Uchaguzi 2020 NEC: Tulifanya uteuzi wa wabunge wa viti maalum baada ya orodha ya majina hayo kuwasilishwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA 19 Novemba 2020

Uchaguzi 2020 NEC: Tulifanya uteuzi wa wabunge wa viti maalum baada ya orodha ya majina hayo kuwasilishwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA 19 Novemba 2020

Hili sakata la wabunge wa kuchonga wa viti maalum 19 mchakato wake hadi lilipofikia hatima yake Jana kwa kufukuzwa na chama tulicho aminishwa kuwa kimewadhamini ni kufanya kukosa sifa ya msingi ya kuwa wabunge, linatosha kabisa kwa Spika na DG wa NEC Kujiuzulu kulinda heshima ya ofisi wanazo tumikia.

Imegundulika wazi kuwa mchakato mzima umehusisha JINAI nyingi ikiwemo kugushi, uongo, nyaraka bandia, matumizi mabaya ya ofisi, kunajisi mfumo wa sheria za mahakama na magereza nk.

Ni wajibu wa taasisi za mambo ya kijamii kujitokeza kwa uwazi na kutamka Spika Ndugai na mkurugenzi wa NEC Mahera wajiuzulu maana kwanza wametenda jinai ambayo ilipaswa washtakiwe lakini pia wameshusha heshima ya vyombo hivyo wanavyo viongoza na sasa sio ndani tuu ya nchi bali hata nje vitaonekana ni vya kihuni.
#NDUGAIOUT
#MAHERAOUT
 
Out wanayoweza tOKa ni ya bia na nyama choma tu..
 
Hili sakata la wabunge wa kuchonga wa viti maalum 19 mchakato wake hadi lilipofikia hatima yake Jana kwa kufukuzwa na chama tulicho aminishwa kuwa kimewadhamini ni kufanya kukosa sifa ya msingi ya kuwa wabunge, linatosha kabisa kwa Spika na DG wa NEC Kujiuzulu kulinda heshima ya ofisi wanazo tumikia...
Usemacho ni kweli lakini kwa nchi hii haiwezekani wakatolewa. Tujizoeze kuishi nao kama tunavyoishi na Covid 19 maisha yaendelee
 
Kupitia aina ya madudu na upambavu wakati na baada ya uchaguzi sijivunii uanachama na upenzi wa ccm, serikali na nchi hii, Ni ushamba, upambavu, ubabe wa kijima, ni aibu na huzuni kubwa sana sana. Ubabe na dhuluma za kishamba ni sumu kwa Taifa.

Niwape pole wapenda demokrasia na amani, Mungu kwa hakika atatoa hukumu stahiki ndani ya miaka mitano hii hamna hati miliki ya uhai na mambo mengine yote, naamini wazee wetu ndani ya ccm na waandamizi wastaafu mioyo yao ina mshangao, huzuni na tafakari isiyoisha. Why? is it about third term seeking strategy?

With third term plan constitutionally someone is purely dreaming mythically. Eeh Mungu umetulinda na tulinde na nchi yetu daima pasipo kuchoka. International community are you asleep? We hope the international community will vehemently say something soon. Tanzania, haki, usawa, demokrasia, utu ni vya msingi kuliko manufaa binafsi yoyote yale.
 
Kupitia aina ya madudu na upambavu wakati na baada ya uchaguzi sijivunii uanachama na upenzi wa ccm, serikali na nchi hii, Ni ushamba, upambavu, ubabe wa kijima, ni aibu na huzuni kubwa sana sana. Ubabe na dhuluma za kishamba ni sumu kwa Taifa...
Barikiwa mkuu, Tanzania kwanza.
 
Wafia vyama. Esther Matiko mke wa Mwalimu yule mgombea mwenza. Eti kaenda bungeni bila mmewe kujua. Mbowe wote hao wanajua sana na wapo Ok.

Sema wanaplay games ili kuwapoza wafia vyama ambao hajawahi hata faidika na Chadema. Mbowe anaingiza ruzuku tu. Mimi ndo maana nasema wote wawe Chadema,CCM .....etc. Tanzania ndo chama langu. Kura nitampigia mtu na siyo sababu ya chama chake.
Wewe ni snitch kinyama.
 
Sasa yule aliekuwepo jela na kutolewa tarehe 23 usiku jee ninani aliye jua kama serekali itaachana na kesi ile??
 
Chadema wala hawatajisumbua kwa kua hili jambo bila shaka lina baraka na ofisi ya Rais.
Kwanini tume na CDM wasishirikiane pamoja kumfahamu mhalifu aliyehusika na ghushi hiyo bila kujali ni kutokea tume au CDM?

Tume haioni kuwa inapakwa matope na sasa ni mtuhumiwa wa hii ghushi?

Si kuwa wanaohangaika kuwasimika wabunge hawa magumashi wana cha kufanya na hii ghushi?
 
Umesoma vizuri barua ya NEC hapo juu? Au umeanza kuchangia bila kusoma barua ya NEC? Wanasema walipokea barua tarehe 19/11/2020.
Hao hao NEC tarehe 20/11/2020 walisema kufikia muda huo walikuwa hawajapokea majina kutoka Chadema. Unaweza kuona screenshot ya picha hapa chini
azaman tv.jpg

Link ya taarifa ya habari youtube ni

Halafu jana wanakana maneno yao wenyewe wanasahau kuwa kuna video walirekodiwa. Tarehe 20/11/2020 walisema hawajapokea majina halafu leo wanatuambia walipokea majina tarehe 19/11/2020. Bado unajitoa ufahamu kwa kujifanya huoni kama NEC wanacheza mchezo?
 
Haya matakataka yalianza huu mchezo hata kwenye uteuzi majimboni walikuwa wakijiandikia barua za kuteuwa watu wasio wa chadema. Chadema ilikuwa ikipeleka iliowateuwa wanaambiwa tumeishatoa form. Yametokea kibamba, Luangwa na sehemu nyingine nyingi. Hatuwezi kushangaa hili.
Utawala huu hauheshimu sheria hivyo yapo mengi ya ajibu tutayasikia na kuusoma.
 
Hao hao NEC tarehe 20/11/2020 walisema kufikia muda huo walikuwa hawajapokea majina kutoka Chadema. Unaweza kuona screenshot ya picha hapa chini
View attachment 1636507
Link ya taarifa ya habari youtube ni

Halafu jana wanakana maneno yao wenyewe wanasahau kuwa kuna video walirekodiwa. Tarehe 20/11/2020 walisema hawajapokea majina halafu leo wanatuambia walipokea majina tarehe 19/11/2020. Bado unajitoa ufahamu kwa kujifanya huoni kama NEC wanacheza mchezo?

Inawezekana ilipokelewa tarehe 19/11/2020 lakini ilikuwa haijawafikia wakubwa ilikuwa bado iko kwa junior staff!
 
Back
Top Bottom