Ndugai: Taarifa ya CAG imeonyesha ATCL inapata hasara, je tuendelee kununua nyingine?

Ndugai: Taarifa ya CAG imeonyesha ATCL inapata hasara, je tuendelee kununua nyingine?

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
8,984
Reaction score
19,288
Spika wa Bunge Job Ndugai amewaasa wabunge kuchangia kwa uwazi bila kuogopa mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022 na sio kusubiri serikali ifeli kisha walaumu.

Spika amesema kwa mfano Taarifa ya CAG imeonyesha ATCL imepata hasara ya bilioni 60 na kuuliza; je ni sahihi kuendelea kununua ndege nyingine?

Pia ameshauri sekta binafsi kuhusishwa kwenye uwekezaji wa miradi mikubwa kama kununua mabehewa ya treni za kisasa zitakazokuja na sio kila kitu kufanya Serikali huku akisema wabunge nao inabidi washiriki na sio kuwaachia wawekezaji wa kutoka nje pekee japo nayo ni vizuri.

 
Ndugai naona mitazamo yake ya kiuchumi ni kama ya Samia Suluhu. Yule jamaa aliyekuwa anaua sekta binafsi alikuwa anaturudisha miaka 40 nyuma na wala hashauriki. Mashirika binafsi ya ndege alifanya juhudi yafe wakati ATCL ni hasara, PPP ilikuwa imeshakufa.

Watu mnalumu tu kwa nini hawakuongea Magufuli akiwa madarakani, pengine mlikuwa hamumjui Magufuli. Pengine waliona anaharibu sana na haambiliki wakaamua wamtangulize tu kama baadhi ya watu wanavyodai.
 
Spika wa Bunge Job Ndugai amewaasa wbunge kuchangia kwa uwazi bila kuogopa mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022 na sio kusubiri serikali ifeli kisha walaumu

Spika amesemakwa mfano Taarifa ya CAG imeonyesha ATCL imepata hasara ya bilioni 60 na kuuliza je ni sahihi kuendelea kununua ndege nyingine?

Pia ameshauri sekta binafsi kuhusishwa kwenye uwekezaji wa miradi mikubwa kama kununua mabehewa ya treni za kisasa zitakazokuja na sio kila kitu kufanya Serikali huku akisema wabunge nao inabidi washiriki na sio kuwaachia wawekezaji wa kutoka nje pekee japo nayo ni vizuri


ndo hasara ya kuwekwa bunge mfukoni na jiwe,haoni sasa kachelewa huyu sabufa naye
 
Spika wa Bunge Job Ndugai amewaasa wbunge kuchangia kwa uwazi bila kuogopa mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022 na sio kusubiri serikali ifeli kisha walaumu

Spika amesemakwa mfano Taarifa ya CAG imeonyesha ATCL imepata hasara ya bilioni 60 na kuuliza je ni sahihi kuendelea kununua ndege nyingine?

Pia ameshauri sekta binafsi kuhusishwa kwenye uwekezaji wa miradi mikubwa kama kununua mabehewa ya treni za kisasa zitakazokuja na sio kila kitu kufanya Serikali huku akisema wabunge nao inabidi washiriki na sio kuwaachia wawekezaji wa kutoka nje pekee japo nayo ni vizuri

Ilani ya ccm 2020 - 2025 inasema tutaendelea kupambana na rushwa na ufisadi kwa nguvu zote.


Haisemi ufisadi umeisha.

Hata Ulaya kina Morinyo, Messi, Ronaldo mara kwa mara tunasikia aamepelekwa mahakamani kwa kukwepa kodi.

Hata Chadema wabunge wengi walihama mwaka jana sababu ya ufisadi michango yao. Kinachotakiwa ni kuendelea kupambana na ufisadi
 
April 8, 2021

CAG: BODI YA WAKURUGENZI YA ATCL HAINA MJUMBE MWENYE UZOEFU NA MASUALA YA ANGA

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amesema hayo na pia kuongeza kuwa Shirika linadaiwa hivyo inakuwa changamoto kuruka kwenye baadhi ya maeneo kwani viwanja haviruhusi ndege ya airbus ikiwa imejaza abiri viti vyote kutua, mojawapo ya kiwanja hicho ni cha Dodoma.

