Uchaguzi 2020 NEC imecheza ngoma ya Tundu Lissu. Je, Wagombea walioenguliwa Ubunge Tume itawarudisha?

Hoja ya picha imejibiwa?
 
Hata darasani tunaingia muda sawa, tunatoka muda sawa, tunafundishwa na Mwalimu mmoja. Ila kuna mi-mburula inapata sifuri wakati wengine tunapata 80% au 100%.
Pole kwa kuwa na kilema cha UPUMBAVU, hatuna msaada na wewe
 
Tume iko sahihi katika maamuzi yake dhidi ya mapingamizi za Lissu kwa vile hazikuzingatia facts za matukio, makosa ya kiufundi kuhusu picha( iwapo ni kweli madai yake)- na ukubwa wa athari au madhara ya ukiukwaji ( gravity of the breach ) na kama itaathiri haki za msingi za mpiga kura chini ya sheria ya uchaguzi hadi kupelekea kutengua uteuzi. Aidha hakuzingatia kanuni ya kukasimu madaraka kwenye sheria ya uchaguzi wakati wa kujenga hoja.Jambo lingine kuhusu maamuzi ya mapingamizi au rufaa za majimbo zitaamuriwa kwa msingi wa merits kwa kila shauri na si vinginevyo. Cha msingi wasimamizi waruhusu rufaa kuifikia Tume na si kuzizuia ie Morogoro iwapo ni kweli. Mapingamizi ya Lissu ni ya kisiasa zaidi kutafuta umaarufu na upotoshaji.
 

Ni kifungu gani cha sheria tume inaweza kukasimisha madaraka yake kwa watu wengine?

Kuhusu Membe, siyo lazima Lissu aweke mapingamizi kwa wote, na ana haki ya kuweka pingamzi kwa yeyote

Siyo kweli eti kulikuwa na sababu za kumuengua, ukweli ni kwamba hazikuwepo kwa sababu yeye alifuata sheria, wengine walifuata maelekezo ya tume yaliyokinyume cha sheria. Na Tume haiwezi kutoa maelekezo yaliyokinyume cha sheria ikawa sahihi, ikifanya hivyo haiwi kinga ya kuvunja sheria

Unadai eti kaachiwa tu ili iwe fair play, fair play ipo kwenye kifungu namba ngapi cha sheria?.
Mbona wagombea wengine wa udiwani na ubunge wanafanyiwa uhuni lakini Tume haijawaachia wagombee ili iwe fair play? , yeye Lissu ana nini hadi aachwe kugombea kama amevunja sheria?

Anayeweza kuachiwa agombee kwa kuvunja sheria ni Magufuli maana tunajua tume siyo huru na inagwaya watawala
 
Mkuu naona kama vile unatumia nguvu nyiiingi kwa jambo usilolijua. Kunywa maji utulie haya yamekuzidi kimo
 
Shida ya Bawacha ni kusaidiwa kufikiri hebu wasikilizeni NEC walivyo wajibu! Lissu ni muongo wa kutupwa
 
Tume haijatoa kifungu chochote cha sheria wala kanuni kukataa mapingamizi ya Lissu yaliyosheheni hoja nzito za kisheria na kikanuni zaidi ya maelezo ya jumla jumla tu!
 
Nani kakwambia ?????? Unahamisha goli eeeh???? Picha alipeleka ila msimamizi akasema hazikubandikwa
You see ...SASA kama hazijabandikwa INA maana hazijagongwa na stamp ya chama kinachomdhamini ktk form husika ili kudhibitisha uhalali wa anayerejesha form Kwa jina na sura
 
Sio lazima. Muhimu hoja yake imeeleweka.
 
You see ...SASA kama hazijabandikwa INA maana hazijagongwa na stamp ya chama kinachomdhamini ktk form husika ili kudhibitisha uhalali wa anayerejesha form Kwa jina na sura
Nani kakwambia usipobandika inamaanisha haijagongwa muhuri???? Wewe jamaa unafikiri kwa kutumia nini???
 
Tume haijatoa kifungu chochote cha sheria wala kanuni kukataa mapingamizi ya Lissu yaliyosheheni hoja nzito za kisheria na kikanuni zaidi ya maelezo ya jumla jumla tu!
Tume ya Taifa ya uchaguzi Tanzania ime idhiirishia dunia kuwa inaendeshwa kwa Mihemko na sio kwa Sheria na Kanuni.
 
Hahahaha umeandika kwa uchungu sana sana
 
Nani kakwambia usipobandika inamaanisha haijagongwa muhuri???? Wewe jamaa unafikiri kwa kutumia nini???
Huo muhuri inabidi uguse/ overlap kwenye fomu husika.

Naona unaanza kuhoji natumia nini kufikiri?... hopefully hutanitukana kama hujapenda maoni yangu.
 
Ninachojiuliza hivi ni kwanini kila wakati tunasikia wameenguliwa wangombea wa upinzani tu?? Na au wapita bila kupingwa wagombea wa CCM tuu???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…