizuri

Hayo wenye akili tuliyajua hata kabla bombadier ya pili haijatua hapa, Ndugai alisimama kidete kufukuza kina Mdee, Heche, Msigwa ili hayo yasizungumzwe na hata kukataa hotuba za bajeti ya wapinzani leo ndio anataka wafunguke si unafiki uliopitiliza?!
 
Huyu bogus mwingine watu kama hawa ndio wanachochea fikra za kijinga kwenye jamii.

I can understand angesema TRC isiwe na monopoly kama shirika la leri, wapate washindani. Lakini sio nonsense sasa mtu akishanunua mabehewa ayapeleke wapi wakati hana train za kuendeshea, si ndio ataishia kuyakodisha TRC na kubadilisha business model yao.

Ina maana TRC ianze kulipa riba za watu wanaokopa bank ovyo kwa riba za juu na kuwapa faida hao wawekezaji uchwara kama ilivyozoeleka miaka ya nyuma ukitaka hela ya haraka fanya biashara na serikali.

Kila mtu anaanza kuwa mwehu sasa.
 
Kama unakuwa mwanasiasa halafu ukawa kila siku kabla hujafunga macho upumzike husali na kuomba toba kwa Mungu unayemwamini basi una possibility kubwa sana ya kukutana na hukumu mbaya siku ukiicha hii dunia.

Maana hawa watu maisha yao kwa asilimia kubwa yamezungukwa na ujanja ujanja sana ni kusema hakuna siku inayoisha mwanasiasa hajatenda dhambi ya uwongo,huyu ungemuuliza kuhusu hili miezi miwili nyuma angekujibu kitu tofauti na anachosema leo.
 
Spika wa Bunge Job Ndugai amewaasa wbunge kuchangia kwa uwazi bila kuogopa mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022 na sio kusubiri serikali ifeli kisha walaumu

Spika amesemakwa mfano Taarifa ya CAG imeonyesha ATCL imepata hasara ya bilioni 60 na kuuliza je ni sahihi kuendelea kununua ndege nyingine?

Pia ameshauri sekta binafsi kuhusishwa kwenye uwekezaji wa miradi mikubwa kama kununua mabehewa ya treni za kisasa zitakazokuja na sio kila kitu kufanya Serikali huku akisema wabunge nao inabidi washiriki na sio kuwaachia wawekezaji wa kutoka nje pekee japo nayo ni vizuri

nchi hii ninaimani na Lisu hata asipopata uraisi
 
Ndugai naona mitazamo yake ya kiuchumi ni kama ya Samia Suluhu. Yule jamaa aliyekuwa anaua sekta binafsi alikuwa anaturudisha miaka 40 nyuma
Watu mnalumu tu kwa nini hawakuongea Magufuli akiwa madarakani, pengine mlikuwa hamumjui Magufuli
Leo ndo umejua alikuwa anauwa sekta binfsi siyo?siye wewe ukipita humu macho juu juu kupingana na waliokuwa wanamkataa?
 
Hayo wenye akili tuliyajua hata kabla bombadier ya pili haijatua hapa, Ndugai alisimama kidete kufukuza kina Mdee, Heche, Msigwa ili hayo yasizungumzwe na hata kukataa hotuba za bajeti ya wapinzani leo ndio anataka wafunguke si unafiki uliopitiliza?!
Kabla ya uchaguzi huyu Ndungai alisema hawahitaji wabunge makini sana, wanachohitaji ni 3/4 ya wabunge wawe CCM ili hoja zao zipite.

Hii badget inajadiliwa na watu wasio makini.
 
Spika wa Bunge Job Ndugai amewaasa wbunge kuchangia kwa uwazi bila kuogopa mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022 na sio kusubiri serikali ifeli kisha walaumu

Spika amesemakwa mfano Taarifa ya CAG imeonyesha ATCL imepata hasara ya bilioni 60 na kuuliza je ni sahihi kuendelea kununua ndege nyingine?

Pia ameshauri sekta binafsi kuhusishwa kwenye uwekezaji wa miradi mikubwa kama kununua mabehewa ya treni za kisasa zitakazokuja na sio kila kitu kufanya Serikali huku akisema wabunge nao inabidi washiriki na sio kuwaachia wawekezaji wa kutoka nje pekee japo nayo ni vizuri

Duh! Huyu ndiye alikuwa kimbelembele kupokea ndege na kusifia leo kageuka?. Wanafiki hawataisha hadi kiama, kageuka Yuda Isikariote.
 
Back
Top Bottom