Ndugu yangu amegoma kunirudishia pesa zangu

Ndugu yangu amegoma kunirudishia pesa zangu

Kipi chaUmpekeleke ndugu yako mahakamani sababu ya hela?

We ni mchaga sorry?

Umesaidia wangapi aisee ije kuwa ndugu yako kabisa tena unasema wadamu!

Potezea tu
Weee naye kipi Cha ajabu hapo? Sasa watu wanauana na ni mtu na ndugu yake sembuse mahakaman? Mahakaman sio jehanami ni sehem ya kupata haki Yako?
 
Ndugu wengi ni wapumbavu sana! Mimi miaka 15 hajanilipa Hela yangu na ni shemeji yangu amemuoa dada yangu! Alikuja anaomba utamhurumia sana na ni mtumishi wa uma! Qmmmmk!
Aiseee huyu mtu mjinga kwel ,yaan anamlq dadako miaka yote iyo alaf anakuja kukopa na anakurusha?
 
Zama za leo watu wengi wenye uhusiano wa karibu wamekuwa matapeli. Utapeli (wizi wa kuaminiana) unaongezeka kwa kasi sana miongoni mwa jamaa wa karibu.
Kama inawezekana msamehe tu then yootezee hilo deni. Msije mkaanza kurogana bure
Kwa ujumla watanzania wengi sio waaminifu. Ukimkopesha hela tu anaanza kuwa adui yako pindi ukianza kumdai.
 
Aiseee huyu mtu mjinga kwel ,yaan anamlq dadako miaka yote iyo alaf anakuja kukopa na anakurusha?
Kama mimi shemeji yangu nilimpa hela yangu toka 2010 lakini mpaka leo namdai kalipa nusu tu. Na thamani ya hela yenyewe imeshuka kwelikweli, hata akilipa sasa hivi haiwezi fidia thamani. Nimempotezea tu.
 
Mwaka jana ndugu yangu kabsa wa damu alikuja na kuomba nimpatie pesa ili a bust biashara zake, kwa vile alijuwa kuwa kuna kititi nimepokea kutoka Taasis fln ya umma.

Sikuweza kumnyima kwa vile mm pia nilikuwa nafikiriaa cha kufanyia hizo pesa either ninunue kiwanja dodoma am au nianzishe ujenzi.

Kwa hyo kwa kifupi sikuwa na haraka sna na hizo pesa, Sasa ni mwaka una karibia kukatiwa hadi Leo hajapata na amekata mawasiliano na mimi kabisa nimeenda home nikamshaki kwa wazazi, wazazi wakasema watampigia aje aseme lini atanipatia hzo pesa kwa vile hata mimi nimekwama, akitoa ahadi kuwa mwezi wa Tisa atanilipa ila hadi sasa hajafanya lolote!

Na fikiria kupeleka mahakamani ili nikapate haki yangu ambayo anataka kunidhulumu

Ndugu yangu ana kazi yake nzuri tu ana maisha mazuri tu ila nashangaa hati kunipa pesa zangu. Nampeleka mahakamani jumatatu

Naombeni ushauri wenu
Ndugu hakopeshwi ndugu yangu, Kwa sababu huwezi pata nguvu ya kudai kwa nguvu
 
Nenda kalijenge Kwa usimamizi wako..kwanza ulifanya makosa kutuma Pesa Kujenga kabri la mzazi bila uwepo wako.

Funga safari, kalijenge, alafu endelea kumjali bibi yako.

Pesa amekula Mama Mdogo wako, ila kwakua ni mtoto wa Bibi yako, bibi yako akaona apoozee tu.
Daktari Carlos The Jackal nimekuelewa Kaka ila Sasa naendaje kulijenga na hela wamekula wao ?

Mimi nawaza sijui nifanyeje warudishe hata kwa vikao vya kuwachamba tu .

Maana nilizungumza na mama mkubwa akasema labda waitwe kwenye kikao wawekwe kitako wachambwe mpaka waseme hela itarudije ijapokuwa Mimi naona bado sio njia ngumu ya wao kurudisha hela ,Mimi nataka njia ngumu mno wajute na wasirudie kwa mwingine
 
Kuna kitu inatakiwa kijulikane ndugu hakopeshwi anasaidiwa tu. Yaani ndugu yako akija na gia ya nikopeshe ww katika hitaji lake angalia kias unachoweza kumsaidia mfano anahitaji laki tano ww unauwezo wa laki moja mwambie sina laki tano ila ntakukopesha laki moja huku moyoni ukijua kabsa umemsaidia
Nimewahi kukopesha ndugu zaidi ya watatu hakuna hata moja amewahi kunirudishia hata mia ila kwakuwa ilikuwa ni pesa ninayoimudu sikuumia wala kuwaza.
Ndugu lawama.

Kumbuka AOCH WAT ILOREGA MOS MOS.
 
2021 nilipata mkopo ndg yangu mfanyabiashara akaniomba hela m10 nikampa m8 akini hakikishia ndani ya miezi 4atakuwa kshamaliza kurudisha hela yote.
mwezi wa kwanza,pili na watatu ukakata bila chotechote kunipa
mwezi wa4 akaniwekea laki5 uliofata 150k uliofaata 200k ndo ikawa mwisho.

nikaenda kwa wazee wakaniambia msamehe vingine mtakosana hadi na watoto wenu akiamua kukupa na akupe
iwapo hata kupa achana nae.

namimi nikaachana nae japo yeye huwa namuona hana amani kabisa na issue kubwa ipo kwa wife hajawahi sahau

NAKUOMBA SAMEHE MKUU.mtakujha uana nakwambia
Nimepiga kelele mpka watu ofisini wamenigeukia .

