Ndugai: Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo uendelee, Dkt. Magufuli alishauriwa vibaya

Ndugai: Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo uendelee, Dkt. Magufuli alishauriwa vibaya

Hii watoto wa mjini wanaita fungulia mbwa maccm yana miminika na facts kudadadeki.[emoji1787]
 
Naomba nipingane na Mh. Spika 100%... Mungu njoo tusaidie, Mungu tusaidie, presentation sio sbb, ukubwa wa mradi sio sbb, mradi wa Bagamoyo utakausha nchi yetu na Rasilimali zote ndani ya miaka 99 au 50 ijayo, kila kitu kitakuwa kimeisha, sbb ukiwapa Chinese ku operate kwa 99 or 50 yrs alafu mmpewe kuendesha hiyo Bandari, itakuwa hakuna kitu hapa Tanzania.. Naumia sana kwa Ndugai kusema haya bila kuwa na datas, anasema ukubwa tu akidhania ndio faida, kumbe isiyo na faida..

Mungu tusaidie jamani.. Mungu tusaidie, Spika amekuwa very theorical badala ya kuangalia deep inside Chinese economic Intelligence yao, ni hatari sana.

Wachina wakishika Bandari wakijenga kwa miaka 99 hakuna kodi ya Bandari, hakuna kipato serikalini, we depend sana kwenye mapato ya bandari, hivi hata huo mshahara spika atapata kweli?

Miaka 99 au 50 tusiwe na Bandari, yaani Chinese millitary waendeshe, sisi tutamalizwa na madini na rasilimali zoteee zitaisha nchii yetu.. Yaani Spika bado hajawajua Chinese hadi leo hii anawaita marafiki? Mchina wa leo unamwita Rafiki?

Mungu tusaidie jamani
 
Mnaotaka 'mkataba' uwekwe wazi nawaonea huruma sana.. perhaps your level of naivete is astonishing!
Binafsi sihitaji mkataba, lakini JPM (RIP) alishotudokeza mambo ya kipuuzi yaliyomo kwa ufupi. Waseme tu ni kweli au hapana? na ukweli ni upi then tutamuona JPM hakujua kitu.
 
Kumaliza utata mkataba huo uwekwe wazi uanikwe hadharani. Wazee akina Ndugai musije achia vizazi vijavyo mizigo isiyowahusu si vizuri kurithisha kizazi kingine zigo Wanamchi tunaomba uwekwe wazi sababu ni wa miaka mingi pengine wote tuliopo hatutakuwepo duniani tutalaaniwa na vizazi vijavyo...

Utawekewa na nani wakati kila upuuzi wa ccm ulikuwa ukuunga mkono, na kuishia kulishwa upuuzi kuwa ccm ni chama imara badala ya majizi ya kura? Spika huyu huyu enzi za Magufuli alisema tena kwa mbwembwe kuwa mradi wa Bagamoyo ni hatari kwa nchi hii.

Leo Magufuli kafariki hana hata mwezi Ndugai huyo huyo anasema mradi wa Bagamoyo rais alishauriwa vibaya. Kibaya zaidi wapuuzi wa aina hiyo ndio waliiba kura na kujaza bungeni kwa kujifanya ni wazalendo, na ndio wanaolinda maslahi ya nchi.

Sasa subiri uone vile ule mradi wa SG utaachwa hewani, na watu kurudi kwenye gas. Hapo ndio utajua jinsi Magufuli alivyoharibu demokrasia ya nchi hii, na sasa nchi inaenda kupata janga kubwa bila kuwa na watu wa kupiga kelele.
 
Kuna jambo naliona kwa wanasiasa wetu ni kwamba wana mutate haraka kazi kuwaelewa!!
 
Ajibu zile hoja za JPM kwanza zilizomfanya akaukataa.
 
Binafsi sihitaji mkataba, lakini JPM (RIP) alishotudokeza mambo ya kipuuzi yaliyomo kwa ufupi. Waseme tu ni kweli au hapana? na ukweli ni upi then tutamuona JPM hakujua kitu.
Sasa ndio utajua ni kwa kiwango gani hilo genge liitwalo ccm ni hatari kwa nchi hii. Hao ambao wiki tatu zilizopita walikuwa wanajifanya wazalendo kwa kuepusha nchi na mikataba ya wizi, ndio haohao wanarudi kwa kasi kwenye mikataba waliyokuwa wanasema ni ya hatari kwa nchi.
 
Kweli mkuu,ila kuna shida kubwa sana kwa vingozi wetu,hivi hofu yao ilikuwa nini hadi wakawa wanamkubalia kila kitu mheshimiwa hayati JPM, uchu Wa madaraka au unafiki?...
Kwa hiyo inawezekana hata hizo report ya CAG ni kutupumbaza kwanza tuone JPM aliharibu kila kitu kumbe wana lao jambo?
 
Kumaliza utata mkataba huo uwekwe wazi uanikwe hadharani. Wazee akina Ndugai musije achia vizazi vijavyo mizigo isiyowahusu si vizuri kurithisha kizazi kingine zigo Wanamchi tunaomba uwekwe wazi sababu ni wa miaka mingi pengine wote tuliopo hatutakuwepo duniani tutalaaniwa na vizazi vijavyo...
Vipi kuhusu tunavyowaachia deni la Taifa, halina laana?
 
