Ndugu yangu amekuwa mlevi wa kupindukia, nataka nimpeleke sober house

Kuna jambo kama limejificha.
Anyway
Kama upo Dar nenda salasala kituo cha mbuyuni....Kuna ofisi ya wa missionaries wanaitwa Changamoto ni matumaini
 
Ninawajua watu wawili waliopelekwa sobb.
Wa kwanza alivyorudi alikuwa amenawiri lakini akaanza mdogo siku hizi anakunywa hadi gongo ya sogodo huko.

Wa pili tulikuwa tunakunywa wote mwaka 2015 bia, chibuku na komoni mara moja moja. Ila baadaye mimi nilihama yale mazingira. Nikasikiaga kwamba kiwango kimepanda, anakunywa sana pombe zote. Familia ikaamua kumpeleka soba na akarudi na bado anakunywa.
Mwaka huu tumeenda kuonana, nikapelekwa hadi kwenye vijiwe vyake vyote hadi tukampata kwenye ubanda mmoja maana amekuwa mnywaji kiasi hadi simu hatumii ndio maana tulimtafuta kianalojia.

Kwanza nilipofika nikamkuta yupo tungi kiasi halafu kanisahau. Jamaa yangu alivyomkumbusha vizuri ndio akanikumbuka.
Yeye kwa kinywa chake alisema ni kweli alipelekwa soba na alirudi akiwa kanenepa na alikuwa hanywi. Upweke ukamrudisha kwenye pombe hasa nyeupe au gongo. Alipoonja alijilaumu kwamba alikuwa wapi siku zote! Maana alijisikia raha iliyoje.
Mpaka muda huu ninavyoandika jamaa anakunya gongo anapumzika wakati wa kulala tu.
 
Duuu
 
You are very right....hapo ni Mungu tu.
Kimsingi wanaopona ni 2% .
Kweli wananenepa lakini shida haipo kwenye mwili.
 
walimpiga wenzie alikua ana kaukorofi na kaubishi ka maudhi, alitandikwa vibaya sana karibu afe ila yeye alisema eti amepata ajali.

actually wale jamaa wa pale sober walikua wakitupatia taarifa zake ila yeye anageuza anatia uongo
kaubishi ka maudhi[emoji1787][emoji1787]
 
kaubishi ka maudhi[emoji1787][emoji1787]
kichwa yake ikipoa pombe kidogo, huwa anahadithia ukweli mambo yalivyo mule ndani, utaskia anasema namnukuu

"uncle acha thu, jamaa wa mulye ndani hawanya hurthuma wanaweztha kukuua kabithaa ukiletha ubisthi, wanapiga matheke hayo ni balaa"

mwisho wa kunukuu.

anayasema hayo huku akiwa amezishika na kuzipapasapapasa taya zake zilizopishana"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…