Kipindi cha korona wakati ndege haziruki, Wakala wa Ndege za serikali TGFA imeendelea kuitoza ushuru wa jumla ya shs. 12.5 bilioni shirika la ATCL kutokana na mkataba mbovu usioangalia maslahi ya ATCL huku ndege hizo zimepaki uwanjani bila kufanya kazi.

Pia Viwanja vya Ndege vimetajwa kuwa na changamoto kutoweza kufanya kazi usiku.

Ripoti ya CAG inabainisha kuwa ATCL inasita kwenda ktk baadhi ya nchi kutokana na madeni mengi hivyo kuhofia ndege kukamatwa na wanaoidai Air Tanzania. Kukamatwa kwa ndege ya ATCL kule Afrika ya Kusini ni moja ya mfano hai wa ATCL kufanya kazi chini ya changamoto nyingi.

Habari toka intaneti​

19 Mei, 2020 Ikulu Chamwino, Dodoma​

Mheshimiwa Kapt (Mst) George H. Mkuchika azindua Bodi ya ushauri ya Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA),​


d41d0aa673397ad06155f58a2afc4450

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Kapt (Mst) George H. Mkuchika, leo tarehe 19 Mei, 2020 amezindua rasmi Bodi ya Ushauri ya Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA), katika hafla fupi iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano ya Makatibu Wakuu, Ikulu Chamwino, Dodoma.

Katika hotuba yake ya uzinduzi, Mheshimiwa Waziri alichukua nafasi hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kwa kumteua Balozi Mhandisi John W.H. Kijazi ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo. “Hii inaonyesha jinsi gani ambavyo Mheshimiwa Rais amelipa uzito jukumu la Usimamizi wa TGFA. Napenda kukupongeza sana wewe pamoja na Wajumbe wa Bodi kwa uteuzi wenu”.

Alisisitiza Mheshimiwa Waziri
Wakala ya Ndege za Serikali ilianzishwa rasmi tarehe 17 Mei, 2002 kupitia Sheria ya Wakala za Serikali Na. 30 ya Mwaka 1997 kama ilivyorekebishwa Mwaka 2009.

Wakati wa kuanzishwa kwake, Wakala hii ilikuwa chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Tarehe 23 Aprili, 2018, Serikali iliamua kuihamisha Wakala hii kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwenda Ofisi ya Rais, Ikulu kwa Tangazo la Serikali Na. 252 la tarehe 8 Juni, 2018.

Wakala ya Ndege za Serikali inatekeleza majukumu makubwa matatu (3). Kwanza, ni kutoa huduma ya usafiri wa anga kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Viongozi Wakuu wa Kitaifa kwa usalama na viwango vya hali ya juu.

Pili, ni kuratibu na kusimamia ununuzi na ukodishaji wa ndege za Serikali kwa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL).

Tatu, ni kuendesha na kufanya matengenezo ya ndege za Serikali kwa ufanisi unaozingatia viwango vya hali ya juu vya usalama.

“Majukumu haya ni nyeti sana, ni matarajio yangu kwamba mtailinda imani na heshima kubwa aliyowapeni Mheshimiwa Rais kwa kuhakikisha kwamba mnaisimamia vizuri Wakala ya Ndege za Serikali ili kuiwezesha kutekeleza majukumu yake ipasavyo”.

Alisisitiza Mheshimiwa Waziri
Mheshimiwa Waziri alibainisha kuwa, moja ya vipaumbele vikubwa vya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuimarisha sekta ya usafiri wa anga.

Sote tunafahamu kwamba hadi sasa Serikali imenunua ndege mpya 11. Kati ya ndege hizo, ndege nane (8) tayari zimeshapokelewa na zimeshakodishwa ATCL. Na kama alivyoeleza Mwenyekiti, ndege tatu (3) ndio zinatengenezwa na zinatarajiwa kuwasili nchini kati ya sasa na mwezi Juni, 2021.

