Binafsi bado sijashawishiwa na hizo sababu za kusitisha huo utaratibu, nilitamani wauboreshe badala ya kusitisha.
Kwanini, nasema hivyo. Sababu zangu ni hizi hapa.
1. Utaratibu ule uliongeza ushindani na kuchochea uwajibikaji miongoni mwa wamiliki, walimu na wanafunzi.
2. Ulichochea ubora katika utoaji wa elimu.
3. Uliwapa wahusika (serikali, taasisi binafsi, wazazi na wanafunzi) tathmini ya haraka na uhakika kujua walipotokea, walipo na wanapoelekea kielimu kulinganisha na wengine waliofanikiwa au kuanguka.
Kiujumla ule utaratibu ulikuwa unaleta Vibe ya kipekee katika masuala ya elimu.