FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Hakuna walioelimika zaidi ya Waislam Tanzania hii.Ona aibu kidogo.
Usijitape umeelimika ikiwa jamii yako ina suffer deficity ya elimu.
Ukiielewa hoja yangu sema AMEN kubwa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakuna walioelimika zaidi ya Waislam Tanzania hii.Ona aibu kidogo.
Usijitape umeelimika ikiwa jamii yako ina suffer deficity ya elimu.
Ukiielewa hoja yangu sema AMEN kubwa
Siamini kama hili andiko murua kaandika muislam.
Nimejaribu kufukua post zako za nyuma, jamaa hujihusishi na mijadala ya dini kabisa hivyo nimeshindwa kutambua dini yako.
kama kweli wewe ni muislam, basi ndio wa kwanza kukuona unayejitambua.
Tuache unafiki wenzetu upande wa Phd na Dr wametuacha hatua kidogo ukitaka kuliamini hili angalia mikutano ya rais akikaa na viongozi wa dini namna ya uchangiaji mada. Nakazia kama mtoa mada sijasema waislam hatujasomaHili suala la Bandari naona baadhi yenu mmelibeba katika namna fulani ya UDINI, kila nikimuangalia kiongozi wangu wa KIISLAM akisimama mahali analizungumzia katika upande wa UDINI.
Sikilizeni, TEC imejaa watu wenye ELIMU kuanzia ya Elimu Dunia hadi elimu ya DINI (THEOLOJIA), ndo maana utasikia Askofu Dr, Eng, Prof fulani fulani wa Parokia fulani. Sisi ukishamqliza kusoma Quran umemaliza, mengineyo ni majungu. Yaani mtu kama Prof Lipumba alitakiwa awe Imamu wa Msikiti fulani mahali fulani na kiongozi fulani katika nafasi za Bakwata taifa, lakini matokeo yake kule tumewaweka wengine. Sisemi kwamba waislam hatujasoma, hapana, PhD zilizopo katika nafasi za uongozi misikitini ni chache mno kulinganisha na wenzetu.
Ndo maana linapofikia jambo la kuongea na kiongozi mkuu wa nchi, hawa TEC, KKKT na mengineyo utaona utofauti, sisi runaomba kupunguziwa ama kuondolewa kodi za TENDE na kuomba tupatiwe VIFAA vya kisasa vya KUUTAZAMA MWEZI mtukufu. Wenzetu wanaomba mismaha ya kodi ya makontena ya vifaa tiba, vifaa vya elimu na mengineyo. Sisi tukishakunywa juisi za tende Ikulu tunashukuru na kuondoka na kushika shikashika videvu kama SUNNAH, tunaondoka.
Leo tunawaona TEC wabaya katika msimamo, mali zetu wenyewe tunashindwa kuzisimamia wenyewe, hapa Kinondoni nadhani kidogo tupigwe na wachache kwenye eneo letu ambalo Bakwata ipo. Tumshukuru Hayati Magufuli (Mkristo) alitusaidia na kutuombea msaada wa kujengewa Msikiti.
Kuna namna nawatazama viongozi kama wanafki, na mnafki siku zote maendeleo kwake yanakawia. Najua huu ujumbe mchungu na mnaweza hata kuitisha kikao mkanisomea ALBADIRI. Ndio, TEC wametoa WARAKA wenye HOJA, mbona hamzikosoi HOJA zao mnajikita katika UDINI? Kwani huu mkataba unaopingwa nyinyi hamkwenda IKULU pamoja nao kabla ya huu waraka? Mlienda kufanya nini? Si mlipeleka mapendekezo ya marekebisho?
Mbona leo mnasita kusema kwamba mlikuwa pamoja? UNAFKI mtupu! Ndo maana katika viongozi wa kidini namkubali Sheikh Nurdin Kishki, Mziwanda, Mazinge na Dr Sulle. Hawa hawana manenomaneno, kazi yao ni kutoa DAGH'AWA tu. Huu unafki nafki umebaki kwa wasiotambua wajibu wao. Kuna shule nyingi za kiislam, matokeo yake ni mabovu. Hatuangalii kuboresha shule zetu, tumekazana kuvaa kanzu na misuli kuzodoana. Tuache Unaa. Astaghafirulah!
