NECTA yaacha Utaratibu wa Kutangaza Wanafunzi bora na Shule bora kwa Kidato cha 4

NECTA yaacha Utaratibu wa Kutangaza Wanafunzi bora na Shule bora kwa Kidato cha 4

wabongo watu wabishi sana
255625458414_status_13ba37e80cbd4928baefa195a8b58264.jpg
 
Dah. Wengine tuliutafuta uTO kwa udi na uvumba tukachemka.
Darasa letu la form six PCB liligeuka bweni. Watu walihamishia hadi mabegi darasani. Sahani, pasi, ndoo za kuogea zote zilihamia darasani. Hadi mashuka tulikuwa tunafua na kuanikia darasani.
Kuna siku hadi mwalimu alikataa kufundisha maana darasa halikuwa na muonekano wa darasa.
Elimu haitakiwi iwe hivyo Sasa ya kutafta u To

You just have to study hard
 
Wanaokosoa huu uamuzi wa NECTA hawana hoja za msingi, ni malofa.
 
utaratibu wa kutangaza shule bora na mwanafunzi bora ulianzishwa na viongozi wale ambao wanamiliki shule. Dhumuni ilikuwa ni kutangaza biashara ya shule zao.

Ukimfananisha samaki na simba kwa uwezo wa kukata mbuga nchi kavu, utakua umekosea sana maana mazingira ya samaki na maisha yake yote ni kwenye maji.

Vivyo hivyo ukilinganisha ufaulu wa wanafunzi ambao wanasoma mazingira tofauti kabisa na wanatoka katika familia tofauti kimazingira na kiuchumi sio sawa.

Katika hili, wamekua wakikosea tokea mwanzo, namshukuru Mungu kuwa sasaivi wamejitambua na kuacha huu ujinga.

Kazi iendelee.
Serikali haiji kuboresha mazingira ya shule zetu za kata kamwe maana hakuna ushindani
 
Dah. Wengine tuliutafuta uTO kwa udi na uvumba tukachemka.
Darasa letu la form six PCB liligeuka bweni. Watu walihamishia hadi mabegi darasani. Sahani, pasi, ndoo za kuogea zote zilihamia darasani. Hadi mashuka tulikuwa tunafua na kuanikia darasani.
Kuna siku hadi mwalimu alikataa kufundisha maana darasa halikuwa na muonekano wa darasa.
Shule gani?
 
Wapuuzi walikuwa wanabandika picha na matangazo hadi kwenye mabasi yao.
 
Baraza la mitihani NECTA limesitisha utaratibu wa kutangaza shule bora na mwanafunzi bora wa matokeo ya kidato cha nne

Kaimu katibu Mtendaji wa Baraza la mitihani Tanzania NECTA Athumani Salumu Amasi amesema utaratibu huo wa kutangaza shule bora ulikuwa unazitangazia biashara baadhi ya shule

"Unamtaja mtu kwamba ameongoza katika kundi ambalo pamoja na kwamba wamefanya mtihani huo huo lakini hawakusoma katika mazingira yanayofanana, alafu sasa unampa sifa mtu mmoja"

Kuhusu kumtangaza mwanafunzi bora wa mtihani huo amesema hakuna tija katika hilo kwani hauwezi kumtangaza mwanafunzi mmoja katika ya wanafunzi wote Tanzania ambao huenda pia mazingira yao ya kusoma yalikuwa tofauti

Chanzo: EA Radio
shule za secret-harsh zimefeli hawataki kusema
 
Back
Top Bottom