NECTA yaacha Utaratibu wa Kutangaza Wanafunzi bora na Shule bora kwa Kidato cha 4

NECTA yaacha Utaratibu wa Kutangaza Wanafunzi bora na Shule bora kwa Kidato cha 4

Kumbe wengi tuu walikuwa hawaipendi hii kitu.
Wengi tu. Leo Illboru ina division One 100 na Two moja. Hawana 3,4 na Zero. Unaenda kumlinganisha na shule ya kata Chinyika iliyopo Mpwapwa vijijini na unampa zawadi Mkuu wa shule na mwanafunzi aliyefanya vizuri obvious ni yule wa Ilboru. Unategemea mpaka Masiah arudi zawadi au sifa za kutangazwa kwamba shule x na mwanafunzi y wametoka Chinyika itakuja kutokea?
 
Afadhali, maana kuna wakati unafikiria mwanafunzi anaenda shule anavuka mabonde na milima kwa miaka minne umlinganishe na mwanafunzi anaelala na kuamka hapo shuleni then mwenye mazingira mazuri ndio anakua bora?

Kuna shule ya secondary ipo moja kata nzima, inahudumia vijiji zaidi ya vitano, mwanafunzi anavuka mito mitatu ndio anafika shule, mwanafunzi huyu huyu anapata division one lakini hawi bora!
 
Matangazo yalivyokua

"Shule imekua ya 65 kitaifa, mlete mwanao kwenye ufaulu bora"

Matangazo ya shule za private yatakua kama ifuatavyo

"Shule ina bembea za kisasa walimu warembo, uwanja mkubwa wa mpira, ewe mzazi unangoja nini kumleta mwanao sasa acheze mpaka asaze" 😂
Sasa Mjomba hata hizo "division" si zinajieleza tu??? Mfano mzuri ni matokeo ya "FEZA GIRLS" - watoto wote wana "Div 1 (One)", na wengi tu wana Div 1 (one) ya "Point 7", sasa hapo watashindwaje kujitangaza??? Hilo ni tangazo la kutosha; Kwa kifupi watawapa shida wale wazazi waliozea kusubiri kutangaziwa na shule, kwa mzazi anaetafuta shule kupitia matokeo ya "NECTA" - bado anaweza kuona shule bora ni ipi.
 
Baraza la mitihani NECTA limesitisha utaratibu wa kutangaza shule bora na mwanafunzi bora wa matokeo ya kidato cha nne

Kaimu katibu Mtendaji wa Baraza la mitihani Tanzania NECTA Athumani Salumu Amasi amesema utaratibu huo wa kutangaza shule bora ulikuwa unazitangazia biashara baadhi ya shule

"Unamtaja mtu kwamba ameongoza katika kundi ambalo pamoja na kwamba wamefanya mtihani huo huo lakini hawakusoma katika mazingira yanayofanana, alafu sasa unampa sifa mtu mmoja"

Kuhusu kumtangaza mwanafunzi bora wa mtihani huo amesema hakuna tija katika hilo kwani hauwezi kumtangaza mwanafunzi mmoja katika ya wanafunzi wote Tanzania ambao huenda pia mazingira yao ya kusoma yalikuwa tofauti

Chanzo: EA Radio

Tangazeni tu…hamna ambae hapendi hayo mazingira bora.kama kweli wanafaulisha sio kosa lao

Siungi mkono hoja ya kutotangaza ni woga+wivu

Isipokuwa tunaweza kuweka list pekee ya private,list ya special schools za bweni na list ya kayumba

Lengo ni kujenga sio kubomoa
Bora inyeshe tuone panapovuja!
 
Baraza la mitihani NECTA limesitisha utaratibu wa kutangaza shule bora na mwanafunzi bora wa matokeo ya kidato cha nne

Kaimu katibu Mtendaji wa Baraza la mitihani Tanzania NECTA Athumani Salumu Amasi amesema utaratibu huo wa kutangaza shule bora ulikuwa unazitangazia biashara baadhi ya shule

"Unamtaja mtu kwamba ameongoza katika kundi ambalo pamoja na kwamba wamefanya mtihani huo huo lakini hawakusoma katika mazingira yanayofanana, alafu sasa unampa sifa mtu mmoja"

Kuhusu kumtangaza mwanafunzi bora wa mtihani huo amesema hakuna tija katika hilo kwani hauwezi kumtangaza mwanafunzi mmoja katika ya wanafunzi wote Tanzania ambao huenda pia mazingira yao ya kusoma yalikuwa tofauti

Chanzo: EA Radio
Waweke ada ya kutangaza majina ya shule zilizofanya vizuri tukusanye mapato😂🤣🤣
 
Vizuri sana kwakutambua jambo hilo. Yajayo yanafurahisha kweli elimu sasa ni biashara.
 
Baraza la mitihani NECTA limesitisha utaratibu wa kutangaza shule bora na mwanafunzi bora wa matokeo ya kidato cha nne

Kaimu katibu Mtendaji wa Baraza la mitihani Tanzania NECTA Athumani Salumu Amasi amesema utaratibu huo wa kutangaza shule bora ulikuwa unazitangazia biashara baadhi ya shule.

"Kutangaza shule ya kwanza huenda tulikuwa tunakufanyia Marketing kwa kuitaja tu hiyo shule, shule zipo nyingi zaidi ya elfu 18, sasa unapotaja moja sidhani kama ina tija" amesema Athumani Salumu.

Kuhusu kumtangaza mwanafunzi bora wa mtihani huo amesema hakuna tija katika hilo kwani hauwezi kumtangaza mwanafunzi mmoja katika ya wanafunzi wote Tanzania ambao huenda pia mazingira yao ya kusoma yalikuwa tofauti.

"Unamtaja mtu kwamba ameongoza katika kundi ambalo pamoja na kwamba wamefanya mtihani huo huo lakini hawakusoma katika mazingira yanayofanana, alafu sasa unampa sifa mtu mmoja" amesema Athumani Salumu.

Utaratibu huu wa kutangaza shule ya kwanza kitaifa na mwanafunzi bora kitaifa umekuwa ukifanyia matangazo ya biashara shule zinazoibuka kidedea na kuchoea shule mbalimbali kujiingiza kwenye vitendo vya udanganyifu kipindi cha mitihani ili tu kutajwa kuwa ya kwanza wakati wa kutangazwa kwa matokeo.
 
Hakuna lolite hapo zimakwepwa kutangaza skul zinazovuta mkia toka kule kwa wala urojo maana wakitangaza skul bora lzm zilizoshika mkia piah zitangwazee.
 
utaratibu wa kutangaza shule bora na mwanafunzi bora ulianzishwa na viongozi wale ambao wanamiliki shule. Dhumuni ilikuwa ni kutangaza biashara ya shule zao.

Ukimfananisha samaki na simba kwa uwezo wa kukata mbuga nchi kavu, utakua umekosea sana maana mazingira ya samaki na maisha yake yote ni kwenye maji.

Vivyo hivyo ukilinganisha ufaulu wa wanafunzi ambao wanasoma mazingira tofauti kabisa na wanatoka katika familia tofauti kimazingira na kiuchumi sio sawa.

Katika hili, wamekua wakikosea tokea mwanzo, namshukuru Mungu kuwa sasaivi wamejitambua na kuacha huu ujinga.

Kazi iendelee.
 
Angeongoza mwanafunzi kutoka shule zetu za kata wangeacha pia?
 
Back
Top Bottom