Ndugu zangu Waislam mtaniwia radhi kidogo

Ndugu zangu Waislam mtaniwia radhi kidogo

Status
Not open for further replies.
Waislam wasikubali kupelekeshwa puta na abrakadabra za imani ya dini yao, akili zao ziwe huru kama za wakristo. Wajifunze kwa wakristo huwezi kuwapelekesha hovyohovyo utakavyo. Mfano ni wakatoliki na walutheri wametia fora na kuua soo la udini.

Misimamo yao juu ya mkataba tata wa bandari imewaacha njia panda wengine. Kwa ujumla kila mkristo ana msimamo wake juu ya mkataba huo bila kuburuzwa na kiongozi wake wa dini hata kama atasoma na kusomewa waraka au msimamo.

Waislam na wao wawe hivyo wengine waunge mkono na wengine wapinge kwa hoja. Udini tupa kule hii ni nchi ya watanzani kwa umoja wao
 
Ndo maana linapofikia jambo la kuongea na kiongozi mkuu wa nchi, hawa TEC, KKKT na mengineyo utaona utofauti, sisi runaomba kupunguziwa ama kuondolewa kodi za TENDE na kuomba tupatiwe VIFAA vya kisasa vya KUUTAZAMA MWEZI mtukufu. Wenzetu wanaomba mismaha ya kodi ya makontena ya vifaa tiba, vifaa vya elimu na mengineyo. Sisi tukishakunywa juisi za tende Ikulu tunashukuru na kuondoka na kushika shikashika videvu kama SUNNAH, tunaondoka.
We jamaa mchochezi.😆😆
 
Nikamsikia Jamaa mmoja anasema wanamionea huyu mama kwa Sababu ni muislamu. Nikasema kwakweli bado safari ni ndefu
Ni safari ndefu sana. Wengine wanasema eti kwa kuwa ni mzanzibar Tanzania bado tuna tabia za kinyani.

Yaani wapinga Bandari wametoa hoja wakifanye reference kipengele cha mkataba moja hadi kingine anatoka nyau from nowhere anakwambia aah mnapinga kwa sababu ni mwislam.

Inaonesha ndio maana hata watawala wakipata madaraka wanaishia kujipigia pesa tu mali maana majitu yenyewe ya kusema utapiganie ndio dizaini hii.
 
Ndugu zangu waislam mtaniuwia radhi kidogo kuna wanaotumia dini yenu kujifichia maovu kuweni makini na Mamluki waislamu maslahi.

Anaandika Muumini wa Islamic.

Hili suala la Bandari naona baadhi yenu mmelibeba katika namna fulani ya UDINI, kila nikimuangalia kiongozi wangu wa KIISLAM akisimama mahali analizungumzia katika upande wa UDINI.

Sikilizeni, TEC imejaa watu wenye ELIMU kuanzia ya Elimu Dunia hadi elimu ya DINI (THEOLOJIA), ndo maana utasikia Askofu Dr, Eng, Prof fulani fulani wa Parokia fulani. Sisi ukishamqliza kusoma Quran umemaliza, mengineyo ni majungu. Yaani mtu kama Prof Lipumba alitakiwa awe Imamu wa Msikiti fulani mahali fulani na kiongozi fulani katika nafasi za Bakwata taifa, lakini matokeo yake kule tumewaweka wengine. Sisemi kwamba waislam hatujasoma, hapana, PhD zilizopo katika nafasi za uongozi misikitini ni chache mno kulinganisha na wenzetu.

Ndo maana linapofikia jambo la kuongea na kiongozi mkuu wa nchi, hawa TEC, KKKT na mengineyo utaona utofauti, sisi runaomba kupunguziwa ama kuondolewa kodi za TENDE na kuomba tupatiwe VIFAA vya kisasa vya KUUTAZAMA MWEZI mtukufu. Wenzetu wanaomba mismaha ya kodi ya makontena ya vifaa tiba, vifaa vya elimu na mengineyo. Sisi tukishakunywa juisi za tende Ikulu tunashukuru na kuondoka na kushika shikashika videvu kama SUNNAH, tunaondoka.

Leo tunawaona TEC wabaya katika msimamo, mali zetu wenyewe tunashindwa kuzisimamia wenyewe, hapa Kinondoni nadhani kidogo tupigwe na wachache kwenye eneo letu ambalo Bakwata ipo. Tumshukuru Hayati Magufuli (Mkristo) alitusaidia na kutuombea msaada wa kujengewa Msikiti.

Kuna namna nawatazama viongozi kama wanafki, na mnafki siku zote maendeleo kwake yanakawia. Najua huu ujumbe mchungu na mnaweza hata kuitisha kikao mkanisomea ALBADIRI. Ndio, TEC wametoa WARAKA wenye HOJA, mbona hamzikosoi HOJA zao mnajikita katika UDINI? Kwani huu mkataba unaopingwa nyinyi hamkwenda IKULU pamoja nao kabla ya huu waraka? Mlienda kufanya nini? Si mlipeleka mapendekezo ya marekebisho?

