Pre GE2025 NEC: CCTV zifungwe kuepusha wizi wa kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hizo hela za kuweka CCTV ni bora zikaboreshe sekta ya afya, elimu na barabara. Maana CCM wataiba tu hizo kura kama kawaida yao
 
Halafu DVR zimilikiwe na CCM? Hapo ni kaz bure. Kikubwa katiba mpya, tume huru isiyokua nominated na Rais, uchaguzi wa kielektroniki!!
 
Naunga mkono hoja 👍👏🤝
 
Kuna mtu humu JF alitoa ushuhuda wa namna wakivyoamriwa wafanye wizi wa kura kwenye uchafuzi wa 2020.Marehemu apate 98 asilimia.
 
Tume huru ya uchaguzi bila watu wenye uhuru na usalama kwenye misimamo yao ni ushamba tu jalponi hatua nzuri lakini watu wanakuwa serikali au kwenye mihimili iundayo serikali lakini inakuwa michawa tu.
 
Lissu alipigwa Risasi ma CCTV zilikuwepo zilisaidia nini
 
Watakwambia gharama ni kubwa mno. Lakini kununua washa washa haihitaji mjadala.
 
CCTV ya modewji si mbona iliwekwa wazi...

Hiyo ya Tundu Lissu nayo wahusika hawakuonwa kwa sura....

Lakini hii ya uchaguzi lazima uingie kwenye chumba ukiwa unaonekana, hivyo ni rahisi kumtambua mtu endapo akifanya ujinga.

Na wewe ukauamini huu ujinga kuwa ndio picha za CCTV zikionyeshw gari lililotelekezwa na waliomteka Mo?
 
Hao wanaozuia mawakala wa upinzani kuingia vituoni ndio watakaozima hizo CCTV cameras.
 
Nani atasimamia hizo CCTV?
 
Saver itakuwa monitored na nani? Kwanini tutumie bilions of money kwa uchaguzi tu na sio kuleta maendeleo?
 
Ni sawa lakini hili si tatizo la msingi kwa sababu mfumo ndo umejikita kutokutenda haki. Tutafute suluhu ya kurekebisha huo mfumo batili na haramu
 
Alipokuwa anqishi Tundu lisu kule Dom zilikuwepo! Baada ya tukio la kupigwa risasi Kuna wamba walikuja kuzinyofoa! Labda mtuambie wale wamba wachomoao CCTV kwenye barabara issue tata wamekufa wote na makaburi yao tumeyaona ndo tutakubali ziwekwe
 
Yaani watu wanaua watu Ili washinde waje wazuiwe na CCTV camera...........!

Tuacheni utani kabisa na ccm, manunuzi yenyewe lazima iwe mara kumi zaidi ya bei halisi. Kwasasa ccm wakuwazuia ni wananchi wenyewe kama wataamua kuwa ccm sasa basi kwa kuwa wasimamizi wakuu wa uchaguzi wakati wa kura.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…