MastaKiraka
JF-Expert Member
- Jan 10, 2015
- 5,736
- 18,648
🤣🤣🤣🤣 mimi binafsi maisha ya Advanced nili enjoy sana na PCM yangu, sikuwahi kuingia darasani isipokuwa siku za mitihani tu, Mtihani wa Mock nikalamba Sifuri safi, madogo wa form five wakaanza kunicheka sana, niliwaambia mimi natafuta div 3 tu ya point 13 nikasome zangu DIT, kama miujiza vile Necta form 6 nikapata 3.13 madogo walionicheka ndio wakawa wakwanza kunitumia matokeoDah. Wengine tuliutafuta uTO kwa udi na uvumba tukachemka.
Darasa letu la form six PCB liligeuka bweni. Watu walihamishia hadi mabegi darasani. Sahani, pasi, ndoo za kuogea zote zilihamia darasani. Hadi mashuka tulikuwa tunafua na kuanikia darasani.
Kuna siku hadi mwalimu alikataa kufundisha maana darasa halikuwa na muonekano wa darasa.