Jibu ni Rahisi tu,
Imeandikwa, mwenye HAKI wangu ataishia Kwa Imani. Na application yake ni kwenye Kila kitu.
Kuna kijana nilimwamini nikampa Bodaboda Kwa mkataba wa miezi 8, akalipa vizuri miezi miwili Kisha akaiweka bond pikipiki yangu na kuacha kuleta marejesho.
Uwezo wa kudeal naye kisheria nilikuwa nao, pia hata kutumia watu ningeweza kumdaka na kumfunga alipe Hadi sent ya mwisho Kwa kuwa mikataba na vithibitisho vyote ilikuwa navyo,
Wengi walinifuata Ili nimkamate kupata HAKI yangu, lakini Kila nilipotaka kuchukua hatua nilikakatazwa na Mungu wangu, akaniambia mwache, HUTAPUNGUKIWA na chochote unachohitaji.
Kinachotokea sasa, ninatumia ninachotaka na sijawahi kuwa mhitaji financially.
Jifunze kuwa, waliookoka kamwe hawaendi mahakamani kudai HAKI, labda upate maelekezo kufanya hivyo Kwa sababu maalum.
Ubarikiwe 🙏