NECTA yaacha Utaratibu wa Kutangaza Wanafunzi bora na Shule bora kwa Kidato cha 4

Nilichogundua humu wanaofurahia huo uamuzi ni wavaakobazi ambao shule zao huwa zinashika mkia miaka yote tangu nchi ipate uhuru,pia wanaona wivu na chuki wakiona zile za mtakatifu fulani zimeongoza.kwa kifupi wavaakobazi wamefichiwa aibu.

Katika mashindano yote lazima ajulikane mshindi na aliyepoteza ili mshindi apongezwe aliyepoteza atiwe moyo apambane zaidi.
Umeongea pumba
 
Kama tukiamua lugha iwe kiingereza toka chekechea basi walimu wengi sana wa shule za umma itabidi warudi kujifunza hiyo lugha. Walimu wengi hawajui kiingereza, hata wale wa somo la English huwa wanalifundisha kwa kiswahili.
Inawezekana. Tunaweza kuweka mkakati wa miaka 20 mbele. Kwamba tuanze sasa kutengeneza waalimu watakaoweza kutufanikishia hilo na ndani ya miaka 20 tuwe tayari tupo kwenye right track.
 
Eeh Mungu tunashukuru,kidogo watuulie watoto kwa vipigo!! Watoto walikuwa wanasomea ufaulu wa mitihani tu, ambacho si maana kamili ya elimu, wanafunzi walikuwa wanapigwa vya kutosha ili wapate 100% kwenye tests na mitihani, hata mtu akipata 97 ni anachapwa tu.
Kuwaongezea pia muda wa kuwa darasani hasa madarasa ya mitihani darasa la nne, saba, form 2 na four ni kulala madarasani.Na kulazimishia boarding madarasa ya mitihani.
 
Dah. Wengine tuliutafuta uTO kwa udi na uvumba tukachemka.
Darasa letu la form six PCB liligeuka bweni. Watu walihamishia hadi mabegi darasani. Sahani, pasi, ndoo za kuogea zote zilihamia darasani. Hadi mashuka tulikuwa tunafua na kuanikia darasani.
Kuna siku hadi mwalimu alikataa kufundisha maana darasa halikuwa na muonekano wa darasa.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kubundi kwa sanaaaa.
 
Ahsanteeeee sanaaa, hakika hapa wame upiga mwingiii. Kongolee kwa watendaji wa hili jamboo.
 
Baraza la mitihani NECTA limesitisha utaratibu wa kutangaza shule bora na mwanafunzi bora wa matokeo ya kidato cha nne

Kaimu katibu Mtendaji wa Baraza la mitihani Tanzania NECTA Athumani Salumu Amasi amesema utaratibu huo wa kutangaza shule bora ulikuwa unazitangazia biashara baadhi ya shule

"Unamtaja mtu kwamba ameongoza katika kundi ambalo pamoja na kwamba wamefanya mtihani huo huo lakini hawakusoma katika mazingira yanayofanana, alafu sasa unampa sifa mtu mmoja"

Kuhusu kumtangaza mwanafunzi bora wa mtihani huo amesema hakuna tija katika hilo kwani hauwezi kumtangaza mwanafunzi mmoja katika ya wanafunzi wote Tanzania ambao huenda pia mazingira yao ya kusoma yalikuwa tofauti

Chanzo: EA Radio
My nigga nigga 😅sing all 🎵
 
Iliboru siyo ya mchezo kabisa. Yaani division 1 zipo 100 na division 2 ipo Moja . Hiyo ni shule hasa
Hapo wanaosoma ni Top cream katika mitihani yaTaifa nchi nzima.

Mazingira Mazuri

Motisha nzuri

Uwekezaji mkubwa katika vifaa vya kujifunza na kufundishia

Lakini KUBWA zaidi ni Walimu, serikali na wanafunzi kutambua kuwa ni shule KUBWA ibayohitajika kuwa ya Mfano katika mambo yote ya kishule nchini.
 