Lengo la Serikali ni kuona kwamba Tanzania inakuwa na Shirika la Ndege imara litakaloweza kushindana na mashirika mengine ya kikanda na kimataifa kwa kuanzisha na kuendesha safari nyingi za ndani ya nchi, za kikanda na za kimataifa”.


Ningependa nisistize pia kwamba suala la kuimarisha usafiri wa anga kwa kulifufua Shirika la Ndege la Tanzania ni moja ya ahadi za Chama cha Mapinduzi iliyopo kwenye Ilani yake ya Uchaguzi ya Mwaka 2015.

Hivyo, mageuzi makubwa yaliyofanyika kataika sekta ya usafiri wa anga katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano ni utekelezaji wa Ilani hii ya CCM.

Mheshimiwa Waziri aliwaeleza Wajumbe wa Bodi hiyo kuwa, kimuundo Bodi hiyo ni chombo cha kumshauri Waziri. Hivyo ni matarajio yake kwamba mara kwa mara atapatiwa ushauri wa namna ya kuboresha ufanisi wa Wakala ya Ndege za Serikali ili kuweza kufikia malengo ya Serikali.

TGFA na ATCL zote ni taasisi za Serikali. Ni matarajio ya Serikali kuona taasisi hizi zinafanya kazi kwa ushirikiano wa karibu. Ni bahati nzuri Mwenyekiti wa Bodi hii pia ndiye Mkuu wa Utumishi wa Umma nchini. Anayo mamlaka makubwa pamoja na rasilimali za kutosha anazoweza kuzitumia kuhakikisha kwamba taasisi hizi mbili zinafanya kazi kwa ushirikiano wenye tija.

Akimalizia hotuba yake ya uzinduzi, Mheshimiwa Waziri alisisitiza kwamba ni matarajio yake kwamba Bodi itasimamia kikamilifu Wakala ya Ndege za Serikali na kuhakikisha kwamba inakuwa na mipango na mikakati mizuri itakayoleta tija katika utekelezaji wa majukumu iliyokabidhiwa ikiendana sambamba na udhibiti wa matumizi ya fedha za umma na usimamizi wa makusanyo ya fedha ya Serikali yatokanayo na ukodishwaji wa ndege kwa ATCL.

Awali kabla ya hotuba ya Mheshimiwa Waziri, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Balozi Mhandisi John W.H. Kijazi ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi, alitoa maelezo mafupi kuhusiana na mikakati ya bodi hiyo katika kutekeleza majukumu yake pamoja na changamoto zinazoikabili Wakala ya Ndege za Serikali.

Na alichukua nafasi hiyo kwa niaba ya Wajumbe wa Bodi kumshukuru Mheshimwa Rais, Dkt. John P. Magufuli kwa kuwa na imani nao na kuwateua kuitumikia bodi hiyo na Serikali kwa Ujumla na kuahidi kuwa watatekeleza majukumu yao kiuweledi na kikamilifu.

Baada ya Mheshimiwa Waziri kuizindua bodi hiyo, wajumbe waliendelea na kikao ambacho kilikuwa ni cha kwanza kufanyika baada ya kuzinduliwa kwake

Source : Katibu Mkuu Kiongozi | Habari
 
Wakati ule wabunge wa upinzani wanatoa Maoni kuhusu hili shirika mliwaita mawakala wa mabeberu, sio wazalendo, wanatumika na meneno mengine kibao hadi wengine kupewa adhabu za ovyo ovyo.

Leo mmeingiza nchi hasara mnasema wabunge wachangie kwa uwazi, wabunge wenyewe wako wapi wa kuchangia kwa uwazi.?

Hawa akina Babu Taletale? Waliopelekwa bungeni kama watoto wanapelekwa chekechea..

CCM na Mwendazake mmeifirisi sana nchi hii na bado mnaendelea kuifirisi na kutuona Watanzania kama mazwazwa.

Halafu Spika bila aibu unashauri watu binafsi wanunue mabehewa halafu wawakodishie shirika la Reli si ndio....Yaani unataka uozo uliopo Tanesco uhamie na shirika la Reli sasa sio.?
 
Back
Top Bottom