Ndugu zangu upande wa baba wanainua vita kali juu yangu

Chakorii Pole mpenzi, ila pia hongera sana!

Ni wazi wamehamia kwako kwasababu wameona wewe ndio mwenye maono, msukumo na uwezo wakuimarisha familia yenu. Simama kwenye imani na malengo yako. Maadam Mungu amekuongoza mpaka hapo ulipofikia, hatokuacha, hivyo hao jamaa zako hawatofanikiwa na nia zao mbaya.

Ila pia jaribu kukaa nao mbali na usiendekeze taarifa wala umbea unaohusiana na wao ili wasikuondoe kwenye mstari. Mtu yeyote akikuletea habari zao waambie hutaki kujua. Focus kwenye malengo yako, familia yako na wewe mwenyewe.
 
Funguka vizuri tukusaidie.

Umeifumba fumba sana stori yako
 
Pole mami ongeza bidii kweny kusali na soma zaburi.
 
pole sana mkuu funga vioo familia ni hio ulio nayo sasa baba,mama na wadogo zako basi, hao ndugu wa baba usiwatukane usiinue mdomo kujibizana nao kitu wapuuze jifunze kufunga hata siku 3 jiimarishe kwa kudoa sadaka na zaka kama kinga ya mali zako kwa Mwenyenzi Mungu.
 
Wasamehe halafu wafungie vioo!
Hii njia imefanya kazi kwangu.
Njia yangu pendwa pia, yaani nimefunga vioo na tinted nimeweka..

Kifupi ndugu zako ni wachawi, wao ndio waliossbabisha wazazi watengane...

Hata maisha magumu mliyoishi ni wao waliosababisha...

Wewe wanakutafuta wakuyumbishe...

Hiyo inaitwa vita baada ya kupata...

Omba MUNGU sana, wasamehe na wafungie vioo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…