NECTA yaacha Utaratibu wa Kutangaza Wanafunzi bora na Shule bora kwa Kidato cha 4

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Baraza la mitihani NECTA limesitisha utaratibu wa kutangaza shule bora na mwanafunzi bora wa matokeo ya kidato cha nne

Kaimu katibu Mtendaji wa Baraza la mitihani Tanzania NECTA Athumani Salumu Amasi amesema utaratibu huo wa kutangaza shule bora ulikuwa unazitangazia biashara baadhi ya shule

"Unamtaja mtu kwamba ameongoza katika kundi ambalo pamoja na kwamba wamefanya mtihani huo huo lakini hawakusoma katika mazingira yanayofanana, alafu sasa unampa sifa mtu mmoja"

Kuhusu kumtangaza mwanafunzi bora wa mtihani huo amesema hakuna tija katika hilo kwani hauwezi kumtangaza mwanafunzi mmoja katika ya wanafunzi wote Tanzania ambao huenda pia mazingira yao ya kusoma yalikuwa tofauti

Chanzo: EA Radio
 
Hatimaye leo wamejitambua.....naunga mkono hoja.
 
Dah. Wengine tuliutafuta uTO kwa udi na uvumba tukachemka.
Darasa letu la form six PCB liligeuka bweni. Watu walihamishia hadi mabegi darasani. Sahani, pasi, ndoo za kuogea zote zilihamia darasani. Hadi mashuka tulikuwa tunafua na kuanikia darasani.
Kuna siku hadi mwalimu alikataa kufundisha maana darasa halikuwa na muonekano wa darasa.
 
Matangazo yalivyokua

"Shule imekua ya 65 kitaifa, mlete mwanao kwenye ufaulu bora"

Matangazo ya shule za private yatakua kama ifuatavyo

"Shule ina bembea za kisasa walimu warembo, uwanja mkubwa wa mpira, ewe mzazi unangoja nini kumleta mwanao sasa acheze mpaka asaze" 😂
 
Back
Top Bottom