Ndugu yangu amegoma kunirudishia pesa zangu

Ndugu yangu amegoma kunirudishia pesa zangu

Mpeleke mahakamani alafu usirudie tena kuja kuomba ushauri wakati tayari una maamuzi yako na hutaki ushauri
 
Nenda kazini kwake kaongee na bosi wake watamkomesha utalipwa tu
 
sikushauri kusamehe ila kumpeleka ndugu maahakamani dah kama mkosi ivi. Ila M5 nyingi Kwa maisha yetu haya. Dah nimesikitika kama hizo hela ni zangu vile.
 
Broo mm sin uwezo wa kumzamehe mtu milion 5 sina kwa kweli sina hata Uwezo wa kusamhe laki mbili sembuse hyo hapna jtatu kesi itanza
Huyo ndugu yako inaonekana ni mbinafsi sana. Hukulijua hilo? Binafsi simkopeshi ndugu kamwe
 
Siku zote ukitaka undugu ufe basi endekeza michezo ya kukopeshana.

Pole sana Mkuu bila shaka ikitokea umepata haki yako basi hutarudia kukopesha tena ndugu.
 
Milion tano nisamehe
Kumbuka vizuri labda na yeye alisha wai ingia gharama kwa ajili yako, sema wwe ukaona kama ni msaada tu,mwenzio nae unaona kama na wwe unastahili kumsaidia pia!!
 
Kaa chini mtengenezee sinema mkuu. Mtokee kwa nyuma huyo. Tafuta watoto wa mjin
Nyie ndiyo mnateka watu alafu lawama mnazipeleka kwa Jeshi la Polisi, ushauri gani huu unampa mwenzio!!??
 
Mwaka jana ndugu yangu kabsa wa damu alikuja na kuomba nimpatie pesa ili a bust biashara zake, kwa vile alijuwa kuwa kuna kititi nimepokea kutoka Taasis fln ya umma.

Sikuweza kumnyima kwa vile mm pia nilikuwa nafikiriaa cha kufanyia hizo pesa either ninunue kiwanja dodoma am au nianzishe ujenzi.

Kwa hyo kwa kifupi sikuwa na haraka sna na hizo pesa, Sasa ni mwaka una karibia kukatiwa hadi Leo hajapata na amekata mawasiliano na mimi kabisa nimeenda home nikamshaki kwa wazazi, wazazi wakasema watampigia aje aseme lini atanipatia hzo pesa kwa vile hata mimi nimekwama, akitoa ahadi kuwa mwezi wa Tisa atanilipa ila hadi sasa hajafanya lolote!

Na fikiria kupeleka mahakamani ili nikapate haki yangu ambayo anataka kunidhulumu

Ndugu yangu ana kazi yake nzuri tu ana maisha mazuri tu ila nashangaa hati kunipa pesa zangu. Nampeleka mahakamani jumatatu

Naombeni ushauri wenu
Ndugu yangu ninaemfuata alinitapeli mil 2 kwa mtindo huu huu, bahati mbaya sana hata wazazi hakuwaheshimu hivyo hakukuwa hata na mtu wa kumkoromea arudishe..nilisamehe na kuendelea na maisha, na kiuchumi alikuwa ameshapigika hata ukimpeleka popote hakuwa na hiyo hela.
 
Usipende kuunganisha Kila Kitu na IMANI.

Ili Karama imrudie Nawewe ubarikiwe, ni lazima uhakikishe WEWE NI MSAFI HAUNA DHAMBI YA AINA YOYOTE.


Samehe alafu uendelee na uzinzi, uongo, n.k uone kama utabarkiwa.

Unadhan kwann Tajiri wa kuzulumu anabakia kua Tajiri mpaka kufa, Nawewe ulodhukumiwa unabaki kua Masikini mpaka kufa??

Wakati mwingine tuamini kama Akili na matumizi ya Akili.


Mahakama ilianzishwa na Mungu mwenyewe.
Mkuu hili jambo na mimi huo tunashindwana na rafiki yangu mmoja mfia imani, kila jambo hata lenye kuhitaji maarifa yeye anasukumia imani iamue...kwa kweli mara kadhaa inanilazimu kumkwepa maana naona atanifubaza ufikiri.
 
Nyie ndiyo mnateka watu alafu lawama mnazipeleka kwa Jeshi la Polisi, ushauri gani huu unampa mwenzio!!??
Kumtokea mtu nyuma sio kumteka mzee. Unamtengenezea watu wanamletea biashara halali halafu akijichanganya siku anayolipa hela unamtokea na mabaunsa unachukua hela yako sasa hapo mpira unageuka. Unamuachia yeye kaz ya kwenda mahakamani si ni ndugu? Mtakutana mahakamani. Mzee hela hazipatikan kilokole.
 
Mzingue kwa kuwatuma watu tofauti tofauti bila kusahau kupiga simu kila siku alfajiri....
Kumbuka kudai nacho ni kipaji Mkuu
 
Binafsi sikopeshi kabisaaa,ni hati hati ya kuua undugu au urafiki.Waaminifu wamebaki wachache sana(1%), otherwise ujifanye mjinga tu maisha yaende ili muendeleze udugu/urafiki.
Yashanikuta sanaaa,nishapoteza hela nyingi sanaaa kwa kumkopa/kum-boost mtu and last hatukua na mwisho mzuri kwa wote.
 
Ushauri mzuri Kaka ila na Mimi nishauri nilituma nyumbani hela ya kaburi la mzazi lijengwe upya ,kichekesho wameikula ni mama mdogo na Bibi yangu wananipa ahadi watalijenga tu .

Sasa nimepanga nizile nisiwatafute hata wakifa nisiwapigie nishauri ndugu Hawa watu ni ndugu zangu niwafenyeje Sasa ?
Sasa watu wananjaa nawewe hujawai kuwatumia pesa yakujikim hata siku moja ila pesa yakujengea kaburi umetuma hata mim ningekula asee
 
Ndugu wengi ni wapumbavu sana! Mimi miaka 15 hajanilipa Hela yangu na ni shemeji yangu amemuoa dada yangu! Alikuja anaomba utamhurumia sana na ni mtumishi wa uma! Qmmmmk!
Daaa dada anakugongea napesa pia kakudhulumu
 
Back
Top Bottom