KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Kuna ID nyingi sana zimeingia humu JF hivi karibuni, zinakuwa ngumu sana kueleweka wanachokieleza. Mada inaanzishwa, halafu inazungushwa weeee, unashindwa kujuwa wapi pa kuanzia na wapi pa kuishia!Wengine sisi tunaona kama watu wanapeana madini wenyewe kwa wenyewe. Wapo Barrick Gold. Wapo WaSriLanka na WaThai ambao wanachukua madini mengi. Halafu wapo wananchi. Nani hasa anafaidika na haya madini yetu ya Watanzania?...
Hivi hii ni staili mpya ya uandishi?
Nikirudi kwenye ID mpya kwenye jukwaa hili la siasa, naona kama kuna ngwe mpya kabisa imeingia kazini hivi karibuni. Hivi kuna utaratibu wa kuachiana majukumu kwa baadhi ya wachangiaji?