Utawekewa na nani wakati kila upuuzi wa ccm ulikuwa ukuunga mkono, na kuishia kulishwa upuuzi kuwa ccm ni chama imara badala ya majizi ya kura? Spika huyu huyu enzi za Magufuli alisema tena kwa mbwembwe kuwa mradi wa Bagamoyo ni hatari kwa nchi hii....
Kwenye big three za samia hiyo gas ni number 2. yeye anaiita LNG ili waswahili wasielewe anazungumzia nini
 
Du! Kweli kuna mabadiliko na hata mhimili wa Bunge umepata sauti ya kuongea.

Mkuu wala sio mabadiliko yenye tija maana wanachofanya ni hatari hata kqa nchi. Maana usishangae akifa rais huyu wakapata mabadiliko tena?
 
Dar es Salaam. Spika wa Bunge, Job Ndugai amebadilisha msimamo wake kuhusu ujenzi wa mradi mkubwa wa ukanda maalumu wa kiuchumi wa Bagamoyo (Bagamoyo SEZ) mkoani Pwani akisema awali yeye na wabunge wenzake hawakuyajua masharti ya mradi huo bali waliangalia tu faida zake.

Kauli ya Ndugai imekuja ikiwa ni siku moja baada ya Rais John Magufuli kupigilia msumari wa mwisho wa zuio la ujenzi wa bandari hiyo, alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara juzi Ikulu jijini Dar es Salaam akisema masharti magumu ya mwekezaji ndiyo sababu inayoufanya usitekelezwe.

Magufuli alisema miongoni mwa masharti hayo ni pamoja na kuwa baada ya ujenzi huo wa bandari kukamilika, Tanzania haitaruhusiwa kujenga na kuendeleza bandari nyingine yoyote Pwani ya Bahari ya Hindi kuanzia Tanga mpaka Mtwara.

Pia alisema wawekezaji hao walitaka wakishajenga bandari hiyo, Tanzania isiruhusiwe kukusanya kodi katika bandari hiyo. Rais Magufuli alisema sharti jingine katika mkataba wa ujenzi wa mradi huo ni kuwa wanatakiwa kupewa muda wa miaka 33 bila kuwauliza chochote watakapokuwa wamewekeza hapo, pamoja na kuwalipa wale watakaokuwa wanafanya kazi ya kuchimba hiyo bandari.

Rais Magufuli aliwaeleza wafanyabiashara kuwa masharti hayo ni magumu na yalikuwa na lengo la kuua bandari nyingine za Tanzania ambazo zinaendelezwa huku akisema Serikali ilifanya utafiti wa kutosha na kuona uwekezaji huo hautakuwa na tija kwa Taifa zaidi ya kuwaumiza Watanzania.

Machi 13, Spika Ndugai wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano bungeni Dodoma yeye na wabunge waliihoji Serikali kwa nini haitekelezi mradi huo ambao hadi kukamilika kwake ungezalisha ajira zaidi ya 1,000 na viwanda vingi vingejegwa.

Hata hivyo, Spika Ndugai akizungumza na Mwananchi kwa simu jana alisema awali hawakuyajua masharti hayo.

“Sisi hatukuwa na taarifa ya masharti ya nyongeza ambayo mheshimiwa Rais ameyaeleza. Katika majadiliano kati ya Serikali na wawekezaji, wakati mwingine siyo kwamba tunaangalia mambo yote, huwa tunaangalia faida za mradi,” alisema Ndugai.

Aliendelea, “Lakini Rais ameeleza masharti kwa mfano kuzuia bandari zote kuanzia Tanga hadi Mtwara zisifanye kazi. Sasa masharti kama hayo ni ya kipumbavu sana, ya kijinga, sijui hata. Haiwezekani kutekeleza huo mradi kwa masharti hayo.”

“Kwamba sisi tusikusanye kodi kwa miaka 100 ni vitu vya ajabu sana. Rais akishasema basi. Kwa masharti yake hayo, haufai kabisa. Lakini kwa zile faida tulikuwa tunaangalia, kumbe kuna masharti hasi ambayo wabunge hawakuyajua,” aliongeza Ndugai.

Maoni ya Ndugai pia yameungwa mkono na Mbunge wa Hanang, Dk Mary Nagu ambaye ndiye alitia saini ujenzi wa bandari hiyo alipokuwa waziri katika Serikali ya awamu ya nne, akisema kwa kuwa muda umebadilika hawezi kutofautiana na Rais.

“Sisi tuliona bandari ni eneo muhimu la uchumi ambalo lingekuwa na maeneo ya mengi ya kuzalisha. “Mimi nilikuwa waziri na hata yeye (Rais) alikuwa waziri na mambo makubwa kama yale yalikuwa lazima yapitishwe na Baraza la Mawaziri. Lakini kwa kuwa wakati umebadilika sioni sababu ya kutofautiana naye,” alisema Dk Nagu.

Advertisement

Screenshot_20210408_213609_com.android.chrome.jpg
Screenshot_20210408_213619_com.android.chrome.jpg
 
Spika alikuwa anamwogopa Rais ndo tafsiri halisi ya alichosema ndugai
 
Back
Top Bottom