Mbona leo mnasita kusema kwamba mlikuwa pamoja? UNAFKI mtupu! Ndo maana katika viongozi wa kidini namkubali Sheikh Nurdin Kishki, Mziwanda, Mazinge na Dr Sulle. Hawa hawana manenomaneno, kazi yao ni kutoa DAGH'AWA tu. Huu unafki nafki umebaki kwa wasiotambua wajibu wao. Kuna shule nyingi za kiislam, matokeo yake ni mabovu. Hatuangalii kuboresha shule zetu, tumekazana kuvaa kanzu na misuli kuzodoana. Tuache Unaa. Astaghafirulah!

Mmenikwaza sana. Kuna huo Sheikh mmoja amesema yeye atasambaza waraka wa kuunga mkono nchi nzima kama tamko la msikiti, huyu hasababishi UDINI, hachochei Udini? Nani katika Uislamu amemuonya aache huo ujinga?

Mnahitaji semina! Mnahitaji kujitokeza na tamko lenye mashiko la aidha kwa nini mnaunga mkono ama mnapinga huu mkataba na muwe na sababu za kujitosheleza. Msijitokeze kwa sababu TEC wametoa WARAKA, mnatengeneza mashindano na mtachochea vurugu zisizo na msingi wowote.

Tuache UDINI, huu mkataba haupingwi kwa sababu ulisainiwa Msikitini au mbele ya imamu na wala huu mkataba hauhusiani na msikiti kwa maana DP World hawaji kujenga misikiti wala kueneza Quran. Wanakuja kuwekeza katika bandari zetu. Tukipinga tupinge kwa hoja na tukikubali tukubali kwa hoja.

Tunahitaji kueleweshana, inawezekana mimi sijaelewa na pengine akijitokeza mtu akanielewesha nitamuelewa na nitaunga mkono lakini ukitumia UDINI sintokuelewa. Maana naona kila anaesimama anasema "NYUMA YA PAZIA"; hiyo nyuma ya pazia kwenye ule waraka hiyo "NYUMA YA PAZIA" iko wapi?
 
Leo ndo ni meamini ukiwa nje ya dini ya uislamu akili zako zinakua na kasoro fulani (unakua na upungufu wa fahamu) ina onekana kama hujakamilika vizuri ona huyu anapoandika upupu wake kabisa, kwake anadhani kusoma theology ndo kua na akili na busara, ukimuuliza Yesu alikua na PhD ngapi? litakodoa tu macho, ukimuuliza mitume Paulo alikua kasoma wapi PhD ya theology atakujibu, wakati bibulia kaandika yeye kuanzia miaka ya 80 ad..........hi elimu dunia Inapoteza sana ndugu zetu wakrist.

Hao mapadiri unao sifia hujawahi kuishi nao ni wapumbavu na wajinga kabisa wanafanya vitu vya hovyo sanaa hizo PhD zao za theology hazija wabadili zaid ya kua Brainwashed na kua useless jatika jamii kuibia waumini masikini kwa njia ya kutoa sadaka.

Wameshindwa kuondoa umasikini miongoni ma wafuasi wao ambao wanaishi kwenye umasikini uko vijijini hao wasomi wanasaidia je jamii yao.
 
Leo ndo nimeamini ukiwa nje ya dini ya uislamu akili zako zinakua na kasoro fulani inaonekana hujakamilika vizuri ona huyu mgalatia anapo andika upupu wake kabisa, kwake anadhani kusoma theology ndo kua na akili na busara, ukimuuliza Yesu alikua na PhD ngapi? Litakodoa tu macho, ukimuuliza mutume Paulo alikua kasoma wapi PhD ya theology atakujibu,..........hi elimu dunia Inapoteza sana ndugu zetu wakristu hao mapadiri unao sifia hujawahi kuishi nao ni wapumbavu na wajinga kabisa wanafanya vitu vya hovyo sanaa hizo PhD zao za theology hazija wabadili zaid ya kua Brainwashed na useless kuibia waumini masikini kwa njia ya kutoa sadaka.
Soma tena comment Yako utajua unakubaliana nae kua viongozi waislan sio wasomi 😂😂
 
Soma tena comment Yako utajua unakubaliana nae kua viongozi waislan sio wasomi [emoji23][emoji23]
Kusoma circulars na kusoma dini yote ni elimu hamna imamu ambae hajasoma theology hayupo ila kuna walokole hata kiswahili kinampa shida kusoma lakini anaongoza watu.
 
Uzi huu ni kama umeamkia kule Ukraine au Congo sehemu zenye waasi inabidi utafute namna ya kuyakabili mapambano mleta uzi kuna kibibi kitakatisha usingizi huko na kuja kukushambulia kikisaidiwa na kaka zake boko haramu na Al shababu wa nyuma ya keyboard bila kuungalia uzito wa ulichokifikisha
 
Kusoma circulars na kusoma dini yote ni elimu hamna imamu ambae hajasoma theology hayupo ila kuna walokole hata kiswahili kinampa shida kusoma lakini anaongoza watu.
Lakini kwenye mikataba kunahitaji wasomi wa elimu Dunia Sasa😂😂
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom