Ndugu wa mke kuja nyumbani kwangu bila mimi kujulishwa imekaa kitaalamu kweli hii kitu?

Ndugu wa mke kuja nyumbani kwangu bila mimi kujulishwa imekaa kitaalamu kweli hii kitu?

Habari zenu watu wa mapenzi.
Iko hivi,kwanza naomba kudiclea interest mimi sio mchoyo wala sina chembe za uchoyo kama ambavyo wengi wenu mngeweza kudhani.
Naishi mkoa tofauti na ambao familia yangu inaishi,so tarehe za mwisho wa mwezi kama hizi huwa natoroka kuja kuwasalimia siku kadhaa then narudi kituo changu cha kazi.
So ktk ujaji wangu home me huwa sitoi taarifa kwa yeyote huwa nawashtukiza tu ghafla ghafla..
Kama mara tano hivi kila nikija home nakuta ndugu za wife tofauti tofauti wapo home hapa,me sikua naona shida sana as me hawanibani kwa lolote,last month nilikuja nikamkuta mdogo wa wife na mwanae wako hapo home na toka nifike mpaka wanaondoka tulikaa nao karibu siku 8 sikutaka kuuliza wamekuja lini.
So jana tena nimekuja kimya kimya home nimemkuta ndugu mwingine wa kike wa wife wamefunga chuo yupo home hapa sijahoji lolote.
So leo nikiwa ndani na laptop yangu namalizia vimeo vyangu vya job mara ghafla nasikia geti linagongwa kaingia wifi wa wife yani mke wa kaka yake na mwanae na ninavyoona hawa sio wa kuondoka leo coz naona mpaka wana kibegi wamebeba.
Sitaki kumuuliza wife hizi mambo za ndugu zake kuja hapa as anajua me sio mtu wa kujali sana mambo hayo ila sasa kama baba wa familia nashangaa kwa nini sihusishwi kwenye ujaji wa hawa wageni as mnavyojua sahivi hali ya maisha imekua ngumu kidogo na watu tunapambania tu familia zetu ziende chooni, sasa huu ugeni mwingine ambao mimi nakua sina taarifa nao naona ka unaenda kinyume na bajeti zangu za mwezi.
Mimi binafsi ndugu zangu huwa wanatoa taarifa siku 3 nyuma kabla hawajaja kwangu hivyo tunajiandaa mapema.
So wakuu hii kitu imekaa kitaalamu kweli na nitumie mbinu gani kufikisha ujumbe kwa wife bila kumkwaza?
Ninachojua, baba mwenye nyumba sio tu anapewa taarifa anaombwa ruhusa.

Kama hakuna ulazima wa kuja kipindi fulani unaweza wapangia wakati mwingine.
 
Wewe mwenyewe ukienda kwako hutoi taarifa umesema na unaona ni kawaida tu, usilaumu kaka, ni mtindo wa maisha uiiouanzisha mwenyewe tulia uuishi!

Kutoa taarifa kwenda kwako hakukuondolei ubaba wako wala haukushushii cheo chako home, ni ustaarabu tu.

Usilalamike kwa mkeo kutokukushirikisha mambo. Anajifunza kwako
Faza house taharifa ya nini?utamfumaniaje mkeo?
 
Wewe na mkeo huwa hamzungumzi..?? Maana katika maongezi yenu ya kawaida ya kila siku ndipo humo hizo taarifa zingekuwa zinakufikia..!!

Hamuwezi kuwa mnaongea kila siku kisha kuna wageni kwako na mkeo asiseme chochote kabisa, it doesn't sit well with me kiukweli..!!

Na mambo mengine anakushirikisha kama kawaida mkuu..? Ama mnaishi tu kama watu mnaoshea nyumba na siyo familia ya mke na mume..? MAWASILIANO yenu yapoje mkuu..?
Kabisa
 
Ukioa mwanamke wa kabila la Tlaatlaah watakuja mabinamu wengi wa kiume kumsalimia. Hao mabinamu karibu wote ni michepuko wa mke. Watamgongea hapohapo kwako. Wanawake wa hilo kabila warembo sana ila hiyo tabia inawaharibia.
 
Back
Top Bottom