Ndugai: Taarifa ya CAG imeonyesha ATCL inapata hasara, je tuendelee kununua nyingine?

Ndugai: Taarifa ya CAG imeonyesha ATCL inapata hasara, je tuendelee kununua nyingine?

Hahahaaa madege waliyapokea naye akiwepo mstari wambele na ngonjera bungeni za kumpongeza aliyenunua,Leo imekuwa hasara tupu!! Bora yangenunuliwa kwa mkopo!! Sasa wanataka kustop kuleta nyingine nao walishalipia??
Hayati alisema tusibinafsishe vitu muhimu ikiwemo treni zetu Leo hayupo wanataka binafsisha kijanja janja kujidai PPR...mbona ndege hamkutaka PPR mpaka fastjet ikapotea?
Bunge lililopita litaingia kwenye rekodi kama bnge dhaifu lakini hili linaweza ingia kama bnge ondoa dhai weka m kabisa!! Na spwika huyu akiwa kinara wa kuliangamiza!
Siku zote "Haramu haizai halali" tusiweke vitu haramu kwenye bunge tena linaloanza na sala alafu tukategemea matokeo mazuri Abadan!!
 
Hivi CAG amekagua na ofisi ya huyu mnafiki ?Huyu nae amechangia kuliingiza hasara taifa kwa kutumia pesa za walipa kodi kwa masilahi ya chama chake tena ikiwa ni kinyume cha katiba ya nchi yetu.Huyu aliewakumbatia na kuwakingia kifua wabunge wasio kuwa wanachama wa chama chochote cha siasa katika bunge lilopita;huku akiwalipa mamilioni ya shilingi kwa posho,mishahara na pensheni leo bila aibu anajifanya kusahau yeye pia ni sehemu ya tatizo iliyotufisha hapo.Asitegemee kwa matamko hayo atarudisha utu na heshima alivyoviweka rehani kwa upofu wa madaraka pengine labda atangaze kujiuzu Kama kweli hakubaliani na yaliyotendeka kipindi cha JPM. Ndugai ni spika wa ovyo kutokea toka tupate uhuru.
Kweli ofisi ya ndugai inabidi ikaguliwe
 
Duh Kazi kuliko hii...

Kwahio alidhani huwa tunapiga faida ?

Na kuwashauri hao wabunge wawe wawekezaji wa hayo mabehewa n.k. (isije ikawa mtunga sheria akajitungia ya kujinufaisha mwenyewe) Au tunawalipa pesa nyingi sana tuwapunguzie?

Sioni ubaya wa mfanyabiashara akiwa mbunge ila kuna ukukasi ya wabunge wakiwa wafanyabiashara (self interest might take its cause)
 
Ndugai naona mitazamo yake ya kiuchumi ni kama ya Samia Suluhu. Yule jamaa aliyekuwa anaua sekta binafsi alikuwa anaturudisha miaka 40 nyuma na wala hashauriki
Watu mnalumu tu kwa nini hawakuongea Magufuli akiwa madarakani, pengine mlikuwa hamumjui Magufuli. Pengine waliona anaharibu sana na haambiliki wakaamua wamtangulize tu kama baadhi ya watu wanavyodai
Good points
 
Ilani ya ccm 2020 - 2025 inasema tutaendelea kupambana na rushwa na ufisadi kwa nguvu zote.


Haisemi ufisadi umeisha.

Hata Ulaya kina Morinyo, Messi, Ronaldo mara kwa mara tunasikia aamepelekwa mahakamani kwa kukwepa kodi.

Hata Chadema wabunge wengi walihama mwaka jana sababu ya ufisadi michango yao. Kinachotakiwa ni kuendelea kupambana na ufisadi
Utaugua bure maradhi yasioambukiza.
Enenda ukatubu na ujitoe kutoka waliokuwa wanaishi kwa kumuimbia shetani mapambio, itakusaidia.
Ukimaliza yafaa ushiriki katika kumtaka Ndugai na wanafiki wengine waanze kujiuzulu kwa hiyari.
 
Spika wa Bunge Job Ndugai amewaasa wbunge kuchangia kwa uwazi bila kuogopa mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022 na sio kusubiri serikali ifeli kisha walaumu

Spika amesemakwa mfano Taarifa ya CAG imeonyesha ATCL imepata hasara ya bilioni 60 na kuuliza je ni sahihi kuendelea kununua ndege nyingine?

Pia ameshauri sekta binafsi kuhusishwa kwenye uwekezaji wa miradi mikubwa kama kununua mabehewa ya treni za kisasa zitakazokuja na sio kila kitu kufanya Serikali huku akisema wabunge nao inabidi washiriki na sio kuwaachia wawekezaji wa kutoka nje pekee japo nayo ni vizuri


Hajasema wapinzani wamewachelewesha?
 
sasa mtu akishanunua mabehewa ayapeleke wapi wakati hana train za kuendeshea, si ndio ataishia kuyakodisha TRC na kubadilisha business model yao
Kampuni ya usafirishaji binafsi inaweza kutumia mabehewa kwa shughuli zake binafsi mbadala wa malori.Rejea kitu anachokifanya bakhresa na shirika la reli!
 
Back
Top Bottom