Bro m .8 hakika nakuambia na undugu ungeisha ,hapa wamekula laki sita ya kaburi nawaza kulipa kisasi na undugu nifutilie mbali Sasa milioni nane nahisi ningeenda kubomoa na nyumba yake
 
Mwaka jana ndugu yangu kabsa wa damu alikuja na kuomba nimpatie pesa ili a bust biashara zake, kwa vile alijuwa kuwa kuna kititi nimepokea kutoka Taasis fln ya umma.

Sikuweza kumnyima kwa vile mm pia nilikuwa nafikiriaa cha kufanyia hizo pesa either ninunue kiwanja dodoma am au nianzishe ujenzi.

Kwa hyo kwa kifupi sikuwa na haraka sna na hizo pesa, Sasa ni mwaka una karibia kukatiwa hadi Leo hajapata na amekata mawasiliano na mimi kabisa nimeenda home nikamshaki kwa wazazi, wazazi wakasema watampigia aje aseme lini atanipatia hzo pesa kwa vile hata mimi nimekwama, akitoa ahadi kuwa mwezi wa Tisa atanilipa ila hadi sasa hajafanya lolote!

Na fikiria kupeleka mahakamani ili nikapate haki yangu ambayo anataka kunidhulumu

Ndugu yangu ana kazi yake nzuri tu ana maisha mazuri tu ila nashangaa hati kunipa pesa zangu. Nampeleka mahakamani jumatatu

Naombeni ushauri wenu
Ushauri gani unataka,wakati unampa pesa uliomba ushauri?
 
Hata waki what?
Niliandika nikiwa na maumivu mtanziko moyoni na akilini baada ya mleta mada kupandisha mada yenye mlengo wa kuziumiza hisia zangu Kama yeye hivyo nikajikuta katika typing errors

Alright ?

Toa ushauri Sasa niwafenyeje Hawa viumbe ila kuhusu undugu nishaanza kuupunguza kwa kutowapigia wakipata shida japo ninachohitaji zaidi ni hela yangu ,maana najua hata marehemu anaumia kuliko kawaida .
 
Kuna kitu inatakiwa kijulikane ndugu hakopeshwi anasaidiwa tu. Yaani ndugu yako akija na gia ya nikopeshe ww katika hitaji lake angalia kias unachoweza kumsaidia mfano anahitaji laki tano ww unauwezo wa laki moja mwambie sina laki tano ila ntakukopesha laki moja huku moyoni ukijua kabsa umemsaidia
Nimewahi kukopesha ndugu zaidi ya watatu hakuna hata moja amewahi kunirudishia hata mia ila kwakuwa ilikuwa ni pesa ninayoimudu sikuumia wala kuwaza.
Ndugu lawama.

Kumbuka AOCH WAT ILOREGA MOS MOS.
Ni kweli. Sio kwa ndugu tu, hata watu wengine. Ukija kukopa laki, nakupa 20k, nyingine kaombe kwa wengine . Nina rafiki watatu ndio tunakopeshana kwa uaminifu mkubwa.
 
Usiende kinyume na mtu uliekula nae chungu kimoja.

Usimfanyie ubaya au kulipiza kwa ubaya mtu uliechangia dae damu.

Soma biblia utaelewa haya ninayokuambia.
 
Ni kweli. Sio kwa ndugu tu, hata watu wengine. Ukija kukopa laki, nakupa 20k, nyingine kaombe kwa wengine . Nina rafiki watatu ndio tunakopeshana kwa uaminifu mkubwa.
Safi kabisa mkuu maana yake hata akikudhulumu hauwezi kuumia kwa kuwa ipo ndani ya uwezo wako
 
Safi kabisa mkuu maana yake hata akikudhulumu hauwezi kuumia kwa kuwa ipo ndani ya uwezo wako
Nimekopesha watu kadhaa lakini wameishia ku block namba yangu. Sitaki stress na hela zangu. Tunajifunza kupitia watu.
 
Nimekopesha watu kadhaa lakini wameishia ku block namba yangu. Sitaki stress na hela zangu. Tunajifunza kupitia watu.
Kaka wanasema tenda wema nenda zako mwaka fulani nikiwa chuo nilinona kuna mwanachuo mwenzetu ni kanda moja alinyimwa kufanya mtihani wa mwisho kwasababu ya michango moyo wa hofu ya mungu ikaniingia nikampa laki tano japo kusema ukweli kipindi kile nilimpa tu sikuwaza madhara yake.
Tukamaliza chuo yeye mwaka moja tu kapata ajira huwezi amini mpka sasa mimi nipo mtaani yeye yupo kwenye mfumo mwaka wa 12 huu hajawahi nirudishia hata mia. Wanasema tenda wema nenda zako
 
Watanzania ni watu wa ajabu sana. Mtu anakuja kwako akiwa na shida, zikiisha hakuthamini tena.
 
Back
Top Bottom