NEC igeni CCM jinsi ya kuhesabu kura. CCM mmeonyesha mfano

NEC igeni CCM jinsi ya kuhesabu kura. CCM mmeonyesha mfano

Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, ameagiza kwamba kura za maoni za Ubunge, uwakilishi na udiwani zinazoanza leo zihesabiwe hadharani kama ilivyokuwa wakati kuhesabu kura za Wagombea Urais wa Zanzibar.

Hata mimi jambo hili nimeliwaza labda ndio mpango mzima, tume ya uchaguzi ikifanya hivi, hakuna tena malalamiko ya kuibiwa kura au habari za tume huru... ngoja tuone, labda ndio njio ya jiwe kutafuta legitimacy ya uchaguzi huru na wa haki... atatua mzingo muda si mrefu kama kweli uraisi ni kazi...
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Uchaguzi tayari? au ni kuropoka ropoka kama mgonjwa wa C1
Ndiyo kuthibitisha WIZI WAO Mkuu. Kura za maccm TRANSPARENCY kama kawa lakini kura za uchaguzi Mkuu TRANSPARENCY kwenye kuhesabu ni SIFURI.
U
 
Kutoka kwa Askofu Bagonza

MAONI NA MAONO Vs
KURA NA KODI

Mchakato wa uchaguzi mkuu unaendelea nchini kote. Tunasikia mengi, tunashauri mengi. Usipojishauri, unashauriwa. Nina mawili:

1. Katika zoezi la upigaji wa kura za maoni, ni muhimu kuazima hekima ya wahenga wasiojulikana isemayo kwamba " wenye maono hawana nafasi na wenye nafasi hawana maono". Kura za maoni hazina uhusiano na maono na watia nia.

2. Nchi inaendeshwa kwa kodi zetu. Hata mikopo inayochukuliwa ni hela yetu. Tutalipa kwa muda mrefu. Hata wasiozaliwa bado watalipa mikopo hiyo. Usimpe kura mtia nia bila kumpa kodi. Kura yako iende na kodi yako. Kura bila kodi inawafanya watawala wetu kukusanya kodi kama hela yao binafsi. Wanatumia kodi kama fedha binafsi! Tuwe macho. Kodi bila kura inawafanya wapiga kura kuwa kama vibarua katika shamba la tajiri. Tuwe macho, tupige kura na kulipa kodi. Tukiishalipa kodi, tusiziombe, tuzidai.

Daima tukumbuke, uchaguzi huru na wa haki, huhamisha mamlaka kutoka kwa watawala kwenda kwa wapiga kura. Uchaguzi kiini macho, hukomba madaraka kutoka wananchi kwenda kwa watawala na koo zao.
 
Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, ameagiza kwamba kura za maoni za Ubunge, uwakilishi na udiwani zinazoanza leo zihesabiwe hadharani kama ilivyokuwa wakati kuhesabu kura za Wagombea Urais wa Zanzibar.
Mkuu tuwe wakweli Magamba wanaendesha kura hizi vizuri.
Japo uchaguzi mkuu watavuruga tu
 
Kama wanafanya vizuri kwenye kura zao kwanini WASHINDWE kufanya vizuri kwenye kura za uchaguzi Mkuu!? Mambo yote yawekwe hadharani bila woga wala kificho. Kama Malawi wameweza na Tanzania pia TUNAWEZA.

Mkuu tuwe wakweli Magamba wanaendesha kura hizi vizuri.
Japo uchaguzi mkuu watavuruga tu
 
Chama changu CCM kinapenda sana haki, bila shaka kitashauri tume ya uchaguzi ifanye hivihivi kama walivyofanya kwenye chaguzi za ndani..
 
Kama wanafanya vizuri kwenye kura zao kwanini WASHINDWE kufanya vizuri kwenye kura za uchaguzi Mkuu!? Mambo yote yawekwe hadharani bila woga wala kificho. Kama Malawi wameweza na Tanzania pia TUNAWEZA.
Hawapendi aibu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Si AIBU Mkuu ni kudumisha uhai wa Taifa kwa kuhakikisha UHURU na HAKI ya wapiga kura kumchagua wamtakaye inaheshimiwa.

Hawapendi aibu
 
Hivi kwani kura za Rais JMT zile za mkutano mkuu zilihesabiwa hadharani ?Magufuli za wenzake tu ndo zinahesabisawa hadharani. Zinazomhusu zitahesabiwa kifichoni.
 
wazi wazi na mubashara ndio njia pekee iliyobaki kuelekea october
 
Kwa kweli utaratibu walio utumia CCM kuhesabu kura japo unatumia muda mwingi lakini ni utaratibu mzuri sana kwa nchi ambazo hazina teknologia kubwa kwenye chaguzi.

1. Kura zinapigwa kwa uwazi
2. Wakati wa kuhesabu zinaonyweshwa na muhusika anapokea kura zake
3. Muhusika ndio ana andika kura zake kwemye daftari za kura na kusaini.
4. Muhusika anazihesabu hadharani
5. Matokeo yanatangazwa vizuri.


Kwa kweli nimependa namna hii ya uchaguzi.

Sasa maCCM hayahaya kwenyeUchaguzi Octoba 25 hayataki mawakala wa Vyama vya Upinzani wawepo.

Si jui kuna pepo gani kwenye vichwa vya wana CCM.
 
macho ya NEC huesabu kura kwa remote ya sisisemu, ndio maana kura zote huziona ni za kijani.
 
Hata machadema inabidi yaige!

Kwanza waliosema Magufuli kaiweka ccm mfukoni sijui wanajisikiaje
 
1595265675393.jpeg


Chama changu CCM kinapenda sana haki, bila shaka kitashauri tume ya uchaguzi ifanye hivihivi kama walivyofanya kwenye chaguzi za ndani..
 
Kama anataka UWAZI kwenye kura za maoni katika kuhesabu kura sioni sababu ya yeye kuukimbia UWAZI huo huo kwenye kuhesabu kura za uchaguzi Mkuu ili tuzijue mbivu na mbichi.
Mhhhh itawezekana kweli?.😃
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom