Awamu ya tano,kaskazini walilalamika kwa kuwa mtawala aliyekuwepo alifanya kila hali kupunguza tabia ya upendeleo waliyokuwa nayo kwenye fursa serikali. Wakalalamika na kuhisi walilokuwa wanafanya ni sahihi. Wakamshambulia kwa kejeli na kabila lake na kunung'unika. Mtawala nae akafanya kosa hilo hilo kwa kuweka upendeleo kwa watu wa kanda ya ziwa kwenye fursa na nafasi za uongozi serikali. Nao wakafurahia na kuhisi ni sahihi na haki yao. Wakabeza na kutukana wengine kwa dini na makabila yao.
Nashukuru awamu ya sita imeamua kuruhusu haki itawale na fursa kwa kila Mtanzania bila kujali dini,kabila au kanda yake. Endelea kufanya marekebisho Mama Samia, mwisho wa siku kila mtu atakuelewa.