Baraza la mitihani NECTA limesitisha utaratibu wa kutangaza shule bora na mwanafunzi bora wa matokeo ya kidato cha nne

Kaimu katibu Mtendaji wa Baraza la mitihani Tanzania NECTA Athumani Salumu Amasi amesema utaratibu huo wa kutangaza shule bora ulikuwa unazitangazia biashara baadhi ya shule

"Unamtaja mtu kwamba ameongoza katika kundi ambalo pamoja na kwamba wamefanya mtihani huo huo lakini hawakusoma katika mazingira yanayofanana, alafu sasa unampa sifa mtu mmoja"

Kuhusu kumtangaza mwanafunzi bora wa mtihani huo amesema hakuna tija katika hilo kwani hauwezi kumtangaza mwanafunzi mmoja katika ya wanafunzi wote Tanzania ambao huenda pia mazingira yao ya kusoma yalikuwa tofauti

Chanzo: EA Radio
Binafsi bado sijashawishiwa na hizo sababu za kusitisha huo utaratibu, nilitamani wauboreshe badala ya kusitisha.

Kwanini, nasema hivyo. Sababu zangu ni hizi hapa.

1. Utaratibu ule uliongeza ushindani na kuchochea uwajibikaji miongoni mwa wamiliki, walimu na wanafunzi.

2. Ulichochea ubora katika utoaji wa elimu.

3. Uliwapa wahusika (serikali, taasisi binafsi, wazazi na wanafunzi) tathmini ya haraka na uhakika kujua walipotokea, walipo na wanapoelekea kielimu kulinganisha na wengine waliofanikiwa au kuanguka.

Kiujumla ule utaratibu ulikuwa unaleta Vibe ya kipekee katika masuala ya elimu.
 
Baraza la mitihani NECTA limesitisha utaratibu wa kutangaza shule bora na mwanafunzi bora wa matokeo ya kidato cha nne

Kaimu katibu Mtendaji wa Baraza la mitihani Tanzania NECTA Athumani Salumu Amasi amesema utaratibu huo wa kutangaza shule bora ulikuwa unazitangazia biashara baadhi ya shule

"Unamtaja mtu kwamba ameongoza katika kundi ambalo pamoja na kwamba wamefanya mtihani huo huo lakini hawakusoma katika mazingira yanayofanana, alafu sasa unampa sifa mtu mmoja"

Kuhusu kumtangaza mwanafunzi bora wa mtihani huo amesema hakuna tija katika hilo kwani hauwezi kumtangaza mwanafunzi mmoja katika ya wanafunzi wote Tanzania ambao huenda pia mazingira yao ya kusoma yalikuwa tofauti

Chanzo: EA Radio
Acha uongo
 
Dah. Wengine tuliutafuta uTO kwa udi na uvumba tukachemka.
Darasa letu la form six PCB liligeuka bweni. Watu walihamishia hadi mabegi darasani. Sahani, pasi, ndoo za kuogea zote zilihamia darasani. Hadi mashuka tulikuwa tunafua na kuanikia darasani.
Kuna siku hadi mwalimu alikataa kufundisha maana darasa halikuwa na muonekano wa darasa.
Mlitusua sasa
 
Inawezekana. Tunaweza kuweka mkakati wa miaka 20 mbele. Kwamba tuanze sasa kutengeneza waalimu watakaoweza kutufanikishia hilo na ndani ya miaka 20 tuwe tayari tupo kwenye right track.
Na ndiko tunakoelekea. Mpango wa MEWAKA (Mafunzo Endelevu kwa Walimu Kazini) utawaimarisha walimu katika eneo hili la lugha na ufundishaji.

Shule binafsi zijiandae miaka kumi ijayo wanaweza kukosa wanafunzi kama ilivyo katika vyuo vya ualimu vya binafsi. Iwapo lugha itakuwa ya Kiingereza Msingi, idadi ya wazazi watakaopeleka watoto wao huko itapungua.
Leo wazazi wengi waliosomesha watoto elimu ya msingi English Medium wanatafuta nafasi katika shule za boarding za serikali kwa sababu wanaamini mtoto akimasta lugha hiyo, ufaulu sekondari ni hakika.
 
Back
Top Bottom