Pre GE2025 NEC: CCTV zifungwe kuepusha wizi wa kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
CCTV ZILIFUNGWA KWENYE LANGO LA KUINGIALIA NYUMBA ALIYOKUWA ANAISHI TUNDU LISSU WAKATI ANAPIGWA RISASI DODOMA LAKINI BAADA YA TUKIO ZILIONDOLEWA MPAKA LEO HIVYO HIZO ZA NEC NAZO ZITAONDOLEWA NA WAHUSIKA
SULUHISHO NI TUME HURU YA UCHAGUZI NA KATIBA MPYA TU.[emoji779][emoji779]
 
Kura zinazoibwa katika mfumo ndani ya tallying system ya kura itazuiwaje na CCTV cameras?

Kura za Urais zitalindwa na camera ikiwa hakuna Tume HURU ya UCHAGUZI yenye uwezo kuruhusu Matokeo ya Urais kihojiwa mahakamani?

Rudi kufikiri UPYA.
 
CCTV mpaka vijijini ndani kabisa. ??!!
Vituo vilivyopo vijijini ndio vingi zaidi kuliko vilivyopo mijini !!
Najaribu kuwaza sijui kama inawezekana !! Kama fomu tu vituo vingine huwa zinachelewa kufika πŸ˜…πŸ˜…
 
Nadhani unajichanganya mwenyewe kwa kutojua.
Teknologia haiwezi kuzuia chochote iwapo inatumiwa na huyo huyo anayeitumia kufanya uhujumu.
Hii itakuwa ni kama kiini macho tu cha kudanganyia watu waone kwamba hujuma haifanyiki, kwa vile tu kuna mazingaombwe ya CCTV yaliyowekwa na kutumiwa na huyo huyo mhujumu ili kukidhi matwakwa yake ya hujuma.

Sasa umetaja CCTV za matukio ya Mo na Tundu Lissu, kuwa zipo, lakini wakati huo huo unasahau kwamba hazikusaidia chochote; wewe huoni mchanganyiko huo unaovuruga pendekezo hili unaloleta hapa?
 
CCTV mpaka vijijini ndani kabisa. ??!!
Vituo vilivyopo vijijini ndio vingi zaidi kuliko vilivyopo mijini !!
Najaribu kuwaza sijui kama inawezekana !! Kama fomu tu vituo vingine huwa zinachelewa kufika πŸ˜…πŸ˜…
Ni pendekezo lisilokuwa na miguu.
 
Siyo Ccm!!!
 
Nani atakuwa ana monitor hizo CCTV?
Au ndo nyani anamchunga ngedere asiibe mahindi shambani
 
Nani atakuwa ana monitor hizo CCTV?
Au ndo nyani anamchunga ngedere asiibe mahindi shambani
Kila mwakilishi wa chama kinachogomgea anakuwemo kwenye Chumba cha CCTV kutizama
 
Tutaingia gharama za bure tu. Muarobaini ni Tume Huru ya Uchaguzi (Independent Electoral Commission) inayojitegemea, yenye watumishi wake yenyewe na matokeo ya wagombea wote yapingwe mahakakamani.
Waangalizi wa Uchaguzi wa ndani na nje wawepo tangia kwenye kampeni mpaka kutangazwa kwa kura. Mabox ya kupigia kura yawe ya Vioo au Plastic isiyo na kificho.
CCTV camera nani atakuwa anazi-monitor in real time nchi nzima?
Zinaweza kufaa tu, kwenye ushahidi Mahakamani.
 

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…