NECTA yaacha Utaratibu wa Kutangaza Wanafunzi bora na Shule bora kwa Kidato cha 4

NECTA yaacha Utaratibu wa Kutangaza Wanafunzi bora na Shule bora kwa Kidato cha 4

Wengi tu. Leo Illboru ina division One 100 na Two moja. Hawana 3,4 na Zero. Unaenda kumlinganisha na shule ya kata Chinyika iliyopo Mpwapwa vijijini na unampa zawadi Mkuu wa shule na mwanafunzi aliyefanya vizuri obvious ni yule wa Ilboru. Unategemea mpaka Masiah arudi zawadi au sifa za kutangazwa kwamba shule x na mwanafunzi y wametoka Chinyika itakuja kutokea?
Iliboru siyo ya mchezo kabisa. Yaani division 1 zipo 100 na division 2 ipo Moja . Hiyo ni shule hasa
 
Baraza la mitihani NECTA limesitisha utaratibu wa kutangaza shule bora na mwanafunzi bora wa matokeo ya kidato cha nne

Kaimu katibu Mtendaji wa Baraza la mitihani Tanzania NECTA Athumani Salumu Amasi amesema utaratibu huo wa kutangaza shule bora ulikuwa unazitangazia biashara baadhi ya shule

"Unamtaja mtu kwamba ameongoza katika kundi ambalo pamoja na kwamba wamefanya mtihani huo huo lakini hawakusoma katika mazingira yanayofanana, alafu sasa unampa sifa mtu mmoja"

Kuhusu kumtangaza mwanafunzi bora wa mtihani huo amesema hakuna tija katika hilo kwani hauwezi kumtangaza mwanafunzi mmoja katika ya wanafunzi wote Tanzania ambao huenda pia mazingira yao ya kusoma yalikuwa tofauti


Chanzo: EA Radio
Ndo wamegundua sasahivi. . Ni jambo zuri
 
Wizara ya elimu iamue shule zitumie lugha moja ya kufundishia kuanzia elimu ya msingi mpaka chuo kikuu. Hii ya kubadili gear angani ndio chanzo cha ubovu wa elimu yetu.
Kama tukiamua lugha iwe kiingereza toka chekechea basi walimu wengi sana wa shule za umma itabidi warudi kujifunza hiyo lugha. Walimu wengi hawajui kiingereza, hata wale wa somo la English huwa wanalifundisha kwa kiswahili.
 
Huu utaratibu walikua nao Loyola secondary, mtoto akifanya mtihani huwezi kuona wametaja kawa wa ngapi,we utaangalia trend ya wastani wa marks zake tu..Sijui kwa miaka ya sasa hivi[emoji1745]
 
Matangazo yalivyokua

"Shule imekua ya 65 kitaifa, mlete mwanao kwenye ufaulu bora"

Matangazo ya shule za private yatakua kama ifuatavyo

"Shule ina bembea za kisasa walimu warembo, uwanja mkubwa wa mpira, ewe mzazi unangoja nini kumleta mwanao sasa acheze mpaka asaze" [emoji23]
[emoji3][emoji119][emoji119][emoji38][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]saafi sana watajua Hawajui

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Nilichogundua humu wanaofurahia huo uamuzi ni wavaakobazi ambao shule zao huwa zinashika mkia miaka yote tangu nchi ipate uhuru,pia wanaona wivu na chuki wakiona zile za mtakatifu fulani zimeongoza.kwa kifupi wavaakobazi wamefichiwa aibu.

Katika mashindano yote lazima ajulikane mshindi na aliyepoteza ili mshindi apongezwe aliyepoteza atiwe moyo apambane zaidi.
 
Back
Top Bottom