Ndugu wa Hamza, mhalifu aliyeua Askari Selander bridge watiwa mbaroni na polisi

Ndugu wa kijana Hamza aliyeuwa polisi watatu na yeye kuuawa pale daraja la Salenda wametiwa mbaroni na polisi usiku huu.

Ndugu wote wamekamatwa na nyumba yao imefungwa na iko chini ya ulinzi.

Chanzo: Ayo tv
Kama ni suala la usalama wao basi polisi walipaswa kutoa ulinzi nyumbani kwao sio kuwaweka ndani.

Polisi wameshindwa kabisa kufuata sheria
 
Mnaowakandia polisi kwa kuwachukua hao ndgu nawashangaa sana. Labda kama nyie ni polisi mngeanzia wapi upelelezi wenu??

Huyo jamaa alikua anaishi hapo kwa maana hiyo hiyo bunduki yake alikua kiishi nayo hapo, lazma starting point iwe mahali anapoishi. Sasa watu wanatokwa povu eti ooh polisi ndo uwezo wao ulipoishia.
Kwanza wao wenyewe wanafamlia usalama wao upo hatarini kuishi na mtu wa namna hiyo, vipi kama wakiuwa na washirika wa jamaa ili wasitoe siri?? Lakini bado mamtu sijui yanataka uyo mwamba aamshwe ndo aseme ukweli.
 
Kama ni kweli huu ni upumbavu wa KUKURUPUKA. Ndugu kuwa mhalifu haina maana ndugu zake wote ni wahalifu labda kama kuna ushahidi wa uhalifu wa ndugu zake. Wakamate na maccm yote basi yaliyokuwa karibu na huyo muuaji. View attachment 1908450
kama nawaona jamaa kwenye hyo picha wanavyotetemeka dah!😟
 
Kuwahoji watu wa karibu na mharifu ndio standard procedures za vyombo vya usalama duniani kote. Huwezi kamata mtu au mtu akafa/akauwawa kisha polisi wakakwepa kuhoji watu na kuwaweka kwenye usalama wao. Kama hatutaki polisi tupendekeze jeshi hili lifutwe tuone tutapata faida gani
 
Bado Akili yangu inakataa ,

Bwana Hamza hakua GAIDI,
Laiti angekua ni gaidi,basi angedili na raia
 
Wanachofanya ni kukosa uweledi tu wa kazi yao.
Wameshindwa kumkamata muhusika mwenyewe akiwa hai wakapoteza ushahidi,sasa wanakwenda kuwasumbua watu wengine wasiohusika.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Siasa zimeharibu akili za waTanzania kwa kiwango kikubwa sana......

Ni kama vile wanasiasa wame install program fulani kwenye vichwa vya waTanzania.......

Uzi huu unadhihirisha hili....siasa zinawaweka mbali waTanzania na weledi........
 
Kama ni kweli huu ni upumbavu wa KUKURUPUKA. Ndugu kuwa mhalifu haina maana ndugu zake wote ni wahalifu labda kama kuna ushahidi wa uhalifu wa ndugu zake. Wakamate na maccm yote basi yaliyokuwa karibu na huyo muuaji. View attachment 1908450

Ni kawaida katika upelelezi kukamata walio karibu na mhalifu kwa ajili ya mahojiano.
 
Ilikuwa ni lazima. Hata marafiki zake nao watatafutwa, hiyo ni njia tu ya upelelezi na kutaka kuujua ukweli.

Haishangazi
Ukweli anao marehemu peke yake, wanakosea sana kushikilia ndugu.
 
Ndugu wa kijana Hamza aliyeuwa polisi watatu na yeye kuuawa pale daraja la Salenda wametiwa mbaroni na polisi usiku huu.

Ndugu wote wamekamatwa na nyumba yao imefungwa na iko chini ya ulinzi.

Chanzo: Ayo tv

ndio mwisho wa kufikili wa jeshi la sirro,
 
Kama ni kweli huu ni upumbavu wa KUKURUPUKA. Ndugu kuwa mhalifu haina maana ndugu zake wote ni wahalifu labda kama kuna ushahidi wa uhalifu wa ndugu zake. Wakamate na maccm yote basi yaliyokuwa karibu na huyo muuaji. View attachment 1908450
BAK maisha yako ya mitandaoni ,unapenda kupinga kila kitu.Hizo ni theory na philosophy za kiintelejensia.
 
Polisi wa Tanzania huo ndio uwezo wao ulipoishia
Polisi hawana data base ya wananchi. Inatakiwa wawe na mahusiano mazuri na wananchi ili linapotikea jambo wanakuwa na first knowledge. Zamani polisi cid walikuwa kila sehemu si kwenye mabaa majumba ya sinema vijiwe vyote na anywhere watu walipokusanyika na walipata taarifa haraka kabla jambo halijatokea. Siku hizi wanasikiliza vyama vya siasa tu wanaacha ulinzi kwa wananchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…