Uchaguzi 2020 NEC imemteua Bernard Membe kugombea Urais na Omary Mohamed Umakamu wa Rais kupitia ACT-Wazalendo

Uchaguzi 2020 NEC imemteua Bernard Membe kugombea Urais na Omary Mohamed Umakamu wa Rais kupitia ACT-Wazalendo

Akizungumza muda mfupi baada ya kuidhinishwa na NEC amesema Kuna Vigogo wakubwa wanatarajia kuondoka CCM na kumuunga mkono, pia amesema wanahabari watakuwa huru katika utawala wake.

#KAZI NA BATA
 
Kwa yanayotendeka sasa nchini, kusema ukweli ni aibu mno kuwa mwana CCM. Ni utawala wa ajabu sana huu kuwahi kutokea hapa nchini. Kiongozi anahodhi kila kitu bila hata ya kuona aibu yoyote ile.
 
Aisee!!

Nakumbuka uchambuzi wa yule jamaa mwosha viatu.
 
Akiongea baada ya kupitishwa na tume Membe amesema endapo tume watafanya mchezo nchi itachafuka.

Anasema ketendo Cha Kila kitu kufanywa kwa matakwa ya mtu mmoja kisa tu Ni Rais wa nchi kinaweza leta machafuko na Wala hayatazuilika kirahisi.


Amesema yeye ametembea nchi nyingi kama mwangalizi wa uchaguzi ila haya yanayofanyika Tanzania Ni kuhatarisha amani ya taifa letu pendwa..

Amesema ni wajibu wa Kila mtu kutenda haki ili watanzania wapate kiongozi wa matakwa yao.

Sio kuchaguliwa kiongozi.
 
Sisi wananchi tukipigana yeye atajifungia kwenye gari,kama ni kuandamana yeye atangulie mbele
 
Back
Top Bottom