Ndugu yangu amekuwa mlevi wa kupindukia, nataka nimpeleke sober house

Ndo maana nataka nimpeleke sober house angalau apumzike, hali yake inazidi kuwa mbaya
 
Nashauri fuata ushauri wa Dream Queen, mtafutie kwanza therapist aongee nae. Ajue shida nini. Hafu ndio stage ifuate ya sober house.

Ila pia nashauri kama upo nae karibu, anza kumshirikisha vikazi vidogo vidogo, au mpe majukumu kadhaa ya kusimamia awe busy kidogo na unakua unamcheki kila muda flani ili awe busy. Sina uhakika ila nahisi inaweza sahidia kidogo.
 
Sawa mkuu
 
Haya mambo yasikie tu kwa watu, usiombe yakukute. Tuliambiwa akiacha atakua mkombozi, sahivi anapiga pambio tu. Mungu ni mwema ameokoka kupitia hizi za 'bakabaka' mwaka mzima yupo anapiga gwaride tu.

Pole sana mkuu King Jody kaeni nae karibu msimuache. Muujiza upo, cha msingi endeleni kuwa nae karibu na hizo tiba wanazoshauri wanajukwaa usiache kujaribu mana mambo ni mengi mnoo ulimwengu huu....
 
Nimewahi kukaa naye mara nyingi namuuliza anasema hata yeye hapendi kunywa lakini hawezi kuacha kunywa
Tafuta nguruwe ananyonyesha, kamua maziwa walau vijiko 2 vya chai!!! Mnunulie tungi alipendaro, anyweeeee mpaka alegee then mchanganyie yale maziwa kwenye kinywaji komojawapo akikisha anakunywa mpaka inaisha!! Baada ya hapo atatapika mpaka mashetani yooote na haji kugusa pombe tena milele na milele!!


NB: hili swala inabidi iwe siri yako na usije kumwambia mtu, kamwe usimwambie mtu
 
Sawa mkuu, inaumiza mno lakini ntampambania naamini Mungu atamsaidia
 
Ndo maana nataka nimpeleke sober house angalau apumzike, hali yake inazidi kuwa mbaya


Mpeleke sober house. Huko wapo therapists pia wanajua namna ya kumsaidia.

Lakini husiende kumtupa huko, hakikisha anapata mahitaji yake yote ya msingi Kama ambavyo anatakiwa.


Miezi 9 ndio standard reset time for alcoholics, vigezo na masharti vikizingatiwa.
 
Sawa mkuu ntafanya hivyo
 
Ntamhudumia kwa mahitaji yote kwa sababu hali yake inaniumiza sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…