Mmenikwaza sana. Kuna huo Sheikh mmoja amesema yeye atasambaza waraka wa kuunga mkono nchi nzima kama tamko la msikiti, huyu hasababishi UDINI, hachochei Udini? Nani katika Uislamu amemuonya aache huo ujinga?
Mnahitaji semina! Mnahitaji kujitokeza na tamko lenye mashiko la aidha kwa nini mnaunga mkono ama mnapinga huu mkataba na muwe na sababu za kujitosheleza. Msijitokeze kwa sababu TEC wametoa WARAKA, mnatengeneza mashindano na mtachochea vurugu zisizo na msingi wowote.
Tuache UDINI, huu mkataba haupingwi kwa sababu ulisainiwa Msikitini au mbele ya imamu na wala huu mkataba hauhusiani na msikiti kwa maana DP World hawaji kujenga misikiti wala kueneza Quran. Wanakuja kuwekeza katika bandari zetu. Tukipinga tupinge kwa hoja na tukikubali tukubali kwa hoja. Tunahitaji kueleweshana, inawezekana mimi sijaelewa na pengine akijitokeza mtu akanielewesha nitamuelewa na nitaunga mkono lakini ukitumia UDINI sintokuelewa. Maana naona kila anaesimama anasema "NYUMA YA PAZIA"; hiyo nyuma ya pazia kwenye ule waraka hiyo "NYUMA YA PAZIA " iko wapi?
Asalaam alaykum!
BAKWATA ni sawa ila sio waislamu.Tuache unafiki wenzetu upande wa Phd na Dr wametuacha hatua kidogo ukitaka kuliamini hili angalia mikutano ya rais akikaa na viongozi wa dini namna ya uchangiaji mada. Nakazia kama mtoa mada sijasema waislam hatujasoma
Inauma lakini mustahamili tu mutazoea Bandari ndio hiyo imeenda poleni sanaWavaa kobaz Elimu hakuna ni udini tu.
Kwa Elimu ipi ajuza, nyie ambao mnakataza wanawake wasisome shule na hapo wanahitaji madaktari wa kike wazalishe wake zao.Hakuna walioelimika zaidi ya Waislam Tanzania hii.
Alaa kwa hiyo kumbe huyo Raisi wa wako wa JMT ni mwanaume sio?Kwa Elimu ipi ajuza, nyie ambao mnakataza wanawake wasisome shule na hapo wanahitaji madaktari wa kike wazalishe wake zao.
Wapi wamekataza ?😅😅 hizi ni porojo mkikaa mkoambiwa mfuatilia mambo ndo hivyo .Kwa Elimu ipi ajuza, nyie ambao mnakataza wanawake wasisome shule na hapo wanahitaji madaktari wa kike wazalishe wake zao.
Ni aina mbili ya watu aidha umuogope Mungu kwa dhati au wanafiki wanaojifocha kwa kujionyesha wana hofu ila ni majiziUmeongea ukweli! hizi taasisi nyingi waumini hawatetei dini kazi kupambania vyeo na kufanya uwizi hamna cha maana ..
Watu wenye akili wengi wamejitoa hawahusiki na taasisi ila wanasaidia watu maskini sio kufanya uwizi na uroho wa madaraka.
Anasema mtume👇Kwa Elimu ipi ajuza, nyie ambao mnakataza wanawake wasisome shule na hapo wanahitaji madaktari wa kike wazalishe wake zao.
Itakuwa hujanielewa kilichosemwa mkuu , ongeza kufikiria walioalikwa viongozi wa dini kwa waislamu huwa wanaenda akina nani? This is publicBAKWATA ni sawa ila sio waislamu.
Kwamba hamna waislamu wenye PhD ? Pia angalia walioko kweny system na wale ambao hawajulikani kabisa..Itakuwa hujanielewa kilichosemwa mkuu , ongeza kufikiria walioalikwa viongozi wa dini kwa waislamu huwa wanaenda akina nani? This is public
Tuache utani, jamaa alivokaa inavutia
Hili suala ni zaid ya ulijuavyo p1 na kasoro zilizopo lkn haya majamaa kamwe hayatokua radhiHili suala la Bandari naona baadhi yenu mmelibeba katika namna fulani ya UDINI, kila nikimuangalia kiongozi wangu wa KIISLAM akisimama mahali analizungumzia katika upande wa UDINI...