Ndugai: Wabunge ishaurini Serikali, iendelee kununua ndege au isitishe

Cannabis

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
11,557
Reaction score
33,535
81f99676f032b0726d3e8059c65900c6.jpeg

Dodoma. Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amewataka wabunge kuchangia Mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa kuishauri Serikali kama iendelee na mpango wake wa kununua ndege au isitishe hadi itakapoweka mambo sawa.

Ndugai amesema hayo bungeni mjini Dodoma leo Alhamisi Aprili 8, 2021 kabla kuchangia Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo (2021/22 hadi 2025/26) uliosomwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba.

Amesema Shirika la Ndege (ATCL) limepata hasara ya Sh60 bilioni, hivyo wabunge wanatakiwa kuishauri Serikali wakati wakichangia mpango huo kama iendelee na mpango wa kuongeza ununuzi wa ndege au wasitishe kwanza hadi watakapoweka mambo sawa.

Amewataka wabunge hao kushauri pia katika ununuzi wa mabehewa kwa ajili ya uendeshaji wa reli ya kisasa (SGR) kama ni vyema yakanunuliwa na Serikali au ununuzi ukafanywa na wabia wa sekta binafsi.

Amesema zipo nchi zinafanya uwekezaji wa miundombinu ya reli na suala la mabehewa linafanywa na wawekezaji binafsi.

Amewataka wabunge kutumia nafasi hiyo kuishauri Serikali na wasisubiri kukosa wakati inapokosea.
 
Ripoti ya CAG isiwatishe, tuendelee mbele. Kenya airway moja ya mashirika kongwe ya ndege Africa limepata hasara bil.zaidi ya 700 na bado linahudumu, sisi bil. 60 unaogopa kununua ndege. Hata tupate hasara ili mradi linaingia nchi mbali mbalimbali ni namna ya kuitangaza Tanzania duniani.
 
Billion 700 sababi ya capital yao, fleet, operating capital pia ni kubwa kuliko yetu. Compare na Rwanda Air kidogo ndio level zetu
 
Hahahahaha dabliusibii..anawadanganyia na viuno vyake hahahah
Ndiyo maana aliimba “Maghufuli baba lao”😂. Hapo walipewa milioni 140 kwa mikoa sita. Ina maana zaidi ya milioni 20 kila mkoa! Duh! Sijui tulikuwa tunaelekea wapi zaidi ya kule kwa Mobutu Sesse Seko kuku wa zabanga?
 
View attachment 1746630
Dodoma. Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amewataka wabunge kuchangia Mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa kuishauri Serikali kama iendelee na mpango wake wa kununua ndege au isitishe hadi itakapoweka mambo sawa.

Ndugai amesema hayo bungeni mjini Dodoma leo Alhamisi Aprili 8, 2021 kabla kuchangia Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo (2021/22 hadi 2025/26) uliosomwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba.

Amesema Shirika la Ndege (ATCL) limepata hasara ya Sh60 bilioni, hivyo wabunge wanatakiwa kuishauri Serikali wakati wakichangia mpango huo kama iendelee na mpango wa kuongeza ununuzi wa ndege au wasitishe kwanza hadi watakapoweka mambo sawa.

Amewataka wabunge hao kushauri pia katika ununuzi wa mabehewa kwa ajili ya uendeshaji wa reli ya kisasa (SGR) kama ni vyema yakanunuliwa na Serikali au ununuzi ukafanywa na wabia wa sekta binafsi.

Amesema zipo nchi zinafanya uwekezaji wa miundombinu ya reli na suala la mabehewa linafanywa na wawekezaji binafsi.

Amewataka wabunge kutumia nafasi hiyo kuishauri Serikali na wasisubiri kukosa wakati inapokosea.
1. Hakuna nchi yoyote ya dunia ya tatu isiyopata hasara kwenye uendeshaji wa biashara ya huduma za ndege
2. Serikali haiendeshi shirika la ndege ila imenunua ndege na kuzikodisha kwenye shirika la ndege la Tanzania (ATCL) ambao ndio wanawajibika kutafuta soko kwa biashara ya huduma hivyo serikali haiwezi kulaumiwa katika hilo ni hao waliokodishwa
3. Ndege za mizigo ndio zinahitajika zaidi ambazo ndizo zinaweza kuziba pengo la ukosefu wa abiria wa kutosha kwa kusafirisha bidhaa kutoka eneo moja kwenda jingine kwa haraka ikiwemo mazao ya kuharibika
4. Spika ni kigeugeu, hana msimamo wakati wa hayati alipongeza sijui ana matatizo gani
5. Hayati ndiye aliyetoa dira ya maendeleo ya taifa kuelekea mwaka 2025, Mh Rais Samia hajatoa hotuba yoyote ya kubadili mwelekeo huo hapo wanajikaanga wenyewe kwenye mafuta yao

Kwa ujumla viongozi wa kisiasa ni wanafiki, wazandiki na kiwanda cha uharifu.

Wapeleke hoja ya mswada wa mabadiliko ya sheria iliyotungwa kumpa kinga Rais, Makamu wa Rais, Waziri mkuu, Spika, Naibu spika na Jaji mkuu kushitakiwa mahakamani ili hawa wanaojifanya kugeuka maamuzi yao ya awali waburuzwe mahakamani sasa hivi hapo ndipo tutajua kwamba kweli wamenuia kudhalilisha pekee hayati au wanajaribu kujisafisha kwa kutumia masizi.
 
Ripoti ya CAG isiwatishe, tuendelee mbele. Kenya airway moja ya mashirika kongwe ya ndege Africa limepata hasara bil.zaidi ya 700 na bado linahudumu, sisi bil. 60 unaogopa kununua ndege. Hata tupate hasara ili mradi linaingia nchi mbali mbalimbali ni namna ya kuitangaza Tanzania duniani.
Naomba source mkuu wa kazi
 
Back
Top Bottom