NECTA yatangaza matokeo ya kidato cha nne 2024. Yatazame hapa!
Sisi tunaamini kwenye hatma baada ya makaratasi na sio kiingereza kukiongea coz kiingereza sio hela Wala pesa ya kununulia chai!!

We nenda kariakoo ongea kiingereza kama utapata Hela ya kula!!
Ondoka kwenye utumwa mkuu wa makaratasi hebu Rudi pale bustani ya Eden "itunzeni na kuipalilia bustani"

Leo muuza mchicha ana tamba mbele ya Graduate aliejazwa ujinga wa theory kichwani coz amerudi Eden Na kulifuata agizo la Mungu kuitunza na kuipalilia Bustani na kitaa anatamba sana!
Jifariji.
 
Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa Kidato cha Nne uliofanyika kuanzia Novemba 11 hadi Novemba 29, 2024.

Matokeo hayo yametolewa rasmi leo, Alhamisi, Januari 23, 2025, na Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Said Mohammed.

Wanafunzi pamoja na wazazi sasa wanaweza kuyaona matokeo hayo kupitia tovuti rasmi ya NECTA.

Bonyeza hapa kutazama matokeo ya kidato cha nne mwaka 2024/2025

Hongera kwa waliofanikiwa, na kwa wale ambao hawakufikia malengo, bado kuna nafasi ya kujifunza na kufanikiwa zaidi!

===================================================

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limezuia matokeo ya wanafunzi 459 wa kidato cha nne mwaka 2024 kwa sababu mbalimbali zilizosababisha wasifanye mitihani yote.

Hata hivyo wanafunzi hao wamepewa fursa ya kurudia mitihani ya kidato cha nne mwaka huu 2025.

Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk Said Mohamed, akitangaza matokeo ya kidato cha nne leo Alhamisi Januari 23, 2025 amesema wanafunzi hao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mitihani ya kidato cha nne kwa masomo yote au idadi kubwa ya masomo.

Aidha, Baraza la Mitihani limetangaza kufuta matokeo ya wanafunzi 67 wakiwemo watano walioandika matusi kwenye mitihani.

Dk Said Mohammed amesema wanafunzi hao wameandika matusi ni tatizo la maadili.

“Maadili, matusi hayakubaliki chumba cha mtiani na kila mahali, mwaka huu wametokea wanafunzi watano wameandika matusi,”
Toka wameacha kupanga wanafunzi walioongoza,shule na Mikoa zoezi la kutangaza limekosa vibes ,binafsi Huwa sifuatilii tena
 
Ki-ukweli sizikandii kabisa EMS hata kidogo, nazikubali kwa asilimia kubwa sanaa. Ila nilipofika chuo ndo nilipokutana na maajabu waliokuwa wanakimbiza almost walikuwa wametoka St Kayumba, wengi wa waliotoka Private walikuwa wababaishaji. Sass sijui nini hutokea hapo katikati
Spoon feeding
 
Nawaza hapa naanzaje kumwambia huyu ndugu yangu matokeo ya kijana wake..

Maana alikua anamsifia Ila muda huu kanambia pia kanipa namba za shule nimwamgalizie..

Nafikilia naanzaje kumweleza haya matokeo ya first born wake 😔😔😔
Ni huzuni sanaaa, huzuni kiasi au huzuni kawaida?
 
Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa Kidato cha Nne uliofanyika kuanzia Novemba 11 hadi Novemba 29, 2024.

Matokeo hayo yametolewa rasmi leo, Alhamisi, Januari 23, 2025, na Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Said Mohammed.

Wanafunzi pamoja na wazazi sasa wanaweza kuyaona matokeo hayo kupitia tovuti rasmi ya NECTA.

Bonyeza hapa kutazama matokeo ya kidato cha nne mwaka 2024/2025

Hongera kwa waliofanikiwa, na kwa wale ambao hawakufikia malengo, bado kuna nafasi ya kujifunza na kufanikiwa zaidi!

===================================================

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limezuia matokeo ya wanafunzi 459 wa kidato cha nne mwaka 2024 kwa sababu mbalimbali zilizosababisha wasifanye mitihani yote.

Hata hivyo wanafunzi hao wamepewa fursa ya kurudia mitihani ya kidato cha nne mwaka huu 2025.

Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk Said Mohamed, akitangaza matokeo ya kidato cha nne leo Alhamisi Januari 23, 2025 amesema wanafunzi hao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mitihani ya kidato cha nne kwa masomo yote au idadi kubwa ya masomo.

Aidha, Baraza la Mitihani limetangaza kufuta matokeo ya wanafunzi 67 wakiwemo watano walioandika matusi kwenye mitihani.

Dk Said Mohammed amesema wanafunzi hao wameandika matusi ni tatizo la maadili.

“Maadili, matusi hayakubaliki chumba cha mtiani na kila mahali, mwaka huu wametokea wanafunzi watano wameandika matusi,”
Kwa mara nyingine Wasichana wamewapelekea moto Vijana wa Kiume,huko tuendako itakuwa kawaida women empowerment imefaulu 👇👇

View: https://www.instagram.com/p/DFKe07-IfMh/?igsh=MWxnYXM4NHAxZ3cybA==
 
Mtoto wako hajafanya vizuri?
Hapana ni First born wa shemeji yangu..
Kuhusu Mimi kwenye ukoo wetu hususani baba zangu wotee...ukoo wa mama wotee..
Pia kwenye tumbo letu katika watoto wa Tano mama alio wazaa hakuna AMBAE amewai ku fail kielimu na wote Wana degree na wote Wana Maisha yao.......last born wetu ndio kamaliza udsm hapo last year so kuhusu elimu hio sekta tupo vizuri
Kwaio Mimi automatically siwezi kuzaa mtoto kilaza 😊😊
 
Back
Top Bottom